Katekesi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yesu Kristo akiwahubiria wanafunzi wake (Injili Siysky, 1340 hivi).

Katekesi (kutoka kitenzi cha Kigiriki κατηχεῖν, kateekhein, maana yake "kufundisha kwa sauti", ambacho ni mnyambuliko wa ἠχεῖν ("kufanya isikike") ni ufafanuzi wa mpango wa imani ya Ukristo.

Hatua ya katekesi inafuata ile ya awali ya kutangaza mbiu ya Injili kwa watu ili waone jinsi habari njema ya kifo na ufufuko wa Yesu ilivyo muhimu kwao, hasa upande wa wokovu.

Kwa kawaida kazi ya katekesi inaongoza waamini kwenye sakramenti mbalimbali, kuanzia ubatizo. Anayejiandaa kuupokea anaitwa mkatekumeni.

Katekista kwa kawaida anatumia kitabu rasmi maalumu kinachoitwa katekisimu, mbali ya Biblia ya Kikristo.

Ujumbe wenyewe unaeleweka kuwa hasa Injili kadiri ya imani ya Kanisa, yaani yale ambayo lenyewe "linaungama, linaadhimisha, linaishi na linasali kila siku" (Papa Yohane Paulo II).

Chuo cha katekesi cha kwanza kilianzishwa na Panteno huko Aleksandria (Misri) mwishoni mwa karne ya 2, kikapata sifa hasa chini ya uongozi wa waandamizi wake, Klemens wa Aleksandria na Origenes.

Mbali ya hiyo Shule ya Aleksandria, wakati wa mababu wa Kanisa ilikuwa maarufu vilevile Shule ya Antiokia (huko Siria, leo nchini Uturuki).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Katekesi kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.