Klemens wa Aleksandria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Klemens wa Aleksandria (150-211/216).

Titus Flavius Clemens (anayejulikana zaidi kama Klemens wa Aleksandria; kwa Kigiriki: Κλήμης Αλεξανδρεύς, Klemes Alexandreus; Athens, 150 hivi; Aleksandria, 215 hivi) alikuwa mwanafalsafa na mwanateolojia wa Ukristo katika mji wa Aleksandria (Misri) mwanzoni mwa karne ya 3[1].

Huhesabiwa kati ya walimu muhimu wa Kanisa la kwanza.

Anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waanglikana na wengineo kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Desemba[2].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Opera omnia, 1715

Klemens alikuwa mwenyeji wa Ugiriki aliyezaliwa katika familia ya wapagani matajiri mjini Athens.

Baada ya kupokea imani ya Kikristo, alisafiri akitembelea walimu Wakristo katika nchi mbalimbali kama vile Ugiriki, Italia na Palestina hadi Misri.

Huko alipewa nafasi ya kufundisha kwenye Chuo cha Kikristo cha Aleksandria akishirikiana na mwanzilishi wake Panteno.

Jitihada ya Klemens ilikuwa kupatanisha imani ya Kikristo na dhana za falsafa ya Kigiriki. Alifaulu kufafanua Ukristo kwa wasomi wapagani na kuvuta wengi kwenye imani yake mpya.

Klemens alikuwa ndiye mwalimu wa Origene.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Maandishi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]