Ukristo wa Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Matawi ya Ukristo yalivyotokea katika historia ya Kanisa. Upande wa juu ndio Kanisa la Magharibi, upande wa chini Makanisa ya Mashariki. Unene wa mistari haulingani na ukubwa wa madhehebu husika.

Ukristo wa Mashariki ni jina linalojumlisha madhehebu yote ya Ukristo yaliyotokea upande wa mashariki wa Bahari ya Kati na nje ya Dola la Roma yakiwa na mielekeo tofauti na ile ya Kanisa la Magharibi, ambalo ndilo aina ya Ukristo iliyoenea zaidi duniani pamoja na ustaarabu wa magharibi ulioathiriwa nayo.

Unajumlisha hasa makanisa ya Waorthodoksi wa Mashariki na Waorthodoksi, ambayo yalitengana na Kanisa la Magharibi hasa katika karne ya 5 na karne ya 11, pamoja na Makanisa Katoliki ya Mashariki ambayo yana ushirika kamili na Papa na Kanisa Katoliki lote.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • (2006) in Angold, Michael: The Cambridge History of Christianity Volume 5, Eastern Christianity. Cambridge University Press. ISBN 978-0-521-81113-2. 
  • Julius Assfalg (ed.), Kleines Wörterbuch des christlichen Orients , Wiesbaden 1975
  • Jenkins, Philip (2008). The Lost History Of Christianity. New York: HarperCollins. ISBN 978-0-06-147281-7. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

ChristianitySymbol.PNG Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ukristo wa Mashariki kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.