Maisha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Maisha ni muda ambao kiumbe hai anajaliwa kuishi. Ni hali tofauti kabisa na uzima wa milele, kwa kuwa uhai wake una mwanzo na mwisho.

Hasa mwisho unasababisha maswali: kama kila chenye mwanzo kina mwisho, ya nini kuwepo kwake? Kukosa lengo, kuwepo bure, kutokuwa na maana kunamfanya mtu ajisikie mnyonge, pengine akate tamaa ya kuishi, la sivyo ajitose kufurahia mazuri yanayopatikana maishani, lakini bila uwezo wa kuondoa moyoni ule utupu wa maana unaomtia huzuni ya dhati.

Ndiyo sababu maana ya maisha ni mojawapo kati ya masuala makuu ya binadamu duniani: hawezi kukwepa maswali ya kutoka moyoni mwake kuhusu thamani, madhumuni na umuhimu wa maisha yake.

Suala hilo linaweza kujitokeza kwake katika maswali mengi tofauti yanayohusiana, kama vile: "mbona tumekuwepo?"; "maisha yanahusu nini?" na "nini maana ya hayo yote? Binadamu anajiuliza maswali kama hayo hasa anapokabiliana na kifo, kwa mfano msiba wa ndugu au rafiki.

Hilo limekuwa suala kuu la udadisi wa sayansi, falsafa na dini tangu zamani. Hivyo kumekuwa na idadi kubwa ya majibu kutoka asili mbalimbali kadiri ya itikadi na utamaduni.

Marejeo

Viungo vya nje