Nenda kwa yaliyomo

Maana ya maisha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tumetoka Wapi? Sisi ni Nani? Tunakwenda Wapi?
Mmojawapo kati ya michoro maarufu ya msanii Paul Gauguin wa kipindi cha baada ya uimpreshonisti.

Maana ya maisha ni mojawapo kati ya masuala makuu kuhusu thamani, madhumuni na umuhimu wa binadamu kuwepo duniani na wa maisha kwa jumla. Suala hilo linaweza kujitokeza katika maswali mengi tofauti yanayohusiana, kama vile Mbona tumekuwepo?, Maisha yanahusu nini? na Ni nini maana ya haya yote?

Binadamu anajiuliza maswali kama hayo hasa anapokabiliana na kifo, kwa mfano msiba wa ndugu au rafiki.

Limekuwa suala kuu la udadisi wa sayansi, falsafa na teolojia tangu zamani. Kumekuwa na idadi kubwa ya majibu kwa maswali hayo kutoka asili mbalimbali kiitikadi na kiutamaduni.

Maana ya maisha imechanganyikana kwa undani na dhana za falsafa na imani za dini na hugusia masuala mengine mengi, kama vile ontolojia, tunu, kusudi, maadili, hiari, uwepo wa Mungu, roho, na kinachoendelea baada ya maisha haya kwisha.

Michango ya sayansi kawaida ni ya moja kwa moja na inaeleza uhalisia kutokana na mambo yanayopimika kuhusu ulimwengu; sayansi inatoa muktadha na mipaka kwa mazungumzo kuhusu mada zinazohusika.

Mbadala ni mtazamo wa kifalsafa unaokabili swali: "Ni nini maana ya maisha 'yangu'?" Thamani ya swali linalohusu kusudi la maisha huweza kuwiana na kuupata ukweli wa mwisho, au hisia za umoja na utakatifu.

Maswali na marejeo yake

Mwanafalsafa akitafakari alivyochorwa na msanii Rembrandt.

Maswali kuhusu maana ya maisha yameulizwa kwa njia mbalimbali zenye upana, yakiwemo yafuatayo:

  • Maana ya maisha ni nini? [18]
  • Cha maana na cha thamani maishani ni nini? [14][19]

Uchunguzi wa kisayansi

DNA ambayo ina maelekezo ya kijenitikia kwa ajili ya maendeleo na utendaji wa viumbe hai vyote.

Kwamba sayansi inaweza kutusaidia kuelewa zaidi masuala ya msingi (kama vile maana ya maisha) inazua mabishano mengi katika jamii za sayansi na falsafa ya sayansi.

Hata hivyo, sayansi inaweza kutupa muktadha fulani na huyaweka mipaka kadhaa mazungumzo kuhusu mada kama hizo.

Umuhimu wa kisaikolojia na thamani katika maisha

Sayansi huenda ikashindwa kutuambia nini ni cha thamani maishani, lakini baadhi ya fani zake hugusia maswali yanayohusiana: watafiti katika saikolojia chanya hutafuta sababu zinazoleta hali ya ndani ya 'kuridhika na maisha',[22] kujihusisha kikamilifu katika shughuli,[23] kutoa mchango mkubwa zaidi kwa kutumia vipawa vya binafsi,[24][25]n.k.

Aina moja ya mfumo wa thamani iliyopendekezwa na wataalamu wa elimunafsia ya jamii, iitwayo kwa upana "Nadharia ya Kupambana na Mambo ya Kutisha", inasema kwamba maana yote ya binadamu inatokana na hofu ya msingi ya kifo, ambapo maadili yanachaguliwa yanapotusaidia kuepukana na kumbukumbu ya kifo.

Sayansi ya nyurolojia imetunga nadharia ya malipo, raha na msukumo katika masuala ya kimwili kama shughuli za kupitisha ujumbe za kinyuro. Ikiwa mtu anaamini kwamba maana ya maisha ni kufanya raha ziwe nyingi iwezekanavyo, basi nadharia zinatoa utabiri unaozidi kuongezeka, kuhusu jinsi ya kufanya ili kufanikisha hilo.

Somo la kijamii linapima thamani katika ngazi ya kijamii kwa kubuni nadharia kama vile nadharia ya thamani kanuni n.k.

Asili na hali ya maisha kibiolojia

Nadharia ya mageuko ya spishi haijaribu kuelezea asili ya uhai, bali mchakato ambao viumbe tofauti vimepitia katika kipindi chote cha historia ya dunia kupitia mabadiliko ya ghafla ya kijenetikia na uteuzi wa kiasili[26] Mwishoni mwa karne ya 20, kwa kuzingatia ufahamu wa mabadiliko ya viumbehai unaotegemea jeni hasa, wanabiolojia George C. Williams, Richard Dawkins, David Haig na wengineo, walihitimisha kwamba ikiwa kuna kazi msingi ya maisha, ni kujinakilisha kwa DNA na kuendelea kuwa hai kwa jeni za mtu.[27][28]

Ingawa wanasayansi wameyachunguza maisha yalivyo duniani, kuyafafanua bayana bado ni changamoto.[29][30][31][32][33][34]

Wanabiolojia kwa jumla wanakubaliana kwamba viumbe mbalimbali ni mifumo inayojipanga inayosimamia mazingira ya ndani ili kudumisha hali hii ya mpango, shughuli za kimetaboli hutumika kutoa nishati, na uzazi unaruhusu uhai kuendelea kwa vizazi vingi. Kwa kawaida, umbile huwa sikivu kwa uchochezi na habari za kijenetikia, hivyo huelekea kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi ili kuruhusu marekebisho kupitia mabadiliko ya mwili. Sifa hizo huongeza nafasi ya kuishi ya kiumbe binafsi na wazao wake kwa mtiririko huo.[35][36]

Viwakala visivyokuwa vya seli vinavyozaana, hasa virusi, kwa jumla havitazamwi kama viumbehai kwa sababu haviwezi kuzaana kwa "kujitegemea" au kuendesha shughuli za kimetaboliki. Pambano hilo ni tatizo, ingawa baadhi ya vimelea na visimbayonti vya ndani ya mwili pia vinaweza kuishi kwa kujitegemea.

Astrobiolojia inajihusisha na uwezekano wa kuwa na aina tofauti ya viumbe hai katika ulimwengu mwingine, kama vile miundo ya kujinakilisha kutoka vifaa vingine visivyo DNA.

Asili na hatima ya ulimwengu

Upanuzi wa kimetriki wa nafasi. Enzi ya kupanda ni kupanuka kwa kivuto cha kimetriki kilichoko upande wa kushoto.

Ingawa dhana ya Mlipuko mkuu ilipotolewa mara ya kwanza ilipambana na shaka kwa wingi, pia kutokana na uhusiano na imani ya dini ya uumbaji, baadaye imekuja kuungwa mkono na uchunguzi kadhaa wa kujitegemea.[37] Hata hivyo, fizikia ya sasa inaweza kuelezea tu ulimwengu ulivyokuwa mapema, sekunde 10 baada ya kutokea. Wanafizikia wengi wamedadisi nini inaweza kuwa imetangulia, na jinsi ulimwengu ulivyoanza.[38] Baadhi ya wanafizikia hudhani kuwa Mlipuko mkuu ulitokea kwa bahati tu, pamoja na uwepo wa ulimwengu maridhawa.[39]

Hata hivyo, haijalishi jinsi ulimwengu ulivyokuja kuwepo, hatima ya binadamu katika ulimwengu huu ni maangamizi kwani - hata kama ubinadamu utaishi muda mrefu - uhai wa kibiolojia hatimaye yatashindwa kujiendeleza.[38]

Maswali ya sayansi kuhusu akili

Hali ya kweli na asili ya fahamu na akili yenyewe pia vinajadiliwa sana katika sayansi. Suala la hiari pia linaonekana kuwa na umuhimu wa msingi. Masuala hayo hupatikana zaidi katika nyanja za sayansi koginitivu, nyurolojia na falsafa ya akili, ingawa baadhi ya wanabiolojia wa maendeleo ya uhai na wanafizikia wa kinadharia pia wameliashiria sana suala hilo.[40][41][42][42] mara nyingi zikijumuisha idadi kubwa ya mitazamo ya ziada.[43]

Kuinuka kwa Watakatifu ni picha iliyochorwa na msanii Hieronymus Bosch. Inaonyesha sehemu inayofanana na pango lenye mwanga na watu wa kiroho, mara nyingi hutajwa katika ripoti za waliokikaribia kifo.

Mbinu nyingine, kwa vile Mfano wa Rasimu Nyingi, hudai kwamba fahamu inaweza kuelezwa kikamilifu na nyurolojia, kupitia utendaji kazi wa ubongo na nyuroni zake.[41][44][45]

Nadharia za sumakuumeme za fahamu zinasema eneo la sumakuumeme linalotokana na ubongo ndilo hasa linalobeba fahamu zoefu. Hata hivyo kuna kutokubaliana kuhusu kutekelezwa kwa nadharia kama hiyo inayohusu utendaji kazi kwingine kwa akili.[46][47]

Nadharia za akili za kikwontamu hutumia nadharia ya kwontamu kuelezea baadhi ya sifa za akili. [48][49][48][50]

Ikitegemea hoja ya maelezo ya akili yasiyoweza kugusika, baadhi ya watu wamependekeza uwepo wa fahamu ya kikosmiki, wakidai kwamba fahamu kwa kweli ndiyo "msingi wa yote kuwepo".[16][49][51] Wanaounga mkono mtazamo huo wanaelezea matukio yasiyo ya kawaida, hasa uwezo wa kuhisi usio wa kawaida na uwezo wa kuyasoma mawazo, kama ushahidi wa uwepo wa fahamu ya juu isiyoeleweka. Ili kuthibitisha uwepo wa mambo hayo yasiyo ya kawaida, wanaelimunafsia wa mambo yasiyo ya kawaida wamefanya majaribio mbalimbali. Uchambuzi unaoangalia mambo yote yaliyopo unaonyesha kuwa asilimia ya wenye nguvu zisizo za kawaida (ingawa ndogo sana) imebaki thabiti.[52] Ingawa baadhi ya wachambuzi wakosoaji wanahisi somo la elimunafsia isiyo ya kawaida kuwa sayansi, hawaridhishwi na matokeo ya majaribio yake.[53][54] Wanaochunguza mambo haya upya, wanabaki na wasiwasi kwamba matokeo yanayoonekana kuwa na mafanikio huenda yakawa yanatokana na utaratibu mbaya, na watafiti wasiokuwa na mafunzo ya kutosha, au mbinu hafifu.[55][56][57][58]

Mitazamo ya kifalsafa

Mitazamo ya falsafa kuhusu maana ya maisha ni itikadi ambazo huelezea maisha kupitia suala la maadili au dhana zinazofafanuliwa na binadamu.

Falsafa za Kale za Ugiriki

Plato na Aristotle katika Shule ya Athene, mchoro wa ukutani wa msanii Raffaello.

Uplato

Plato alikuwa mmoja wa wanafalsafa wa mwanzo, na mwenye ushawishi mwingi hadi leo, hasa kwa uhalisia kuhusu uwepo wa malimwengu. Katika Nadharia ya Maumbo, malimwengu hayapo kimwili, lakini yapo katika maumbo ya kimbingu. Katika Jamhuri mazungumzo ya mhusika wa mwalimu wake Sokrates yanaelezea Umbo la Zuri, jambo la kimaadili, hali kamili ya uzuri, hivyo basi kipimo cha ujumla cha haki. Katika falsafa ya Plato, maana ya maisha ni kufikia umbo la juu zaidi la elimu, ambalo ni Umbo la Zuri, ambapo mambo yote mema na ya haki yanatoa umuhimu na thamani. Binadamu wana wajibu wa kuyatekeleza mazuri, lakini hakuna yeyote anayeweza kufanikiwa katika harakati hiyo bila fikira za kifalsafa, ambazo zinaruhusu elimu ya kweli.

Uaristoteli

Aristotle, mwanafunzi wa Plato, alikuwa mwanafalsafa mwingine wa mapema, mwenye ushawishi mkubwa, ambaye alisema kuwa maarifa ya maadili si ya hakika kama metafizikia na somo la maarifa, lakini ni maarifa ya kijumla. Kwa sababu si fani ya kinadharia, inambidi mtu asome na afanye mazoezi ili awe 'mzuri', kwa hiyo mtu angekuwa mwema, hangeweza kusoma tu fadhila ni nini, ingembidi awe na fadhila, kupitia juhudi za kiadili. Kufanya hili, Aristotle alifafanua kitendo kilicho cha fadhila: "Kila tajriba na kila swali, na vilevile kila tendo na chaguo la tendo, linadhaniwa kuwa na uzuri fulani kama lengo lake. Ndiyo sababu lile zuri limefafanuliwa ifaavyo kama lengo la bidii yote [...]
Kila kitu hufanywa na lengo, na lengo hilo ni "zuri". (Maadili ya Kinikomakea 1.1).

Hata hivyo, ikiwa kitendo A kinafanyika ili kufikia lengo B, kisha lengo B pia litakuwa na lengo (lengo C), na lengo C pia litakuwa na lengo, hivyo muundo huo utaendelea mpaka kitu kiusimamishe. Suluhisho la Aristotle ni Wema mkuu, ambao ni wa kuwaniwa kwa ajili yake pekee, ni lengo lake lenyewe. Wema mkuu hauwaniwi kwa ajili ya kufikia mema mengine, na mema yote yanawaniwa kwa ajili yake. Hili linahusisha kufikia "eudemonia", ambayo kwa kawaida hutafsiriwa kama "furaha", "ustawi", "kutokosa chochote muhimu", na "ubora".

Falsafa ya Shaka

Katika Ugiriki ya Kale wanafalsafa wa shaka walisema kuwa lengo la maisha ni kuishi kwa fadhila yanayowiana na viumbe wengine. Furaha inatokana na kujitegemea na kuusimamia mtazamo wa kiakili; mateso yanatokana na maamuzi ya uongo kuhusu thamani, ambayo husababisha hisia mbaya na tabia ya uhasama.

Maisha ya shaka yanakataa tamaa za kawaida za mali, nguvu, afya, na umaarufu, kwa kuwa huru kutoka vitu vinavyopatikana katika kuyatafuta ya kawaida.[59][60] Kama viumbe wenye uwezo wa kufikiria, watu wanaweza kufanikisha furaha kupitia mafunzo kabambe, kwa kuishi katika njia iliyo ya kiasili kwao. Dunia ni ya kila mtu kwa kiwango sawa, hivyo mateso yanasababishwa na uamuzi wa uongo kuhusu kile ambacho ni cha thamani na kile ambacho hakina maana kulingana na tamaduni na itikadi za jamii.

Ukurene

Falsafa ya Ukurene, iliyoanzishwa na Aristipo wa Kurene, ilikuwa shule ya zamani ya Kisokrate iliyotia maanani upande mmoja tu wa mafundisho ya Sokrates - kwamba furaha ni tokeo la mwisho la hatua za kimaadili na kwamba radhi ni zuri kuu; hivyo basi mtazamo wa dunia wa kuipenda raha pekee ambapo kutimiza tamaa za mwili ni za faida kuliko radhi ya akili. Wakurene walipendelea kutimiza tamaa haraka kuliko faida inayopatikana baada ya kusubiri kipindi kirefu; kunyimwa ni huzuni mbaya.[61][62]

Uepikuro

Mchongo wa Epikuro akimuegemea mwanafunzi wake Metrodorus katika makavazi ya Louvre.

Kwa Epikuro, jambo zuri kuliko yote ni kutafuta raha za wastani, kupata utulivu na kuwa huru kutoka hofu (“ataraxia”) kupitia maarifa, urafiki na wema, kuishi kwa kujichunga; maumivu ya kimwili (“aponia”) hayapo kupitia maarifa ya mtu kuhusu hali ya dunia na mipaka ya matamanio ya mtu. Vikiwa pamoja, uhuru kutoka maumivu na uhuru kutoka hofu ndiyo furaha kuu. Kukusifu kwake kufurahia anasa ambazo hazijapita kiasi kunakaribia dhana ya "kujiepusha" na raha zote kama vile ngono na anasa:

Tunaposema... kuwa radhi ndio mwisho na lengo, hatumaanishi raha za upotevu au raha za kimwili, jinsi tunavyoeleweka na wachache kwa ujinga, ubaguzi au udanganyifu wa makusudi. Tukisema radhi tunamaanisha kutokuwepo kwa maumivu mwilini na taabu katika nafsi. Si kwa mfululizo wa ulevi na kuponda raha, si kwa tamaa ya ngono, wala kufurahia utamu wa samaki, na vyakula vingine vitamu kutoka meza iliyojaa vinono, ambavyo huzalisha maisha mazuri; ni fikira za kimakini, kutafuta nje ya misingi ya kila uchaguzi na kuepuka, na kuikataa mitazamo ambayo hufanya shida kubwa kuichukua nafsi.[63]

Maana ya Kiepikuro ya maisha inakanusha kutokufa na dhana ya maisha mengine mbali na haya ya duniani; kuna nafsi, lakini inaweza kufa kama mwili. Hakuna maisha baada ya kifo, ingawa mtu hatakiwi kuogopa kifo, kwa sababu "Kifo si chochote kwetu, kwani yale ambao hunywea, ni bila hisia, na kile ambacho hakina hisia si chochote kwetu."[64]

Falsafa ya uvumilivu

Falsafa ya uvumilivu hufunza kwamba kuishi kulingana na fikira njema ni kuwa katika uwiano na mpango wa ulimwengu wa Kimungu, unaotokana na mtu kufahamu logos, fikira ya ulimwengu wote, thamani muhimu inayopatikana kwa wote. Maana ya maisha ni uhuru kutoka mateso (kwa Kigiriki: απαθεια, apatheia ). Mashauri ya moja kwa moja ya falsafa ya uvumilivu ni fadhila, fikira na sheria ya kimaumbile, zinazojumuisha kuendeleza kujidhibiti kibinafsi na ujasiri wa kiakili kama njia za kuzishinda hisia haribifu. Mwenye kuifuata falsafa ya uvumilivu hanuii kuzizima hisia, bali kuepuka shida za kihisia, kwa kuendeleza uamuzi wazi na utulivu wa ndani kupitia uzoefu makini wa kimantiki, kutafakari, na kuziweka fikira pamoja.

Msingi wa kimaadili wa falsafa ya uvumilivu ni kuwa "zuri liko katika hali ya nafsi", yenyewe inaonyeshwa katika hekima na kujidhibiti, hivyo kuboresha ustawi wa kiroho: "Fadhila" inatokana na "nia" ambayo inawiana na maumbile."[64] Kanuni inatumika katika uhusiano wa kibinafsi, yaani: "kuwa huru kutokana na hasira na wivu".[64]

Falsafa ya Mwangaza

Enzi ya Kutaalamika na ile ya ukoloni zote mbili zilibadilisha hali ya falsafa ya Ulaya na kuieneza duniani kote. Ibada na kumnyenyekea Mungu viligeuka kuwa dhana za haki za binadamu zisizoweza kunyimwa na dhana ya uwezo wake mkuu wa kifikira. Maadili ya ulimwengu mzima ya upendo na huruma yaligeuka dhana za kiraia za uhuru, usawa, na uraia. Maana ya maisha pia yalibadilika, ikiacha kidogo kuhimiza uhusiano na Mungu na kusisitiza uhusiano kati ya watu binafsi na jamii yao. Kipindi hicho kilijaa nadharia zinazolinganisha kuwepo kwa maana na utaratibu wa kijamii.

Uhuru kutoka mipango ya kiuchumi ya jamii

Uhuru kutoka mipango ya kiuchumi ya kijamii ni seti ya mawazo yaliyoibuka katika karne za 17 na 18, kwa sababu ya migogoro iliyochukua nafasi kubwa barani Ulaya kati ya waliozidi kuwa matajiri, pamoja na utaratibu wa viongozi matajiri, na watu wa dini.

Uhuru kutoka mipango ya kiuchumi ya kijamii ulionyesha binadamu kama viumbe wenye haki walizozaliwa nazo na wasizowezwa kunyimwa (pamoja na haki ya mtu kubaki na mali inayotokana na kazi yake binafsi), na ulitafuta mbinu za kupima haki kuwa sawa katika jamii yote. Kijumla, uhuru binafsi ulitazamwa kuwa lengo kuu,[65] kwa sababu ya kudhani kwamba kupitia hakikisho la uhuru tu haki nyingine zilizojikita kwa ndani zitakapolindwa.

Kuna aina nyingi za dhana ya uhuru kutoka mipango ya kiuchumi ya kijamii, lakini dhana zao kuu kuhusu maana ya maisha zinaambatana na dhana tatu za msingi. Wanafalsafa wa awali kama vile John Locke, Jean-Jacques Rousseau na Adam Smith waliona binadamu akianza katika hali ya kimaumbile, kisha akitafuta maana kupitia ajira na mali, na kutumia mikataba ya kijamii ili kujenga mazingira ambayo yanasaidia juhudi hizo.

Ukanti

Immanuel Kant anafahamika kama mmoja wa wanafalsafa wenye ushawishi mwingi zaidi katika kipindi cha mwisho cha Kutaalamika.

Ukanti ni falsafa iliyo na msingi katika maandishi ya kimaadili, ya somo la maarifa na ya kimetafizikia ya Immanuel Kant. Kant anajulikana kwa nadharia ya uwajibikaji ambayo msingi ni wajibu mmoja wa kimaadili, "dhana ya lazima bila kujalisha", inayotokana na dhana ya uwajibikaji. Wakanti wanaamini kuwa vitendo vyote vinafanywa kulingana na lengo au kanuni fulani isiyobainika wazi, na kuwa ili vitendo viwe adili, ni lazima viambatane na dhana ya lazima bila kujalisha.

Kifupi, mtihani ni kwamba lazima mmoja afanye lengo litumike ulimwenguni kote, kisha angalia kama bado itawezekana kulitekeleza duniani. Katika kitabu chake, Kazi ya msingi, Kant anatoa mfano wa mtu ambaye anataka kukopa pesa bila nia ya kuzirudisha. Huu ni utata kwa sababu kama ingalikuwa hatua ya wote ulimwenguni, hakuna mtu ambaye angemkopesha mwingine, tena kwani yeye angejua kwamba hangerudishiwa pesa hizo. Lengo la hatua hii, anasema Kant, linaleta matokeo ya mkanganyiko katika matazamio (na hivyo linapingana na wajibu kamili).

Kant pia alikanusha kwamba matokeo ya tendo huchangia kwa njia yoyote thamani ya kimaadili ya tendo, hoja yake ikiwa kwamba ulimwengu wa kimwili upo nje ya udhibiti kamili wa mtu na hivyo mtu hawezi kuwajibika kwa matukio yanayofanyika hapo.

Falsafa za karne ya 19

Falsafa ya faida

Jeremy Bentham

Asili ya falsafa ya faida inaweza kurudi nyuma sana hadi Epikuro, lakini, kama shule ya mawazo, inahusishwa na Jeremy Bentham,[66] ambaye aligundua kuwa asili imemweka mtu chini ya utawala wa mabwana wawili wa kujitegemea, maumivu na raha. Basi, kutokana na busara hiyo ya kimaadili, na kuiunda Sheria ya Utumizi, kwamba wema ni chochote ambacho huleta furaha nyingi zaidi kwa idadi kubwa zaidi ya watu. Alifafanua maana ya maisha kama "kanuni ya furaha nyingi zaidi".

Jeremy Bentham aliungwa mkono sana na James Mill, mwanafalsafa muhimu katika siku zake, na baba yake John Stuart Mill. Mill mdogo alifunzwa kulingana na kanuni za Bentham, pamoja na kunakili na kufupisha maandishi mengi ya baba yake.[67]

Umaksi

Kulingana na Umaksi na Ukomunisti, maana ya maisha ni kutumikiana katika amani na kwa uadilifu kama wanadamu walio sawa na wenye haki.

Ubatilivyote

Ubatilivyote ni falsafa inayokataa madai kuwa yeyote ana maarifa na ukweli, na hivyo inapeleleza umuhimu wa kuishi bila ukweli unaoweza kujulikana. Badala ya kusisitiza kwamba maadili yanabadilika kulingana na mtu, na huenda yasipewe sababu, mbatilivyote anasema: "Hakuna kitu chenye thamani", maadili hayana thamani, hutumika tu kama maadili bandii ya jamii.

Friedrich Nietzsche aliutambulisha ubatilivyote kama kuifanya dunia kuwa tupu, hasa kuhusu uwepo wa binadamu, wa maana, wa kusudi, wa ukweli wa kueleweka, na wa thamani muhimu; kwa ufupi, ubatili wa vyote ni mchakato wa "kuyafanya maadili makuu yasiwe na thamani".[68] Ubatilivyote ni kama matokeo ya wazo kwamba Mungu amekufa, na kusisitiza kwamba hicho ni kitu kilichokuwa kinafaa kushindwa.[69]

Kwa Friedrich Nietzsche, maisha ni ya thamani tu ikiwa kuna malengo yanayomshawishi mtu kuishi. Hivyo, aliona falsafa ya ubatilivyote ("yote ambayo hufanyika ni ubatili") kama bila malengo. Alikana kujiepusha na anasa, kwa sababu kufanya hivyo kunakanusha kuishi katika ulimwengu; alikanusha kuwa maadili ni malengo ya ukweli, ambayo kifikira ni ahadi za lazima zinazotumika ulimwenguni kote: tathmini zetu ni tafsiri, na si tafakari za dunia, kama ilivyo kwa kweli, na basi, dhana zote hufanyika kupitia mtazamo fulani.[69]

Mwisho wa Dunia, picha iliyochorwa na msanii John Martin.

Martin Heidegger, kama Nietzsche, aliona "kifo cha Mungu" kuwa chanzo cha ubatilivyote kuibuka:

Kama Mungu, ambaye ndiye lengo na msingi unaozidi yale yanayoweza kuhisika, na wa ukweli wote, amekufa; kama ulimwengu unaozidi yanayoweza kuhisika wa mawazo umeumizwa kwa kupoteza nguvu zake za lazima za kujijenga juu, na juu ya hayo, za kuipa nguvu zaidi, basi hakuna chochote kinachobaki ambacho mtu anaweza kushikilia, na ambacho anaweza tumia kuitafuta njia.[70]

[68] Heidegger,

Falsafa za karne ya 20

Kipindi cha sasa kimeyaona mabadiliko makuu katika dhana ya hali ya binadamu. Sayansi ya kisasa imefanikiwa kuandika upya uhusiano kati ya wanadamu na ulimwengu halisia, maendeleo katika matibabu na teknolojia yametufanya tuwe huru kutoka maradhi ya vipindi vya awali, na falsafa - hasa kufuatia mgeuko wa kilugha - ilibadilisha jinsi uhusiano kati ya watu unavyotazamwa.

Maswali kuhusu maana ya maisha pia yamekabiliwa na mabadiliko makuu, kutoka majaribio ya kutazama upya kuwepo kwa binadamu kupitia biolojia na sayansi kwa jumla (kama katika upragmatiki na uchanya wa kimantiki), hadi jitihada za kinadharia kuhusu kufanya maana kama shughuli (udhanaishi, utu wa kidunia).

Upragmatiki

Upragmatiki, ulianzishwa mwishoni mwa karne ya 19 nchini Marekani ukidokeza kwamba ukweli ni katika kukabiliana na mazingira tu na kwamba matokeo pia ni sehemu za ukweli. Isitoshe, upragmatiki unadokeza kwamba chochote muhimu na chenye vitendo si kweli daima, akisema kwamba kile ambacho huchangia zaidi mema ya binadamu wengi katika kipindi cha muda mrefu ndicho kweli. Katika mazoezi, madai ya kinadharia lazima yathibitishwe kwa vitendo, yaani lazima mtu aweze kutabiri na kupima madai, na kwamba, mwishowe, mahitaji ya watu yanapaswa kuongoza uchunguzi wa kisomi wa binadamu.

Wanafalsafa wa Kipragmatiki wanadokeza kwamba kuyaelewa maisha kupitia vitu vinavyotendwa ni muhimu kuliko kutafuta dhana ya kiakili ambayo ni vigumu kuwekwa katika vitendo kuhusu maisha. William James alisema ukweli unaweza kufanywa, lakini hauwezi kutafutwa.[71][72] Kwa Wapragmatiki, maana ya maisha yanajulikana tu kupitia uzoefu.

Udhanaishi

Kila mwanamume na kila mwanamke anaumba maana ya maisha yake; maisha hayadhamiriwi na Mungu mwenye nguvu kuliko binadamu au mamlaka ya kidunia, bali kila mtu yuko huru. Kwa hiyo, mambo muhimu yanayomuendesha mtu kimaadili ni vitendo, uhuru na uamuzi. Hivyo, udhanaishi unapinga ufikiriaji na uchanya. Katika kutafuta maana ya maisha, mdhanaishi anatazama mahali ambapo watu hupata maana ya maisha, ambapo katika kutumia fikira tu kama chanzo cha maana ni pungufu. Upungufu huibua hisia za wasiwasi na hofu, zinazohisika katika kukabiliana na uhuru mkuu, na kuambatana na mwamko kuhusu kifo. Kwa mdhanaishi, kuwepo kunatangulia kiini; kiini cha maisha ya mtu huja tu baada ya mtu kuwa.

Søren Kierkegaard aliunda neno "mruko wa kiimani", akidokeza kuwa maisha yamejaa mkanganyiko, na mtu lazima aunde maadili yake katika ulimwengu usiojali. Mtu anaweza kuishi maisha yenye maana (yasiyo na kukata tamaa wala wasiwasi) kwa kufanya ahadi kwa vyovyote kuhusu kitu kilicho na mwisho, na kujitolea kwa maisha hayo ya kufanya ahadi, licha ya mazingira magumu yaliyojikita katika kufanya hivyo.[73]

Arthur Schopenhauer alijibu: "Ni nini maana ya maisha?" kwa kubainisha kuwa maisha ya mtu yanaonyesha nia yake, na kwamba nia (maisha) kiendeshaji kisichokuwa na lengo, kisichofuata fikira na kinachokuwa chungu. Wokovu, ukombozi, na kuepuka mateso yamo katika kutafakari mambo mazuri, kuhurumia wengine, na kujieupusha na anasa.[74][75]

Ukanganyikaji

Albert Camus, mwanafalsafa wa Kifaransa toka Algeria, ambaye mara nyingi anahusianishwa na udhanaishi lakini alilikataa neno hilo kabisa,[76] ni maarufu kwa kudokeza nadharia yake ya mkanganyiko. Mkanganyo wa hali ya binadamu ni kwamba watu wanatafuta maadili ya nje na maana katika dunia ambayo haina maana yoyote, na ambayo haiwajali. Camus anaandika kuhusu wabatilivyote wa thamani kama Meusrault,[77] na pia kuhusu maadili katika ulimwengu wa kuyabatili yote, kwamba watu wanaweza badala yake kujitahidi kuwa "wabatilivyote wa kishujaa", wanaoishi na hadhi wanapopambana na mkanganyiko, kuishi kwa "utakatifu wa kidunia", mshikamano wa kindugu, na kuuasi na kupambana dhidi ya kutojali kwa dunia.[78]

Kulingana na ukanganyikaji, kuna ukosefu wa umoja wa kimsingi unaotokana na kuwepo kwa ushirikiano wa binadamu na ulimwengu. Mtu ana hamu ya mpango, maana, na kusudi katika maisha, lakini ulimwengu haujali na hauna maana; mkanganyo unatokana na mgogoro huu.

Kama viumbe vinavyotafuta matumaini katika dunia isiyokuwa na maana, Camus anasema kuwa binadamu wana njia tatu za kuutatua mtanziko.

  • Kujiua: ufumbuzi wa kwanza wa mtanziko ni mtu kuyakomesha maisha yake. Camus anakataa chaguo hili kama la woga.
  • Imani ya dini katika Ulimwengu Upitao Fikira: imani ya namna hiyo huenda ikadokeza kuwepo kwa ulimwengu ambao umezidi huu wa kukanganya, na, kwa hivyo, una maana. Camus anauita ufumbuzi huo "kujiua kifalsafa" na anaukataa kwa sababu ni sawa na kuangamizwa kwa fikira, ambayo kwa maoni yake ni janga sawa na kujiua kimwili.
  • Kukubali mkanganyo: kwa Camus, huu tu ndio ufumbuzi wa kweli. Ni kukubali na hata kukumbatia mkanganyo wa maisha na kuendelea kuishi. Mkanganyo ni tabia muhimu ya hali ya kibinadamu, na njia pekee ya kweli ya kukabiliana na hili ni kulikubali kwa ujasiri. Kulingana na Camus, tunaweza "kuishi maisha bora zaidi ikiwa hayana maana."[79]

Utu wa Kidunia

Picha ya "binadamu mwenye furaha" ishara ya Utu wa Kidunia.

Kulingana na Utu wa Kidunia, wanadamu walitokana na kuzaana katika maendeleo ya mabadiliko ambayo hayakuongozwa kama sehemu muhimu ya maumbile, ambayo huishi yenyewe.[80][81] Maarifa hayatoki katika vyanzo vyenye nguvu visivyo vya kawaida, lakini kutoka uchunguzi wa binadamu, majaribio, na uchambuzi wa kimantiki (mbinu ya kisayansi): asili ya ulimwengu ni kile ambacho watu huitambua kuwa hivyo.[80] Aidha, maadili na ukweli vinalengwa kwa njia ya uchunguzi wa kiakili[80] na yanatokana na mahitaji ya binadamu na hamu kama ilivyopimwa na uzoefu, yaani kupitia akili yenye uchambuzi.[82][83] "Kulingana na yale tunayojua, tabia za mtu kiujumla ni [chanzo] cha kiumbe cha kibiolojia kinachoendesha shughuli zake katika muktadha wa kijamii na wa kiutamaduni."[81]

Watu huamua kusudi la binadamu, bila ya ushawishi wa Kimungu; ni tabia ya binadamu, hisia ya kijumla, ambayo ni lengo la maisha ya binadamu. Utu wa Kidunia unataka kuendeleza na kutimiza ubinadamu:[80] "Utu husisitiza uwezo wetu, na uwajibikaji wetu, kuishi maisha adili yenye utimilifu wa binafsi yanayolenga mema makuu ya ubinadamu".[82] Wanautu huendeleza kufunguliwa kifikra ili kuyashughulikia maslahi ya binafsi na yenye manufaa kwa watu wote. Furaha ya mtu binafsi inahusishwa kwa njia isiyoweza kubadilishwa na ustawi wa binadamu wengine, kwa sababu sisi ni wanyama wanaolazimika kuishi katika jamii, ambayo hupata maana kutokana na uhusiano wa karibu, na kwa sababu maendeleo ya kiutamaduni humnufaisha kila mtu katika utamaduni.[81][82]

Falsafa ndogo za Utu wa Baadaye na Utu Unaopita Yote (ambazo wakati mwingine hutumiwa kimbadala) ni upanuzi wa maadili ya kiutu. Mtu anapaswa kutafuta maendeleo ya ubinadamu na ya maisha yote kwa kiasi kikubwa iwezekanavyo ili kupatanisha Utu wa Kirainasansi na utamaduni wa karne ya 20 wa sayasansi na teknolojia. Hivyo, kila kiumbe hai ana haki ya kuamua "maana ya maisha binafsi" kwa mtazamo wa kijamii na kibinafsi.[84] Kutoka mtazamo wa kiutu na kielimunafsia ya kupunguza maumivu, suala la maana ya maisha pia linaweza kutafsiriwa tena kama "Ni nini maana ya maisha "yangu"?"[85]

Badala ya kujifunga na swali la kidini au la kikozmiki kuhusu madhumuni makuu, mbinu hii inapendekeza kwamba swali hili ni la binafsi sana. Kuna majibu mengi ya kimatibabu ya kupunguza maumivu kwa swali hili, kwa mfano Viktor Frankl anadokeza kuwa dhana ya "Kutowaza", ambayo kwa kiasi kikubwa hutafsiriwa kama kukoma kutafakari bila mwisho juu ya ubinafsi, badala ya kujishughulisha na maisha. Kwa ujumla, mwitikio wa matibabu ya kuyapunguza maumivu ni kwamba swali la maana ya maisha huvukiza ikiwa mtu anajishughulisha kikamilifu na maisha. Swali kisha linabadilika kuwa wasiwasi maalum zaidi kama vile "Ni upotovu upi unaonisumbua?", "Ni nini kinachozuia uwezo wangu kufurahia vitu?", "Mbona mimi huwasahau wapendwa wangu?". Angalia pia Matibabu ya Kupunguza Maumivu ya Kidhanaishi kadiri ya Irvin Yalom.

Uchanya wa kimantiki

Wachanya wa kimantiki huuliza: Ni nini maana ya maisha? na Ya nini kuuliza?[86][87] Kama hakuna maadili yanayolengwa, basi, hiyo ni kusema maisha hayana maana?[88] Ludwig Wittgenstein na wachanya wa kimantiki walisema: "Linapoulizwa kilugha, swali ni batili"; kwa sababu, maishani taarifa ya "maana ya x", kawaida inaashiria madhara ya x, au umuhimu wa x, au kile ambacho ni dhahiri kuhusu x na kadhalika, kwa hivyo, wakati dhana ya maana ni sawa na "x", katika taarifa ya "maana ya x", taarifa inakuwa ya kujirudia, na kwa hiyo ya kipuuzi, au inaweza kutaja kama ukweli kwamba maisha ya kibiolojia ni muhimu ili kuwa na maana maishani.

Mambo (watu, matukio) katika maisha ya mtu yanaweza kuwa na maana kama sehemu ya uzima, lakini maana isiyobainika ya maisha hayo, yenyewe, mbali na mambo hayo, haiwezi kubainika. Maisha ya mtu yana maana (kwake mwenyewe na kwa wengine) kama matukio ya maisha yanayotokana na mafanikio yake, urithi, familia, na kadhalika, lakini, kusema kwamba maisha yenyewe yana maana ni matumizi mabaya ya lugha, kwani yoyote yaliyo muhimu, au ya mwisho, ni muhimu tu "katika" maisha (kwa walio hai), hivyo basi kuifanya taarifa iwe ya kimakosa. Bertrand Russell aliandika kwamba ingawa alipata kwamba chuki yake ya mateso haikuwa kama chuki yake ya mboga ya brokoli, hakupata utaratibu wowote wa kuridhisha, na wa kupimika wa kuthibitisha hili:[64]

Tunapojaribu kuwa na uhakika, kuhusu kile tunachomaanisha tunaposema kuwa hiki au kile ni "tunu", tunajikuta katika matatizo makubwa sana. Tamko la Bentham, kwamba radhi ndiyo Zuri, lilizua upinzani mkali, na ilisemekana kuwa falsafa ya nguruwe. Yeye na wapinzani wake walishindwa kuibua hoja zozote. Katika swali la kisayansi, ushahidi unaweza kupatikana kutoka pande zote mbili, na mwishowe, upande mmoja unabainika kuwa na hoja bora au, kama hili halitokei, swali linabaki kama halijajibiwa. Lakini katika swali, kuhusu ikiwa hili, au hilo, ndilo mwisho Mzuri, hakuna ushahidi, kwa vyovyote vile; kila mtetezi anaweza kupendekeza tu hoja kulingana na hisia zake, na kutumia vifaa vya ushawishi ambavyo vitaibua hisia sawa katika wengine... Maswali kuhusu "maadili" - yaani, kuhusu kile ambacho chenyewe ni kizuri au kibaya, bila kutilia maanani madhara yake - yanapatikana nje ya uwanja wa sayansi, jinsi watetezi wa dini wanavyodai kwa msisitizo. Nadhani kwamba, katika hili, wako sawa, lakini mimi napata hitimisho zaidi, ambalo hao hawapati, kwamba maswali kuhusu "maadili" yanapatikana kabisa nje ya uwanja wa maarifa. Hiyo ni kusema, tunaposema kwamba hili au lile lina "thamani", sisi tunaeleza tu hisia zetu wenyewe, si ukweli, ambao bado ungalikuwa kweli ikiwa hisia zetu za binafsi zingalikuwa tofauti.[89]

Baada ya Usasa

Falsafa ya Baada ya Usasa - tukizungumza kwa upana- inaona hali ya binadamu ikiwa kama iliyojengwa na lugha, au na miundo na taasisi za jamii ya kibinadamu. Ikitofautiana na aina nyingine za falsafa, ni nadra kwa falsafa ya Baada ya Usasa kutafuta maana zinazopatikana kabla ya tendo au zilizojikita kwa undani katika uwepo wa binadamu. Badala yake inalenga kuchunguza au kukosoa maana zilizopewa ili kuzitafakari au kuzirekebisha upya. Chochote kinachofana na 'maana ya maisha', katika maana ya falsafa hiyo, kinaweza kueleweka tu ndani ya muundo wa kijamii na wa kilugha, na lazima ufuatwe kama kimbilio kutoka miundo ya nguvu ambayo tayari imejikita katika aina zote za hotuba na mwingiliano.

Kama kanuni, wanafalsafa wa Baada ya Usasa wanatazama mwamko wa vikwazo vya lugha kama muhimu kuvikwepa vikwazo vivyo, lakini wananadharia tofauti wana maoni mbalimbali kuhusu asili ya mchakato huu: kutoka ujenzi wa dharura wa maana na watu binafsi (kama katika falsafa ya Kuharibu Yaliyojengwa) hadi kwa nadharia ambamo watu ni upanuzi wa kimsingi wa lugha na jamii, bila uhuru halisi (kama katika falsafa ya Baada ya Muundo). Kiujumla, falsafa ya Baada ya Usasa inatafuta maana kwa kuangalia miundo ya msingi ambayo inaunda au kulazimisha maana, kuliko yale yanayoonekana kiepifenomenali duniani.

Dhana ya Uhisia

Kulingana na dhana ya kihisia, maana kuu ya maisha ni kupata kutosheleza hisia za kibinadamu. Wafuasi wa falsafa hiyo wanaamini kuwa vitendo vyote maishani ni matokeo ya hisia na hasa haja ya kuzaa. Uwepo wa mtu binafsi huwa chanzo cha kuzaa na unamfanya binadamu kutafuta lengo la kuzaa maishani kwa kuufuata mzunguko. Haraka inasisitiza kuwa watu wanapofikiria kwa kina, watapata kuwa lengo kuu la matendo yote wafanyayo ni kuvutia watu wa jinsia nyingine. Dhana kuu ya uhisia inaweza kufuatwa hivi:

Kama inayokubalika kuwa watu hufunzwa kujifunza shuleni. Kwa nini tusome kwa bidii? Ili tufuzu mitihani. Kwa nini tufuzu mitihani? Ili tuweze kuenda chuo kikuu? Kwa nini tuweze kuenda chuo kikuu? Ili tuweze kupata kazi nzuri? Kwa nini tupate kazi nzuri? Ili tuwe na mali. Kwa nini tuwe na mali? Ili tununue magari mazuri; ili tununue nyumba nzuri; ili tununue bidhaa nzuri. Kwa nini vitu vyote vizuri kumfanya mtu aonekana mzuri? Mwishowe kuvutia watu wa jinsia nyingine, kutosheleza haja ya msingi ya kuzaa na kuendeleza familia ya kibinadamu.

Wanahisia hutumia mawazo hayo kuendeleza dhana kuwa matukio yote ya kibinadamu yanaweza kuelezwa kwa kutumia lengo letu la kuzaa: Kwa nini watu wanapinga sana ndoa baina ya watu wa jinsia moja? Kwa sababu watu katika jozi la namna hiyo hawawezi kuzaa Kwa nini watu hupendana? Kwa sababu upendo husababisha ngono, ambayo huchangia ustawi wa spishi ya binadamu Kwa nini akina mama hupenda watoto hata kama hawajazaliwa bado? Kwa sababu inachangia kutunza na kuongeza idadi ya binadamu Kwa nini watu wengi hupinga utoaji mimba? Kwa sababu inazuia uzazi Kwa nini madaktari wengi sana na matibabu mengi? Ili kutunza idadi ya watu Kwa nini uuaji ni hatia kubwa sana? Kwa sababu kuua kunapunguza idadi ya watu

Upanthei wa kiasilia

Kulingana na upanthei wa kiasilia, maana ya maisha ni kutunza viumbe na mazingira.

Mitazamo ya kidini

Dini za Asia ya Kusini

Falsafa za Kihindu

Aum ya dhahabu iliyoandikwa katika Devanagari. Aum ni takatifu katika dini za Uhindu, Ujaini na Ubuddha.

Uhindu ni jamii ya kidini inayojumuisha itikadi na desturi nyingi. Kwa sababu Uhindu ulikuwa njia ya kuonyesha maisha yenye maana tangu jadi, wakati ambapo hapakuwa na haja ya kutaja Uhindi kama dini tofauti, mafundisho ya Uhindu ni nyongeza na yanayowiana kiasili, kiujumla yasiyo ya kipekee, yenye kudokeza tu na yenye maudhui ya kuvumiliana.[90]

Wengi wanaamini kwamba ātman (roho, nafsi), nafsi ya kweli ya mtu, ni ya milele.[91]. Kwa sehemu, hili linatokana na imani ya Kihindu kwamba maendeleo ya kiroho hufanyika katika maisha mengi, na malengo yanafaa kuwiana na hali ya maendeleo ya mtu binafsi. Kuna malengo manne ya maisha ya binadamu, yanayojulikana kama purusharthas (yamepangwa kuanzia lile dogo zaidi hadi lile kuu): Kama (kazi, upendo na radhi ya kingono), Artha (mali), Dharma (haki, maadili), na Moksha (ukombozi kutoka mzunguko wa kuzaliwa upya).[92][93][94]

Katika shule zote za Uhindu, maana ya maisha imefungwa ndani ya dhana za karma (kitendo chenye matokeo), samsara (mzunguko wa kuzaliwa na kuzaliwa upya), na moksha (ukombozi). Kuwepo kunaaminika kuwa maendeleo ya atman kupitia vipindi vingi vya maisha, na maendeleo yake ya mwisho kuelekea ukombozi kutoka karma. Malengo hasa ya maisha kwa jumla husongeshwa chini ya (mazoea) pana ya yoga au dharma (kuishi kisahihi) ambayo yanakusudiwa kujenga kuzaliwa kupya kuzuri zaidi, ingawa hayo pia kwa ujumla ni matendo chanya katika maisha haya. Shule za jadi za Uhindu mara nyingi huabudu Madeva ambao ni dhihirisho ya Ishvara (Mungu wa kibinafsi au wa kuchaguliwa).

Uhindu wa Advaita na Dvaita

Shule za baadaye zilizitafsiri upya veda kuzingatia Brahman, "Yule Asiye na Wa Pili",[95] kama kielelezo muhimu kinachomfanana Mungu.

Katika Advaita Vedanta ya kimoni, atman hatimaye haitofautishwi na brahman, na lengo la maisha ni kujua au kutambua kwamba (nafsi) ya mtu ya atman inafanana na Brahman.[96]

Kwa Maupanishadi, yeyote anayefahamu kikamilifu atman, kama msingi wa ubinafsi, anajitambua na Brahman, na hivyo, anapata Mokasha (ukombozi, uhuru).[91][97][98]

Dvaita Vedanta yenye pande mbili na shule zingine za bhakti zina tafsiri yenye pande mbili. Brahaman anaonekana kama kiumbe kikuu chenye tabia na sifa wazi. Atman inategemea Brahman kwa kuwepo kwake; maana ya maisha ni kupata Moksha kupitia upendo wa Mungu na neema yake.[97]

Uvaishnavi

Tawi lingine la Uhindu ni Uvaishnavi, ambapo Vishnu ndiye Mungu mkuu. Si shule zote za Uvaishnavi hufunza maana ya maisha, lakini Gaudiya Vaishnavism, kwa mfano, hufunza Achintya Bheda Abheda inayomaanisha Kumuabudu Mungu tofauti na Mungu pekee wa kweli na wakati huo huo ikitambua umoja muhimu wa nafsi zote, huku viumbe vyote hai ni sehemu za milele za Mungu mkuu aitwaye Krsna.

Mtazamo wa kikatiba wa kiumbe hai ni kumtumikia Mungu na upendo na kujali. Huduma bila malipo isiyositishwa na isiyosukumwa na chochote kwa Krsna na wafuasi wake ndiyo maana ya maisha katika hali uhuru. Sisi tupo katika Dunia ya kinafsi tukimtumikia Krsna kwa furaha huku tukifahamu vyema kuwa sisi ni roho za kinafsi na tunayo maisha ya milele. Kwa sababu ya kumchukia Krsna na kwa sababu ya mapenzi yetu ya kutaka kuwa na anasa m,bali na Krsnatupo katika Dunia hii ambapo tunapitia mzunguko unaojirudiarudia wa kuzaliwa, magonjwa, uzee na kifo katika miili tuliyopata ya spishi 8.4 za kimaisha, tukihama kutoka mwili mmoja hadi mwingine kulingana na karma yetu na mapenzi yetu.

Lengo la maisha ya binadamu haswa ni kufikiria zaidi ya njia ya kinyama ya kula, kulala, kufanya mapenzi na kulinda na kufuata akili ya juu zaidi ili kuanzisha upya uhusiano na Krsna, Baba yetu wa milele, ambaye kutoka kwake vyote vilitoka, ambaye ndiye mwezeshaji na mwenye kuangamiza. Maandiko yaliyoonyehswa kwetu kama vile Bhagavad-Gita na Srimad Bhagavatam yanafunza kuwa Sambandha (Mimi ni nani? Mungu ni nani? Uhusiano kati ya Mungu na mimi ni upi?) na Abhideya (mchakato wa kuanzisha uhusiano ulipotea na Mungu kupitia michakato 9 ya Bhakti - Huduma ya Maombi) na Prayojana - matokeo - kupata upendo wa Mungu. Mchakato rahisi zaidi ni kuimba maha Bhakti "Hare Krsna Hare Krsna KRsna Krsna Hare Hare - Hare Rama Hare Rama Rama Rama Hare Hare" pamoja na wafuasi wa Mungu. Huku maana ya maisha yakiwa kuanzisha upya uhusiano ulioisha na Mungu anayewapenda watu wote, lengo la uumbaji ni kutumia rasilimali kurudi nyumbani kwa Mungu, Dunia ya milele ya kinafsi inayoitwa Goloka Vrindavana - milki ya Mungu.

Ujaini

Ujaini ni dini iliyoanza katika Uhindi ya kale, mfumo wake wa kimaadili unakuza nidhamu ya kibinafsi kushinda yote mengine. Kupitia kuyafuata mafundisho ya kujiepusha na anasa zote, ya ujaini, binadamu anapata kutaalamika (maarifa kamili). Ujaini unaugawanya ulimwengu katika viumbe vilivyohai na visivyohai. Wakati tu visivyohai vinavyoshikilia vyenye uhai ndipo mateso hutokea. Kwa hivyo, furaha ni matokeo ya utekaji-kibinafsi na uhuru kutoka kwa vitu vya nje. Maana ya maisha basi huweza kusemwa kuwa kutumia mwili unaoonekana kupata utambuzi wa kibinafsi na neema..[99]

Wajaini huamini kwamba kila binadamu anawajibika kwa matendo yake na viumbe wote hai wana roho ya milele, jīva. Wajaini wanaamini nafsi zote ni sawa kwa sababu zote zinamiliki uwezekano wa kufanywa ziwe huru na kufikia Moksha. Mtazamo wa Kijanini wa karma ni kwamba kila hatua, kila neno, kila wazo linazalisha, mbali na yanayoonekana, matokeo yasiyoonekana, na yanayopita fikira kwa nafsi.

Ujaini unajumuisha kushikilia vikali ahimsa (au ahinsā), mbinu ya aina ya Kusitisha Vurugu ambayo huzidi kwa mbali ulaji mboga. Wajaini wanakikataa chakula kilichopatikana kwa ukatili usiohitajika. Wengi wana mazoezi ya maisha sawa na ulaji mboga pekee kutokana na vurugu ya mashamba ya maziwa ya kisasa, na wengine huepukana na mboga za mizizi katika maakuli yao ili kulinda maisha ya mimea ambayo wao hula.[100]

Ubudha

Ubudha wa Mapema

Ubudha ni mafundisho yasiyo na pande mbili, ambapo kichwa, chombo, na hatua yote ni huonekana yakiwa si ya kweli.

Wabudha wanaamini kwamba maisha kwa undani yamejaa mateso au kuchanganyikiwa. Hilo si kumaanisha kwamba hakuna raha maishani, lakini kwamba raha hii haisababishi furaha ya milele. Mateso yanasababishwa na kuvishikilia vitu vinavyonekana na kuguzika au visivyoonekana na visivyokuguzika ambavyo mwishowe husababisha mtu kuzaliwa tena na tena katika mzunguko wa kuwepo. Sutra na tantra za Kibudha haziongei kuhusu "maana ya maisha" au "madhumuni ya maisha", bali huzungumzia kuhusu uwezo wa maisha ya binadamu wa kukomesha mateso kupitia kujiepusha na tamaa na kushikilia dhana fulani. Mateso yanaweza kushindwa kupitia shughuli za binadamu, tu kwa kuondoa sababu ya mateso. Kufikia na kutimiza kutopenda raha ni mchakato wa ngazi nyingi ambazo hatimaye matokeo yake ni hali ya Nirvana. Nirvana inamaanisha uhuru kutoka mateso na kuzaliwa upya.[101]

Gurudumu la dharmacakra lenye sehemu nane

Ubudha wa Kitheravada kwa jumla unadhaniwa kuwa karibu na mazoezi ya mapema ya Wabudha. Unakuza dhana ya Vibhajjavada (Pali), maana ya moja kwa moja "Kufunzwa kwa Uchambuzi", ambao Unasema kwamba lazima ufahamu utokane na uzoefu wa anAyenuia kuupata, uchunguzi makini, na kufikiria badala ya kutumia imani ya kipofu. Hata hivyo, mapokeo ya Kitheravadin pia yanasisitiza kuutilia maanani ushauri wa wenye busara, hasa ikizingatiwa kuwa ushauri huo na tathmini ya uzoefu wa kibinafsi kuwa vipimo viwili ambavyo vinafaa kutumiwa kuyapima mazoea. Lengo la Kitheravadin ni ukombozi (au uhuru) kutoka mateso, kulingana na Kweli Nne Adimu. Hili linapatikana katika kuipata Nirvana,au kufunguliwa ambao pia husitisha 0}mzunguko unaorudiwa wa kuzaliwa, uzee, maradhi na kifo.

Ubudha wa Kimahayana

Shule za Ubudha wa Kimahayana zinasita kusisitiza mtazamo wa jadi (ambao bado unatekelezwa katika Kitheravada) wa kuachiliwa kutoka Mateso (Dukkha) ta kibinafsi na kufikia Mwamko (Nirvana). Katika Mahayana, Budha huonekana kama kiumbe wa milele, asiyebadilika, asiyeeleweka, na ambaye yupo kila mahali. Misingi mikuu ya mafundisho ya Kimahayana imejikita katika uwezekano wa ukombozi kutoka mateso wa viumbe vyote, na kuwepo kwa Budha-asili apitaye fikira , ambaye ni kiini cha Budha wa milele aliopo, lakini aliyejificha na asiyetambulika, katika viumbe wote.

Shule za kifalsafa za Ubudha wa Kimahayana, kama vile Chan / Zen na shule za Utibeti wa vajrayana na Shingon, hufunza wazi kwamba boddhisattva lazima wajiepushe na ukombozi kamili, wajiruhusu wenyewe kuzaliwa tena ulimwenguni hadi viumbe wote wapate kutaalamika. Shule za kiibada kama vile Ubhuda wa Ardhi Takatifu hutafuta msaada wa mabudha wa mbinguni - watu binafsi ambao wametumia maisha yao wakikusanya karma chanya, na kuutumia mkusanyiko huo kuwasaidia wote.

Kalasinga

Ishara ya kidini ya Khanda, ambayo ni ishara muhimu ya dini ya Kalasinga.

Dini yenye Mungu mmoja ya Kalasinga ilianzishwa na Guru Nanak Dev. Neno "Kalasinga" linamaanisha mwanafunzi, kuashiria kwamba wafuasi wataishi maisha yao milele wakijifunza. Mfumo huu wa falsafa ya dini na kueleza imejulikana tangu jadi kama Gurmat (maana yake shauri la maguru) au Sikh Dharma. Wafuasi wa Kalasinga wametakaswa kuyafuata mafundisho ya maguru wa Sikh kumi, au viongozi wa kutaalamika, na pia maandiko matakatifu yaitwayo Gurū Granth Sāhib yanayojumuisha maandiko mbalimbali yaliyochaguliwa na wanafalsafa wengi kutoka mazingira mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kidini.

Maguru wa Kikalasinga hutuambia kwamba wokovu unaweza kupatikana kwa kuzifuata njia mbalimbali za kiroho, kwa hivyo si Wakalasinga pekee wanaopata wokovu: "Bwana anakaa ndani ya kila moyo, na kila moyo una njia yake yenyewe ya kumfikia."[102] Wakalasinga huamini kwamba watu wote ni muhimu mbele ya Mungu.[103] Wakalasinga hupima maadili yao ya kitabia na ya kiroho na kuyatafuta maarifa, na lengo la kukuza maisha ya amani na usawa, na pia yenye hatua chanya.[104]

Sifa muhimu na tofauti ya Kalasinga ni dhana ya Mungu isiyo ya kumtazama Mungu akiwa na umbo fulani, kiasi kwamba mtu anaweza kumtafsiri Mungu kama Ulimwengu wenyewe (upanthei). Kalasinga kwa hivyo inayaona maisha kama fursa ya kumuelewa huyu Mungu na pia kuugundua uungu ambao upo katika kila mmoja. Ingawa ufahamu kamili wa Mungu unazidi ubinadamu,[105] Guru Nanak alielezea Mungu kama asiye eleweka kikamilifu, na kusisitiza kwamba Mungu lazima aonekana kutoka kwa "jicho la ndani", au "moyo", wa binadamu: wanaoamini lazima watafakari ili kuelekea kutaalamika. Nanak alihimiza ufunuo kupitia kutafakari, kwani kutumika kwake kila wakati kunaruhusu kuwepo kwa mawasiliano kati ya Mungu na binadamu.[105]

Dini za Mashariki ya mbali

Ushinto

Shinto torii, mlango wa kitamaduni wa Kijapani

Ushinto ni dini iliyoanzia Ujapani. Neno Shinto linamaananisha "njia ya kami", lakini kwa ufasaha zaidi, linaweza kumaanisha "sehemu yenye njia nyingi ambapo kami anachagua njia yake". Njia yenye sehemu nyingi ya 'kimungu' inaashiria kwamba ulimwengu wote ni roho ya kimungu. Msingi wa nia huru kuichagua njia ya mmoja, inamaanisha kwamba maisha ni mchakato wa ubunifu.

Ushinto Unayataka maisha ya kuishi, siyo ya kufa. Ushinto unakitazama kifo kama uchafuzi na inatazama maisha kama eneo ambapo roho ya kimungu inanuia kujitakasa yenyewe kwa kujiendeleza inavyostahili. Ushinto unayataka maisha ya kibinafsi ya kibinadamu kuendelezwa milele duniani kama ushindi wa roho ya kimungu katika kuhifadhi tabia yake ya usawa kwa hali ya juu kabisa. Kuwepo kwa uovu duniani, kama inavyodokezwa na Ushinto, hakupingi hali ya kimungu kwa kuweka juu ya uungu jukumu la kuweza kuyapunguza mateso ya binadamu huku ikikataa kufanya hivyo. Mateso ya maisha ni mateso ya roho ya kimungu katika kuyatafuta mafanikio katika ulimwengu unaolenga usawa.[106]

Utao

Taijitu ni ishara ya umoja wa vinyume vya yin na yang.

Kosmojenia ya Watao inasisitiza haja ya viumbe wote wenye fahamu na watu wote kurudi kwa mwanzo au kuungana na Umoja wa Ulimwengu kupitia njia ya kujikuza na kujitambua. Wahumini wote wanapaswa kuelewa na kuwiana na mwisho wa kikweli.

Wanaamini yote awali yalikuwa kutoka Taiji na Tao, na maana maishani kwa wahumini ni wao kugundua hali ya muda mfupi ya kuwepo. "Kujiangalia tu kindani ndio kunaoweza basi kutusaidia kupata sababu zetu za undani kabisa za kuishi...jibu rahisi limo humu ndani yetu."[107]

Ukonfusio

Ukonfusio unatambua hali ya binadamu kulingana na mahitaji ya nidhamu na elimu. Kwa sababu binadamu anaendeshewa na ushawishi mzuri na mbaya, Wakonfiuso huona lengo katika kupata tabia nzuri kupitia uhusiano wa nguvu na kufikiria na pia kukanusha nishati hasi. Msisitizo huu wa maisha ya kawaida unaonekana katika msemo wa mwanachuoni wa Kikonfiuso Tu Wei-Ming, "tunaweza kutambua maana kuu ya maisha katika kuwepo kwa kawaida kwa binadamu."[108]

Dini mpya

Kuna harakati nyingi mpya za kidini katika Asia ya Mashariki, baadhi yao zikiwa na mamilioni ya wafuasi: Chondogyo, Tenrikyo, Cao Đài, na Seicho-No-ie. Dini mpya kawaida zina maelezo ya kipekee kuhusu maana ya maisha. Kwa mfano, katika Tenrikyo, mtu anatarajiwa kuishi Maisha ya Furaha kwa kushiriki katika mazoea yanayokuza furaha yake binafsi na pia ya watu wengine.

Dini za Magharibi na Mashariki ya Kati

Uzoroastro

Uzoroastro ni dini na falsafa inayopata jina lake kutoka kwa nabii wake Zoroaster, ambayo labda iliathiri imani za Uyahudi na dini zilitokana na Uyahudi. Wazoroastro wanaamini ulimwengu na Mungu apitaye fikra, Ahura Mazda, ambaye ibada yote inaelekezwa kwake. Kiumbe cha Azhura Mazda ni asha, ukweli na mpango ambao unazozana na kinyume chake, druj, uwongo na machafuko.

Kwa sababu binadamu wana hiari, ni lazima wawe na uwajibikaji kwa maadili wanayoyachagua. Kwa kutumia hiari, watu lazima wawe na jukumu tendaji katika mgogoro wa dunia nzima, wawe na mawazo mema, maneno mema na matendo mema ili kuhakikisha furaha na kuepuka machafuko.

Uyahudi

Kipengele muhimu zaidi cha Uyahudi ni ibada ya Mungu mmoja anayejua yote, mwenye nguvu kuliko wote, ambaye ni mkarimu kila wakati, anayepita fikra zote, na ambaye aliumba ulimwengu na anautawala. Kulingana na Uyahudi wa awali, Mungu alifanya agano na Waisraeli katika mlima Sinai, alipowapa sheria na amri zake zinazopatikana katika Torati. Katika Uyahudi wa Kirabi, Torati inajumuisha maandishi ya Torati na sheria ya mapokeo ya mdomo (iliyoandikwa baadaye kama maandiko matakatifu).

Katika mtazamo wa ulimwengu wa Kiyahudi, maana ya maisha ni kumtumikia Mungu pekee wa kweli na kujiandaa kwa ulimwengu ujao.[109][110] Fikira za "Olam Haba"[111] Inahusu kujiinua kiroho, ni mtu kutumia "Olam Hazeh" (dunia hii) kwa kuunganika na Mungu na kujiandaa kwa "Olam Haba" (ulimwengu ujao). [112]

Ukristo

Picha ya Hans Memling inayoitwa Hukumu ya Mwisho, inaonyesha Malaika mkuu Mikaeli akipima nafsi na kuwafukuza waliohukumiwa kuelekea jehanamu.

Ingawa Ukristo una mizizi yake katika Uyahudi, na unafanana sana na ontolojia ya Uyahudi, imani kuu ya Ukristo inatokana na mafundisho ya Yesu Kristo yaliyotolewa katika Agano Jipya. Kusudi la maisha kwa Mkristo ni kutafuta wokovu wa Kimungu kupitia neema ya Mungu iliyoletwa na Yesu (Yoh 11:26).

Agano Jipya linaongea kuhusu Mungu kutaka uhusiano na binadamu wote katika maisha haya na yale yajao, jambo ambalo linaweza kufanyika tu kama dhambi za mtu zimesamehewa (Yoh 3:16-21), (2 Pet 3:9).

Katika mtazamo wa Kikristo, watu waliumbwa katika hali njema kwa mfano wa Mungu, lakini kuanguka kwao (dhambi ya asili) kulisababisha wanaozaliwa kuirithi dhambi hiyo.

Sadaka ya Yesu Kristo ya upendo, kifo na ufufuko hutoa njia ya kuishinda hali hiyo chafu (Rum 6:23).

Njia ya kufanya hivyo inatofautiana kati ya madhehebu mbalimbali ya Wakristo, lakini yote yanategemea imani kwa Yesu, kazi yake msalabani na kufufuka kwake kama msingi wa uhusiano mpya na Mungu. Chini ya mtazamo wa Ukristo, watu wanafanywa waadilifu kupitia imani katika kafara ya Yesu kufa msalabani.

Injili inafundisha kwamba, kupitia imani hiyo, kizuizi ambacho dhambi imeunda kati ya mtu na Mungu kinaondolewa, ili kumruhusu Mungu kuwageuza watu na kuweka ndani yao moyo mpya unaotii mapenzi yake, na uwezo wa kutii hivyo.

Hii ndiyo maana inayoashiriwa na maneno 'kuzaliwa upya' au 'kuokolewa'.

Jambo hili linatofautisha sana Ukristo na dini nyingine ambazo zinadai kwamba waumini ni waadilifu kwake Mungu kwa kushikamana na mwongozo au sheria waliyopewa na Mungu.

Katika "Katekisimu Fupi ya Westminster", swali la kwanza ni: "Ni nini lengo kuu la binadamu?". Jibu ni: "Lengo kuu la binadamu ni kumtukuza Mungu na kufurahi naye milele. Mungu anataka mtu atii sheria ya maadili aliyomwonyesha akisema tumpende Bwana Mungu wetu kwa moyo wetu wote, kwa roho yetu yote, kwa nguvu zetu zote, na kwa akili zetu zote; na majirani wetu kama sisi wenyewe".[113]

Katekisimu ya Baltimore inajibu swali, "Kwa nini Mungu amekuumba?" ikisema "Mungu ameniumba ili nimjue, nimpende na kumtumikia katika dunia hii, na kuwa na heri pamoja naye milele mbinguni."[114]

Mtume Paulo alijibu swali hilo katika hotuba yake kwenye Areopago mjini Athene: "Kutokana na mtu mmoja (Mungu) alifanya kila taifa la wanadamu, ili waishi duniani kote; akapima nyakati hasa zilizowekwa kwao na mahali ambapo wanapaswa kuishi. Mungu alifanya hivyo ili binadamu amtafute kama kwa kupapasa ili kumpata, ingawa hayupo mbali na kila mmojawetu. (Mdo 17:26-27)[115]

Uislamu

Katika Uislamu, lengo kuu la maisha ya binadamu ni kumtumikia Allah (kwa Kiarabu sawa na "Mungu") na kukaa na miongozo ya Kimungu iliyofafanuliwa katika Qur'an na Mapokeo ya Mtume. Maisha ya duniani ni mtihani tu ambao huamua maisha ya mtu baada ya kifo, katika Jannat (Mbinguni) au katika Jahannum (Kuzimu).

Kwa ajili ya radhi ya Mwenyezi Mungu, kupitia Qur'ani, lazima Waislamu wote waamini katika Mungu, ufunuo wake, malaika wake, wajumbe wake, na katika "Siku ya Kiyama".[116] Qur'an inaelezea madhumuni ya uumbaji kama ifuatavyo: "Heri yeye ambaye mkononi mwake ana ufalme, yeye ana nguvu juu ya kila kitu, ambaye aliumba mauti na uhai ili apate kuchunguza nani kati yenu ndiye bora katika matendo, na yeye ni mwenyezi, Mwenye kusamehe "(Qur'an67 :1-2) na" 'Mimi tu niliumba malaika na binadamu kuniabudu Mimi "(Qur'an 51:56). Ibada inashuhudia kuwepo kwa umoja wa Mungu katika uongozi wake, majina yake, na sifa yake. maisha ya Duniani ni mtihani; jinsi mtu anavyotenda huamua kama nafsi ya mtu inakwenda Jannat (Mbinguni) au Jahannam (Motoni).

Nguzo Tano za Kiislamu ni wajibu wa kila Muislamu; yaani: Shahadah (ungamo la imani); Salah (Maombi); Zakah (ukarimu); Sawm (kufunga wakati wa Ramadhan) na Hajj (Hija kwenda Makka).[117] Zinatokana na maandiko ya Hadith, hasa ya Sahih Al-Bukhari na Sahih Muslim.

Imani ni tofauti kati ya Kalam. Dhana ya Kisunni ya mwisho wa safari iliyoamuliwa awali ni amri ya Kimungu;[118] aidha, dhana ya Kishi'a ya nafsi kuwa na mahali pa kwenda kabla ya kifo ni haki ya Kimungu; katika mtazamo wa Kisufi unaoeleweka na wachache Ulimwengu upo tu kwa radhi ya Mungu; Uumbaji ni mchezo mkubwa, ambapo Mwenyezi Mungu ndiye tuzo kuu.[119][119]

Imani ya Bahá'í

Imani ya Bahai inasisitiza umoja wa ubinadamu.[120] Kwa Wabahá'í, madhumuni ya maisha ni kukua kiroho na kutoa huduma kwa ubinadamu. Binadamu wanatazamwa kama viumbe wa kiroho kwa undani. Maisha ya watu katika dunia hii tunayoishi hutoa fursa zilizopanuliwa za kukua, kukuza sifa na fadhila za Kimungu, na manabii walitumwa na Mungu kuwezesha hili.[121][122]

Katika sanaa

Siri ya maisha na maana yake ni jambo linalorudiwa mara nyingi katika utamaduni maarufu, unaoonyeshwa katika burudani ya vyombo vya habari na aina mbalimbali za sanaa.

Yote ni bure, picha ya Charles Allan Gilbert, ni mfano wa vanitas. Inaonyesha mwanamke akitazama uso wake katika kioo, lakini vyote vimepangwa ili kuifanya picha ya kifuvu kuonekana.

Katika mfululizo maarufu wa vitabu vya kuchekesha vya Douglas Adams kwa jina "The Hitchhiker's Guide to the Galaxy", Jibu la Swali Kuu la Maisha, Ulimwengu, na Yote lina ufumbuzi wa kinambari wa 42, ambayo ilipatikana baada ya muda wa zaidi ya miaka milioni saba na nusu kupitia tarakilishi yenye nguvu kubwa kwa jina "Deep Thought". Baada ya kunganyika kwingi kutoka wazao wa waumbaji wake, "Deep Thought" anaelezea kuwa tatizo ni kuwa hawajui Swali Kuu, na ingewabidi kujenga kompyuta yenye nguvu zaidi ili kulibainisha. Kompyuta inaonyeshwa kuwa Dunia, ambayo, baada ya kuhesabu kwa miaka milioni, inaharibiwa ili kuunda Barabara ya Kiulimwengu dakika tano kabla ya kukamilisha kufanya hesabu.[5][7][11][123] Katika Maisha, Ulimwengu na Kila kitu, inathibitishwa kwa kweli kuwa 42 ndilo Jibu Kuu, na kwamba haiwezekani kwa Jibu Kuu na Swali Kuu kujulikana katika ulimwengu mmoja, kwani zitafutana na kuuchukua ulimwengu, na kubadilishwa na kitu cha maajabu zaidi,(mhusika mmoja, Prak, anapendekeza kwamba hili huenda likawa limetokea tayari).[124] Hatimaye, katika matumaini kwamba fahamu yake ina swali, Arthur Dent anajaribu kuliwaza swali, na anapata "unapata nini ukizidisha sita mara tisa?", Pengine ni dhana isiyosahihi, kwani kuwasili kwa "Golgafrinchans" katika Dunia ya kabla ya historia ingeharibu mchakato wa kuhesabu.[125] Hata hivyo, Dent, Fenchurch, na Marvin anayekaribia kufa waliona ujumbe wa mwisho wa Mungu kwa uumbaji wake: "Sisi tunaomba msamaha kwa shida tuliyowaletea".[126]

Hamlet na fuvu la kichwa la Yorick

Katika maana ya maisha ya Monty Python,kuna kugusia kwingi kwa maana ya maisha. Katika "Sehemu ya VI B: Maana ya Maisha" mwanamke anayefanya kazi ya kusafisha anaelezea "Maisha ni mchezo, wakati mwingine unashinda au kushindwa" na baadaye mtu wa kupelekea watu vyakula hotelini anaelezea falsafa yake ya kibinafsi "Dunia ni pahali pazuri. Lazima uende ndani yake, na upende kila mtu, usiwachukie watu. Lazima hujaribu na kumfanya kila mtu awe na furaha, na upeleke amani na ridhaa kokote uendapo.[127] Katika mwisho wa filamu, tunaweza kumuona Michael Palin akipewa bahasha, anaifungua, na kupea watazamaji 'maana ya maisha': "Basi, si kitu maalumu sana. Uh, jaribu kuwa mzuri kwa watu, epuka kula mafuta, soma kitabu kizuri kila wakati, pata kutembea, na jaribu kuishi pamoja kwa amani na utulivu na watu wa Imani zote na mataifa yote.[127][128][129]

Katika kipindi kimoja cha "The Simpsons" kilichoitwa "Homer the Heretic", mfano wa Mungu unakubali kumwambia Homer maana ya maisha, lakini majina ya wahusika wa kipindi yanaanza kuonekana anapoanza kusema ni nini. Mapema katika kipindi hicho, Homer anaanzisha dini yake mwenyewe, ambapo anajaribu kumwabudu Mungu kwa njia yake mwenyewe, baadaye akimwwambia Moe kwamba dini hiyo haina kuzimu na haina kupiga magoti. Hata hivyo, Homer anaiacha kwa haraka dini yake ya anasa na ubinafsi baada baada ya nyumba yake kunusurika kuchomeka, akitafsiri moto kama ishara ya kulipiza kisasi kwa kimungu, na kuita "O Mwenye Nguvu za Kuumiza, nionyeshe nani wa kuumiza, naye ataumizwa." Ned anamfariji Homer kuwa moto haukuwa kisasi cha Mungu na Lovejoy anaelezea kwamba Mungu alikuwa "akifanya kazi katika mioyo ya marafiki na majirani wako walipokuja kukusaidia."[130]

Mwishoni mwa "The Matrix Revolutions", Smith anahitimsha kwamba "madhumuni ya maisha ni kuisha" na anakusudia kuharakisha lengo hilo.[131] The Matrix series. Mfululizo wa filamu wa "The Matrix" pia unatoa wazo la "wanaoishi katika ukweli uliobuniwa" na swali linalohusika na wazo hilo ikiwa kuwepo huko kunafaa kutazamwa kama kusiokuwa na maana, katika njia inayoweza kulinganishwa na Hadithi fupi yenye mafunzo ya pango ya Plato na jinsi baadhi ya mifumo ya imani hutazama ukweli, kama Ubuddha au Uaginostiki.[132]

Tazama pia

Tanbihi

  1. Jonathan Westphal (1998). Philosophical Propositions: An Introduction to Philosophy. Routledge. ISBN 0415170532.
  2. Robert Nozick (1981). Philosophical Explanations. Harvard University Press. ISBN 0674664795.
  3. Albert Jewell (2003). Ageing, Spirituality and Well-Being. Jessica Kingsley Publishers. ISBN 184310167X. {{cite book}}: line feed character in |publisher= at position 17 (help)
  4. 4.0 4.1 "Question of the Month: What Is The Meaning Of Life?". Philosophy Now. Issue 59. Iliwekwa mnamo 2007-07-26.
  5. 5.0 5.1 Glenn Yeffeth (2005). The Anthology at the End of the Universe: Leading Science Fiction Authors on Douglas Adams' The Hitchhiker's Guide to the Galaxy. BenBella Books, Inc. ISBN 1932100563.
  6. David Seaman (2005). The Real Meaning of Life. New World Library. ISBN 1577315146.
  7. 7.0 7.1 7.2 7.3 Julian Baggini (2004). What's It All About? Philosophy and the Meaning of Life. USA: Granta Books. ISBN 1862076618. {{cite book}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  8. Ronald F. Thiemann; William Carl Placher (1998). Why Are We Here?: Everyday Questions and the Christian Life. Continuum International Publishing Group. ISBN 1563382369.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  9. Dennis Marcellino (1996). Why Are We Here?: The Scientific Answer to this Age-old Question (that you don't need to be a scientist to understand). Lighthouse Pub. ISBN 0945272103.
  10. F. Homer Curtiss (2003). Why Are We Here. Kessinger Publishing. ISBN 0766138992.
  11. 11.0 11.1 William B. Badke (2005). The Hitchhiker's Guide to the Meaning of Everything. Kregel Publications. ISBN 0825420695.
  12. 12.0 12.1 Hsuan Hua (2003). Words of Wisdom: Beginning Buddhism. Dharma Realm Buddhist Association. ISBN 0881393029.
  13. 13.0 13.1 Paul Davies (Machi 2000). The Fifth Miracle: The Search for the Origin and Meaning of Life. Simon & Schuster. ISBN 0-684-86309-X. Iliwekwa mnamo 2007-07-26.
  14. 14.0 14.1 14.2 14.3 Jose Fadul (2008). Lessons in Chess, Lessons in Life: Application of the Psychology of the Game in Real Life. Lulu Press. ISBN 978-0-557-02158-1.
  15. 15.0 15.1 Charles Christiansen; Carolyn Manville Baum; Julie Bass-Haugen (2005). Occupational Therapy: Performance, Participation, and Well-Being. SLACK Incorporated. ISBN 1556425309.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  16. 16.0 16.1 Evan Harris Walker (2000). The Physics of Consciousness: The Quantum Mind and the Meaning of Life. Perseus Books. ISBN 0738204366.
  17. Rick Warren (2002). The Purpose Driven Life: What on Earth Am I Here For?. Zondervan. ISBN 0310255252.
  18. 18.0 18.1 Jiddu Krishnamurti (2001). What Are You Doing With Your Life?. Krishnamurti Foundation of America. ISBN 188800424X.
  19. Puolimatka, Tapio (2002). "Education and the Meaning of Life" (PDF). Philosophy of Education. University of Helsinki. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2007-09-26. Iliwekwa mnamo 2007-07-26. {{cite web}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  20. Stan Van Hooft (2004). Life, Death, and Subjectivity: Moral Sources in Bioethics. Rodopi. ISBN 9042019123.
  21. Russ Shafer-Landau; Terence Cuneo (2007). Foundations of Ethics: An Anthology. Blackwell Publishing. ISBN 1405129514.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  22. E. Diener, J.J. Sapyta, E. Suh (1998). "Subjective Well-Being Is Essential to Well-Being." Psychological Inquiry, Lawrence Earlbaum
  23. Csíkszentmihályi, Mihály (1990). Flow: The Balls of Optimal Experience. New York: Harper and Row. ISBN 0-06-092043-2.
  24. Peterson, Christopher; Seligman, Martin (2004). Character strengths and virtues: A handbook and classification. Oxford: Oxford University Press. ISBN 0-19-516701-5.
  25. Seligman, M.E.P. (2002). Authentic Happiness: Using the New Positive Psychology to Realize Your Potential for Lasting Fulfillment. New York: Free Press. ISBN 0-7432-2297-0 (Paperback edition, 2004, Free Press, ISBN 0-7432-2298-9)
  26. Charles Darwin (1859). On the Origin of Species.
  27. Richard Dawkins (1976). The Selfish Gene. Oxford University Press. ISBN 019857519X.
  28. Richard Dawkins (1995). River out of Eden. New York: Basic Books. ISBN 0-465-06990-8.
  29. Astrobiology Magazine: Defining Life
  30. "Defining Life, Explaining Emergence". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-03-14. Iliwekwa mnamo 2010-01-15.
  31. Schrödinger, Erwin (1944). What is Life?. Cambridge University Press. ISBN 0-521-42708-8.
  32. Margulis, Lynn (1995). What is Life?. University of California Press. ISBN 0-520-22021-8. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  33. Lovelock, James (2000). Gaia – a New Look at Life on Earth. Oxford University Press. ISBN 0-19-286218-9.
  34. Avery, John (2003). Information Theory and Evolution. World Scientific. ISBN 9812383999.
  35. Davison, Paul G. "How to Define Life". The University of North Alabama. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-11-01. Iliwekwa mnamo 2008-10-17.
  36. Witzany, G. (2007). The Logos of the Bios 2. Bio-Communication. Helsinki, Umweb.
  37. Helge Kragh (1996). Cosmology and Controversy. Princeton University Press. ISBN 069100546X.
  38. 38.0 38.1 Nikos Prantzos; Stephen Lyle (2000). Our Cosmic Future: Humanity's Fate in the Universe. Cambridge University Press. ISBN 052177098X.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  39. Rem B. Edwards (2001). What Caused the Big Bang?. Rodopi. ISBN 9042014075.
  40. Harvey Whitehouse (2001). The Debated Mind: Evolutionary Psychology Versus Ethnography. Berg Publishers. ISBN 1859734278.
  41. 41.0 41.1 Jeffrey Alan Gray (2004). Consciousness: Creeping Up on the Hard Problem. Oxford University Press. ISBN 0198520905.
  42. 42.0 42.1 John D. Barrow; Paul C. W. Davies; Charles L. Harper (2004). Science and Ultimate Reality: Quantum Theory, Cosmology and Complexity. Cambridge University Press. ISBN 052183113X.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  43. Jean Millay; Ruth-Inge Heinze (1999). Multidimensional Mind: Remote Viewing in Hyperspace. North Atlantic Books. ISBN 1556433069.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  44. Paul M. Churchland (1989). A Neurocomputational Perspective: The Nature of Mind and the Structure of Science. MIT Press. ISBN 0262531062.
  45. Daniel Clement Dennett (1991). Consciousness Explained. Little, Brown and Co. ISBN 0316180661.
  46. J. McFadden (2002) "Synchronous Firing and Its Influence on the Brain's Electromagnetic Field: Evidence for an Electromagnetic Field Theory of Consciousness Ilihifadhiwa 18 Desemba 2005 kwenye Wayback Machine.". Journal of Consciousness Studies 9 (4) pp. 23-50.
  47. R. Buccheri; V. Di Gesù; Metod Saniga (2000). Studies on the Structure of Time: From Physics to Psycho(patho)logy. Springer. ISBN 030646439X.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  48. 48.0 48.1 David Bohm; Basil J. Hiley (1993). The Undivided Universe: An Ontological Interpretation of Quantum Theory. Routledge. ISBN 0415065887.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  49. 49.0 49.1 Alexandra Bruce (2005). Beyond the Bleep: The Definitive Unauthorized Guide to What the Bleep Do We Know!?. The Disinformation Company. ISBN 1932857222.
  50. Benjamin Libet; Anthony Freeman; Keith Sutherland (1999). The Volitional Brain: Towards a Neuroscience of Free Will. Imprint Academic. ISBN 0907845118.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  51. Mae-Wan Ho (1998). The Rainbow and the Worm: The Physics of Organisms. World Scientific. ku. 218–231. ISBN 9810234279.
  52. Radin, Dean (1997). The Conscious Universe: The Scientific Truth of Psychic Phenomena. HarperSanFrancisco. ISBN 0062515020.
  53. Alcock, James E. (2003). "Give the Null Hypothesis a Chance" (PDF). Journal of Consciousness Studies. 10 (6–7): 29–50. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2007-08-10. Iliwekwa mnamo 2007-07-30. {{cite journal}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  54. Hyman, Ray (1995). "Evaluation of the program on anomalous mental phenomena". The Journal of Parapsychology. 59 (1). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-09. Iliwekwa mnamo 2007-07-30. {{cite journal}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  55. Akers, C. (1986). "Methodological Criticisms of Parapsychology, Advances in Parapsychological Research 4". PesquisaPSI. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-27. Iliwekwa mnamo 2007-07-30. {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  56. Child, I.L. (1987). "Criticism in Experimental Parapsychology, Advances in Parapsychological Research 5". PesquisaPSI. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-27. Iliwekwa mnamo 2007-07-30. {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  57. Wiseman, Richard (1996). "Exploring possible sender-to-experimenter acoustic leakage in the PRL autoganzfeld experiments - Psychophysical Research Laboratories". The Journal of Parapsychology. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-09. Iliwekwa mnamo 2007-07-30. {{cite journal}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  58. Lobach, E. (2004). "The Invisible Gaze: Three Attempts to Replicate Sheldrake's Staring Effects" (PDF). Proceedings of the 47th PA Convention. ku. 77–90. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2007-08-10. Iliwekwa mnamo 2007-07-30. {{cite web}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  59. Kidd, I., "Cynicism," in The Concise Encyclopedia of Western Philosophy. (ed. J. O. Urmson and Jonathan Rée), Routledge. (2005)
  60. Long, A. A., "The Socratic Tradition: Diogenes, Crates, and Hellenistic Ethics," in The Cynics: The Cynic Movement in Antiquity and Its Legacy. (ed. Branham and Goulet-Cazé), University of California Press, (1996).
  61. "Cyrenaics." Internet Encyclopedia of Philosophy. The University of Tennessee At Martin. 4 Nov. 2007 <http://www.iep.utm.edu/>.
  62. "The Cyrenaics and the Origin of Hedonism." Hedonism.org. BLTC. 4 Nov. 2007 <http://www.hedonism.org Ilihifadhiwa 22 Mei 2020 kwenye Wayback Machine.>.
  63. Epicurus, "Letter to Menoeceus", contained in Diogenes Laertius, Lives of Eminent Philosophers, Book X
  64. 64.0 64.1 64.2 64.3 Bertrand Russell (1946). A History of Western Philosophy, New York: Simon and Schuster; London: George Allen and Unwin
  65. A: "'Liberalism' is defined as a social ethic that advocates liberty, and equality in general." – C. A. J. (Tony) Coady Distributive Justice, A Companion to Contemporary Political Philosophy, editors Goodin, Robert E. and Pettit, Philip. Blackwell Publishing, 1995, p.440. B: "Liberty is not a means to a higher political end. It is itself the highest political end." – Lord Acton
  66. Rosen, Frederick (2003). Classical Utilitarianism from Hume to Mill. Routledge, pg. 28. ISBN 0415220947 "It was Hume and Bentham who then reasserted most strongly the Epicurean doctrine concerning utility as the basis of justice."
  67. Mill, John Stuart. 'On Liberty', ed. Himmelfarb. Penguin Classics, 1974, Ed.'s introduction, p.11.
  68. 68.0 68.1 Jérôme Bindé (2004). The Future Of Values: 21st-Century Talks. Berghahn Books. ISBN 1571814426.
  69. 69.0 69.1 Bernard Reginster (2006). The Affirmation of Life: Nietzsche on Overcoming Nihilism. Harvard University Press. ISBN 0674021991.
  70. Heidegger, "The Word of Nietzsche," 61.
  71. William James (1909). The Meaning of Truth. Prometheus Books. ISBN 1-57392-138-6.
  72. Walter Robert Corti (1976). The Philosophy of William James. Meiner Verlag. ISBN 3787303529.
  73. Amy Laura Hall (2002). Kierkegaard and the Treachery of Love. Cambridge University Press. ISBN 0521893119.
  74. Dale Jacquette (1996). Schopenhauer, Philosophy, and the Arts. Cambridge University Press. ISBN 0521473888.
  75. Durno Murray (1999). Nietzsche's Affirmative Morality. Walter de Gruyter. ISBN 3110166011.
  76. Solomon, Robert C. (2001). From Rationalism to Existentialism: The Existentialists and Their Nineteenth Century Backgrounds. Rowman and Littlefield. uk. 245. ISBN 074251241X.
  77. Camus (1946) L'Etranger
  78. Camus (1955) The Myth of Sisyphus
  79. Albert Camus at the Internet Encyclopedia of Philosophy Accessed Mei 25th, 2009
  80. 80.0 80.1 80.2 80.3 "Humanist Manifesto I] [http://www.americanhumanist.org/about/manifesto1.html url=http://www.americanhumanist.org/about/manifesto1.html". American Humanist Association. 1933. {{cite web}}: |access-date= requires |url= (help); External link in |title= (help); Missing or empty |url= (help); Missing pipe in: |title= (help)
  81. 81.0 81.1 81.2 "[[Humanist Manifesto II]]] [http://www.americanhumanist.org/about/manifesto2.html work=American Humanist Association". 1973. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-08-09. Iliwekwa mnamo 2007-08-01. {{cite web}}: External link in |title= (help); Missing pipe in: |title= (help); URL–wikilink conflict (help)
  82. 82.0 82.1 82.2 "[[Humanist Manifesto III]]] [http://www.americanhumanist.org/3/HumandItsAspirations.php work=American Humanist Association". 2003. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-08-09. Iliwekwa mnamo 2007-08-01. {{cite web}}: External link in |title= (help); Missing pipe in: |title= (help); URL–wikilink conflict (help)
  83. "[[A Secular Humanist Declaration]]] [http://www.secularhumanism.org/index.php?section=main&page=declaration work=Council for Democratic and Secular Humanism (now the Council for Secular Humanism)". 1980. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-08-17. Iliwekwa mnamo 2007-08-01. {{cite web}}: External link in |title= (help); Missing pipe in: |title= (help); URL–wikilink conflict (help)
  84. Nick Bostrom (2005). "Transhumanist Values". Oxford University. Iliwekwa mnamo 2007-07-28.
  85. Irvin Yalom, Existential Psychotherapy, 1980
  86. Richard Taylor (1970). Good and Evil. Macmillan Publishing Company. ku. "The Meaning of Life" (Chapter 5). ISBN 0026166909. {{cite book}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  87. Wohlgennant, Rudolph. (1981). "Has the Question about the Meaning of Life any Meaning?" (Chapter 4). In E. Morscher, ed., Philosophie als Wissenschaft.
  88. McNaughton, David (1988). Moral Vision: An Introduction to Ethics. Oxford: Blackwell Publishing. ku. "Moral Freedom and the Meaning of Life" (Section 1.5). ISBN 0631159452. {{cite book}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  89. Bertrand Russell (1961). Science and Ethics Ilihifadhiwa 14 Novemba 2007 kwenye Wayback Machine.
  90. Kigezo:Harvard reference
  91. 91.0 91.1 Kigezo:Harvard reference
  92. For dharma, artha, and kama as "brahmanic householder values" see: Flood (1996), p. 17.
  93. For the Dharma Śāstras as discussing the "four main goals of life" (dharma, artha, kāma, and moksha) see: Hopkins, p. 78.
  94. For definition of the term पुरुष-अर्थ (puruṣa-artha) as "any of the four principal objects of human life, i.e. धर्म, अर्थ, काम, and मोक्ष" see: Apte, p. 626, middle column, compound #1.
  95. Kigezo:Harvard reference
  96. Kigezo:Harvard reference
  97. 97.0 97.1 Kigezo:Harvard reference
  98. See also the Vedic statement "ayam ātmā brahma" (This Atman is Brahman)
  99. Shah, Natubhai. Jainism: The World of Conquerors. Sussex Academic Press, 1998.
  100. "Viren, Jain" (PDF). RE Today. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2007-06-14. Iliwekwa mnamo 2007-06-14. {{cite web}}: External link in |publisher= (help)
  101. "The Four Noble Truths". Thebigview.com. Iliwekwa mnamo 2009-11-06.
  102. Daljeet Singh (1971). Guru Tegh Bahadur. Language Dept., Punjab.
  103. Jon Mayled (2002). Modern World Religions: Sikhism. Harcourt Heinemann. ISBN 0435336266.
  104. The Sikh Coalition
  105. 105.0 105.1 Parrinder, Geoffrey (1971). World Religions: From Ancient History to the Present. United States: Hamlyn Publishing Group Limited. ISBN 0-87196-129-6.
  106. J. W. T. Mason (2002). The Meaning of Shinto. Trafford Publishing. ISBN 1412245516.
  107. Ming-Dao Deng (1990). Scholar Warrior: An Introduction to the Tao in Everyday Life. HarperCollins.
  108. Tu, Wei-Ming. Confucian Thought: Selfhood as Creative Transformation. Albany: State University of New York Press, 1985.
  109. Dan Cohn-Sherbok (2003). Judaism: History, Belief, and Practice. Routledge. ISBN 0415236614.
  110. Abraham Joshua Heschel (2005). Heavenly Torah: As Refracted Through the Generations. Continuum International Publishing Group. ISBN 0826408028.
  111. Wilfred Shuchat (2006). The Garden of Eden & the Struggle to Be Human: According to the Midrash Rabbah. Devora Publishing. ISBN 1932687319.
  112. Randolph L. Braham (1983). Contemporary Views on the Holocaust. Springer. ISBN 089838141X.
  113. "The Westminster Shorter Catechism". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-03-11. Iliwekwa mnamo 2008-03-21.
  114. "The Baltimore Catechism". Iliwekwa mnamo 2008-06-12.
  115. Bible, Acts 17:26-27, NKJV
  116. Qur'an 2:4, Qur'an 2:285, Qur'an 4:136
  117. "Pillars of Islam". Encyclopaedia Britannica Online.
  118. Kigezo:Muslim
  119. 119.0 119.1 Abdullah Yusuf Ali (2000). The Holy Qur'an. Wordsworth Editions. ISBN 1853267821.
  120. "Bahaism." The American Heritage Dictionary of the English Language, juz. la Fourth Edition, Houghton Mifflin Company, 2007
  121. Smith, P. (1999). A Concise Encyclopedia of the Bahá'í Faith. Oxford, UK: Oneworld Publications. ku. 325–328. ISBN 1851681841.
  122. For a more detailed Bahá'í perspective, see "The Purpose of Life" Bahá'í Topics An Information Resource of the Bahá'í International Community
  123. Douglas Adams (1979). The Hitchhiker's Guide to the Galaxy. London: Pan Books. ISBN 0-330-25864-8. {{cite book}}: Unknown parameter |published= ignored (help)
  124. Douglas Adams (1982). Life, the Universe and Everything. London: Pan. ISBN 0-330-26738-8. {{cite book}}: Unknown parameter |published= ignored (help)
  125. Douglas Adams (1 Januari 1980). The Restaurant at the End of the Universe. New York: Ballantine Books. ISBN 0-345-39181-0.
  126. Douglas Adams (1985). So Long, and Thanks for All the Fish. London: Pan. ISBN 0-330-28700-1. {{cite book}}: Unknown parameter |published= ignored (help)
  127. 127.0 127.1 Monty Python's Completely Useless Web Site: Monty Python's The Meaning Of Life: Complete Script
  128. Terry Burnham (2005). Mean Markets and Lizard Brains: How to Profit from the New Science of Irrationality. John Wiley and Sons. ISBN 0471716952.
  129. Yolanda Fernandez (2002). In Their Shoes: Examining the Issue of Empathy and Its Place in the Treatment of Offenders. Wood 'N' Barnes Publishing. ISBN 1885473486.
  130. Mark I. Pinsky (2001). The Gospel According To The Simpsons: The Spiritual Life Of The World's Most Animated Family. Westminster John Knox Press. ISBN 0664224199.
  131. Matt Lawrence (2004). Like a Splinter in Your Mind: The Philosophy Behind the Matrix Trilogy. Blackwell Publishing. ISBN 1405125241.
  132. Christopher Grau (2005). Philosophers Explore the Matrix. Oxford University Press.

Viungo vya nje

Jumla

Kisayansi

Kifalsafa

Kiroho