Matengenezo ya Kiprotestanti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Hizi ni tasnifu 95 za Luther

Matengenezo ya Kiprotestanti ni muda ambao ulitumiwa na watu kuelezea mifululizo ya matukio ambayo yametokea katika karne ya 16 katika Ukristo.

Tangu karne za nyuma waamini wengi wa kila ngazi, kama vile watakatifu na Erasmus wa Rotterdam, waliona uhitaji wa kurekebisha hali ya Kanisa Katolikihuko Ulaya, lakini juhudi zao hazikutosha.

Kati ya ukosoaji muhimu ni kama haya yafuatayo:

  • Kanisa lilionekana kuuza misamaha ya dhambi ili kupata fedha za kujengea Basilika la Mt. Petro huko Vatikani. Hili lilitazamwa kama kwamba matajiri wangeweza kununua tiketi za kuenda peponi wakati maskini wasingeweza - kinyume kabisa na Biblia inavyosema.
  • Watu wengi walikuwa hawaelewi ibada kwa sababu zilikuwa zikifuata vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kilatini, ambayo haikutumiwi tena katika maisha ya kawaida. Wachungaji tofauti walieleza mambo tofauti. Baadhi ya mambo hayo yana uhusiano na yaliyoandikwa katika Biblia (kitabu kitakatifu cha Kikristo). Wachungaji peke yao ndio walikuwa wanaweza kukisoma, kwa hiyo watu wa kawaida hawakujua mambo mengi kuhusu dini yao.

Watu kama Martin Luther na halafu Calvin waliyaona hayo, wakawa wanayapinga, lakini pia walibadilisha mafundisho mengi ya Kanisa, na kupelekea kuligawanya katika idadi kadhaa ya madhehebu ya Kiprotestant. Kutokana na hayo yalizuka vita vingi Ulaya kwa muda mrefu ambavyo viliishia kufanya watu wachukie dini.

Martin Luther alikuwa mtu wa kwanza kutafsiri Biblia kwa Kijerumani. Aliweza hata kuchapisha baadhi ya nakala, kwa sababu miaka ya nyuma Johannes Gutenberg alikuwa amegundua njia ya kuchapisha. Hivyo alitoa idadi ndogo ya nakala (imekisiwa kuwa 50-100) kwa kiasi kidogo kabisa.

Matengenezo ya Kiprotestanti yaliwachoma sana Wakatoliki na kupelekea kuongeza juhudi za kurekebisha upya Ukatoliki.

Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Matengenezo ya Kiprotestanti kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Matengenezo ya Kiprotestanti kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.