Shule ya Antiokia
Mandhari
Shule ya Antiokia ilikuwa kimojawapo kati ya vituo vikuu viwili vya teolojia na ufafanuzi wa Biblia ya Kikristo wakati wa Mababu wa Kanisa; kingine kilikuwa Shule ya Aleksandria. Majina ya vituo vyote viwili yalitokana na majiji vilipostawi katika Ukristo.
Wakati wanateolojia wa Aleksandria (Misri) walipenda zaidi kufafanua Biblia kiroho, wale wa Antiokia ya Siria (leo nchini Uturuki) walifuata zaidi maneno yenyewe. Matokeo ya tofauti hizo yalijitokeza katika teolojia kuhusu fumbo la Yesu Kristo yakasababisha mafarakano makubwa ya karne ya 5.[1][2]
Historia ya shule ya Antiokia inaweza kugawiwa katika vipindi vitatu:
- 170-mwanzo wa karne ya 4: Theofilo wa Antiokia, Eusebi wa Emesa, Akasio wa Kaesarea na Theodoro wa Heraklea.
- 350-433: Diodoro wa Tarso, Yohane Krisostomo, Theodoro wa Mopsuestia, Nestori.
- baada ya 433: Basili wa Seleukia na Genadio wa Konstantinopoli.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Shule ya Antiokia kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |