Kasumba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Huko Marekani kulikuwa na kasumba ya watu weupe kuamini watu weusi wanapenda sana matikiti maji. Picha hii ilikuwa katika moja ya kadi zao za posta mnamo 1911.

Kasumba ni wazo au fikra/imani ya watu wengine kuhusu kitu au kundi la watu ya kwamba wana tabia fulani hasa kwa kumwonekano wao wa nje, ambapo kiasi fulani inaweza kuwa kweli au sio kweli.[1] Watu wenye kasumba ni aina fulani ya wale wanaopenda kuhukumu au kuchukia wenzao kwa sehemu fulani ya utu wao. Kasumba inaweza kutumiwa kwa sababu za kibaguzi dhidi ya mtu mwingine, au wakati mwingine hata uchale wa katika vipindi mbalimbali vya televisheni.

Huko Tanzania kuna kasumba ya watu wengi kuamini Wazaramo wanapenda ngoma kuliko kitu chochote, ilhali kila kabila nchini humo lina ngoma zao za asili, ila tu, ikiwa zamu ya Mzaramo maneno, tena mji mzima utajua. Kuna kasumba ya kuamini simu za Kichina ni mbovu, kasumba ya kuamini Wachagga ni wezi, Wahaya wanajidai na kadhalika. Hali kadhalika huko Ulaya na Marekani kuna baadhi ya Wazungu wanaoamini Waafrika hawawezi kupata maendeleo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Word Central Student Dictionary: Definition of Stereotype. Mirriam-Webster. Iliwekwa mnamo 01/14/2013.