Katekisimu

Codex Manesse, fol. 292v, "Mwalimu wa Esslingen" (Der Schulmeister von Eßlingen)
Katekisimu (kwa Kigiriki κατηχισμός, katekismos, kutokana na kata = "chini" + echein = "kusikika" masikioni) ni kitabu chenye muhtasari wa mafundisho ya imani na maadili ya Kikristo.
Vitabu vya namna hiyo vinatumika toka karne za kwanza za Kanisa la Magharibi hasa kwa kuandaa watu kupokea ubatizo na sakramenti nyingine.[1]
Mara nyingi mafundisho hayo yanatolewa kwa namna ya majibizano, yaani maswali yakifuatwa na majibu ambayo yanafaa kukaririwa.
Katekisimu ya Kanisa Katoliki, iliyotolewa na Papa Yohane Paulo II kufuatana na Mtaguso wa pili wa Vatikano, ndiyo katekisimu yake rasmi na ndiyo inayotumika zaidi duniani siku hizi.
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- Martin Luther, John Nicholas Lenker, Luther's two catechisms explained by himself, in six classic writings, Minneapolis, Minn., The Luther Press, 1908 – Google Books
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
- Catechism of the Catholic Church from the official website of the Vatican
- Search the Catechism of the Catholic Church
- Westminster Shorter Catechism From Christian Classics Ethereal Library
- Westminster Larger Catechism From Christian Classics Ethereal Library
- Heidelberg Catechism From Christian Classics Ethereal Library
- A Catechism of the Steam Engine at Project Gutenberg by John Bourne
- CatechismClass an interactive tool developed to provide the Catechism of the Catholic Church, Baltimore Catechism, and other Catholic catechisms in an integrated format
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Katekisimu kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |