Muziki wa Kikristo
Muziki wa Kikristo ni muziki uliotungwa ili kutokeza imani ya Ukristo katika sanaa hiyo, kwa mfano katika kumsifu Mungu, kumshangilia Yesu Kristo, na kuomba msamaha wa dhambi.
Hivyo, tofauti na miziki mingine, lengo kuu si kuburudika na uzuri tu.
Namna zake ni tofautitofauti kadiri ya nyakati, madhehebu, utamaduni n.k. Mojawapo, kati ya zile za zamani zaidi, inaitwa muziki wa Kigregori, kwa sababu iliagizwa na Papa Gregori I itumike kanisani.
Matumizi makubwa zaidi ni yale ya ibada, ambapo waamini waliokusanyika wanaimba pamoja, mara nyingi wakiongozwa na kwaya na wakisindikizwa na ala za muziki.
Matumizi mengine ni wakati wa kutoa mahubiri na mafundisho hata barabarani.
Pengine yanafanyika makongamano maalumu kwa wapenzi wa muziki huo, na vilevile siku hizi unarekodiwa kwa vifaa vya teknolojia hata kwa matumizi ya mtu binafsi.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Boyer, Horace Clarence, How Sweet the Sound: The Golden Age of Gospel Elliott and Clark, 1995, ISBN 0-252-06877-7.
- Broughton, Viv, Too Close To Heaven – The Illustrated History Of Gospel Music, Midnight Books, 1996, ISBN 1-900516-00-4
- Albert E Brumley & Sons, The Best of Albert E Brumley, Gospel Songs, 1966, ISBN na-paperback Amazing Grace
- Darden, Robert, People Get Ready: A New History of Black Gospel Music Continuum International Publishing Group, 2005, ISBN 0-8264-1752-3.
- Heilbut, Tony, The Gospel Sound: Good News and Bad Times Limelight Editions, 1997, ISBN 0-87910-034-6.
- Zolten, Jerry, Great God A' Mighty!:The Dixie Hummingbirds – Celebrating The Rise Of Soul Gospel Music, Oxford University Press, 2003, ISBN 0-19-515272-7.
- "Ecclesiastical Music". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
- Enciclopedia Cecilia Ilihifadhiwa 17 Desemba 2014 kwenye Wayback Machine. (in Spanish) Includes a Catholic Encyclopedia about music, wiki-style
- Palackal, Joseph, Syriac Chant Traditions in South India Ilihifadhiwa 8 Februari 2012 kwenye Wayback Machine.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Muziki wa Kikristo kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |