Woga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtoto mwenye hofu

Woga ni tabia ya kupatwa na hofu kupita kiasi inayokuwa ndani ya binadamu juu ya kitu au vitu fulanifulani. Wakati hofu ni ono la kawaida kwa binadamu na kwa wanyama wengi, woga ni tatizo la kisaikiolojia.

Kila mtu anaweza akawa na woga wake, huenda ukawa juu ya Mungu, malaika, shetani, roho, lakini pia juu ya mnyama, mahali, kifo, mauaji, giza n.k.

Saikolojia inaweza kumsaidia mtu kujitawala asije akashindwa na tabia hiyo hata kutotimiza majukumu yake maishani.