Utamadunisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makundi ya watoto na vijana ndiyo njia mojawapo muhimu ya utamadunisho.

Utamadunisho (kwa Kiingereza "enculturation") ni mchakato wa mtu kupokea utamaduni wa wale wanaomzunguka[1] ili kuingia zaidi katika maisha ya jamii husika.

Katika Ukristo[hariri | hariri chanzo]

Watoto wakicheza wakati wa Misa katika kanisa kuu la Basankusu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Katika Ukristo msamiati huo unamaanisha hasa mchakato wa ujumbe wa Injili kuingia kwa dhati zaidi katika maisha ya watu wa utamaduni fulani ili Kanisa lizidi kutia mizizi katika kabila au taifa husika badala ya kubaki kasumba.

Mchakato huo hauwezi kufanyika mara moja, bali unadai uwazi wa waumini kwa Neno la Mungu na kwa Roho Mtakatifu pamoja na jitihada za makusudi na za pamoja.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Grusec, Joan E.; Hastings, Paul D. "Handbook of Socialization: Theory and Research", 2007, Guilford Press; ISBN 1-59385-332-7, ISBN 978-1-59385-332-7; p 547.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Grace, Lindsay. "Handbook of Research on Computational Arts and Creative Informatics: The Challenge of Enculturation in the Arts, 2009, IGI Global Press; ISBN 978-1-60566-352-4; 312-324.
  • School & Society:Learning Content through Culture. Henry T. Trueba (editor), Concha Delgado-Gaitan (editor). Praeger Publishers. New York. 1988. p. 167

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]