Mtihani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mtihani ni njia ambayo mtu anapimwa kutokana na alichokisoma au alichofundishwa ili atambuliwe kwamba alielewa au hakuelewa. Au ni kipimo cha maisha kutokana na ulichojifunza.

Katika shule mwanafunzi hupimwa na walimu wake juu ya kile walichomfundisha ili kumjua kama anaelewa au haelewi.

Mitihani yaweza kuwa migumu au rahisi kutokana na mwanafunzi mwenyewe: kama huwa hajisomei ataiona migumu na kama anajisomea ataiona rahisi hata kama mwalimu alitunga migumu kiasi gani.

Sifa za mwanafunzi[hariri | hariri chanzo]

  • 1) Mwanafunzi kama hajaelewa anatakiwa kuuòiza bila ya kuogopa kupigwa
  • 2) Anatakiwa kuwaheshimu walimuj na wanafunzi wenzake ili ajenge upendo baina yao
  • 3) Ajenge ushirikiano na wenzake katika kufanya kazi walizopewa
  • 4) Kama amepewa mtihani asimsaidie/asisaidiwe maana ni kipimo cha uelewa wao
  • 5) Mwanafunzi anatakiwa afanye kazi alizopewa kwa muda aliopangiwa bila kuchelewa.

Mwanafunzi akifaulu mtihani tunasema kuwa alielewa na hupewa zawadi na walimu na wazazi nyumbani kama pongezi, hivyo basi mwanafunzi anapopewa zawadi hujijengea kwamba ili apewe zawadi inambidi asome kwa bidii sana.

Katika shule huwa na mashindano ya wanafunzi ili waweze kumpata wa kwanza kati yao. Mitihani hutungwa na walimu wenyewe. Huwa na mtihani wa wiki, mwezi, robo mhula, nusu mhula na mtihani wa mwisho.

Katika mitihani asilimia kubwa ya wanafunzi huwa na woga, ndiyo maana hupewa mitihani shuleni ili waizoee.

Nchini Tanzania kuna mtihani wa taifa: mtihani huo humvusha mwanafunzi katika daraja alilopo na kwenda katika hatua nyingine (kutoka shule ya msingi kwenda sekondari, kutoka sekondari kwenda chuo kikuu na hatimaye kufaulu na kutimiza malengo yako).

Faida za mitihani[hariri | hariri chanzo]

  • 1) Kwanza humfanya mtu azoee kitu fulani
  • 2) Humwondolea mwanafunzi uwoga juu ya kitu anachokifanya, n.k.

Ili tufaulu mitihani tunatakiwa tusome sana na kwa bidii juhudi kubwa sana.

Nuvola apps bookcase.svg Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtihani kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.