Nenda kwa yaliyomo

Uuaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mauaji)
Uaji katika nyumba - taswira ya Jacub Schikaneder (1890)

Uuaji (kwa Kiingereza: homicide) kwa macho ya sheria ni tendo la mtu mmoja linalosababisha kifo cha mtu mwingine.

Uuaji kwa maana hiyo unahitaji tendo la mtu ambalo limelengwa, unaweza kutokana kwa bahati mbaya, kwa kutojali au kupuuza hata bila nia ya kusababisha hasara, au kwa kusudi.

Kisheria mauaji huangaliwa kwa namna tofauti zinazoweza kutofautiana kati ya nchi na nchi kufuatana na mifumo mbalimbali ya sheria, kama ni jinai au la. Namna hizo ni pamoja na kuua bila kukusudia (Kuuwa bila kunuia, ing. manslaughter) au kuua kwa kukusudia (Kuua kwa kunuia, ing. murder)[1], kujitetea, kujilinda, kuua vitani, kuua kwa amri ya wakubwa, au kutekeleza adhabu ya kifo.

Sheria zinazofuata mapokeo ya Sheria ya Kiroma zinatofautisha mara nyingi kati ya mauaji yanayotekelezwa kwa kukusudia na bila kukusudia; sheria za nchi kama Marekani hutofautisha kati ya ngazi au uzito tofauti wa uuaji kwa kukusudia (first - second degree murder) ambayo haipo katika sheria zinazofuata mapokeo ya Uingereza kama Tanzania.

Kwa jumla dini zinakataza uuaji kama dhambi kubwa, ingawa si kila mara, hasa katika juhudi za kujihami dhidi ya mvamizi.

  1. Wakati wa kutunga makala hii kwenye Februari 2021 msamiati wa sheria ya jinai haujaamuliwa bado nchini Tanzania; kuna tafsiri tofauti ya istilahi za Kiingereza

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]

Kigezo:Wikimedia

Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uuaji kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.