Arthur Schopenhauer

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Arthur Schopenhauer  (22 Februari 1788 - 21 Septemba 1860) alikuwa Mwanafalsafa wa Ujerumani. Yeye anajulikana kwa kazi yake ya 1818 (The World as will and Representation) "Dunia kama wito na Uwakilishi" (kupanuliwa mwaka wa 1844), ambako anafafanua ulimwengu wa matukio kuwa uzao wa dhamira yakimetafizikia ambayo ni kipofu na isiyotosheka. Kutoka kwa dhana ngambo ya bara la uzoefu (Transendental idealism) ya Immanuel Kant, Schopenhauer alibuni mfumo wa kimetafizikia na wa kiMaadili ambao unaokana mungu ambao umeelezewa kuwa mfano wa falsafa za uhasi wa maisha (philosophical pessimism). Alikataa falsafa za rika lake za dhana kwamba ulimwengu ulitegemea michakato ya kikakili kwa kuwepo kwake; dhana zilizotawala falsafa za Ujerumani Karne hio(German Idealism). Schopenhauer alikuwa miongoni mwa wasomi wa kwanza katika falsafa ya Magharibi kushiriki na kuthibitisha mambo muhimu ya falsafa ya Mashariki (kwa mfano, utawa, ulimwengu-kama-kuonekana), baada ya kufikia hitimisho sawa kama matokeo ya kazi yake ya falsafa.  

Ingawa kasi yake haikupata umaarufu  wakutajika wakati alikua hai, Schopenhauer amekua na ushawishi mkubwa baada ya kifo chake kupitia kazi zake katika nyanja kadhaa, zikiwemofalsafa, fasihi na sayansi.

Maandishi yake juu ya esthete, maadili na saikolojia ilikua na ushawishi wa mkubwa kwa wasomi na wasanii wengi wa karne za 19 na 20. Wale wamemtaja nikama Friedrich Nietzsche, Albert Einstein Richard Wagner, Leo Tolstoy, Ludwig Wittgenstein, Erwin Schrödinger, Otto Rank, Gustav Mahler, Joseph Campbell, Carl Jung, Thomas Mann, Emile Zola, George Bernard Shaw, Guy de Maupassant, Jorge Luis Borges na Samuel Beckett.

Fikira[hariri | hariri chanzo]

Falsafa ya "wito"[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu: Dunia kama wito, na Uwakilishi

Lengo muhimu la Schopenhauer ilikuwa uchunguzi wake wa motisha ya mtu binafsi. Kabla ya Schopenhauer, Hegel alikua amemaarufisha dhana ya Zeitgeist, dhana kwamba jamii ikona fahamu unganifu ya pamoja ambayo inayosafiri kwa njia teule, na inatawala vitendo vya wanachama wake. Schopenhauer, msomaji wa Kant na Hegel Wote, alikashifu dhana zao za mantiki chanya (Logical optimism) na imani kwamba maadili ya mtu binafsi inaweza kuongozwa na jamii au sababu tupu. Schopenhauer alishikilia imani kuwa binadamu alipata motisha kwa msingi ya uchu na dhamira zao wenyewe au witoe zum Leben ( "wito wa kuishi"), ambayo yote ya wanadamu huelekezwa. wito, kwa mujibu wa Schopenhauer, ni kile Kant alichoita "kitu-ndani-yenyewe". [39]

Kwa Schopenhauer, tamaa ya kibinadamu haikuwa na maana, haijulikani, haielewi, na, kwa upanuzi, hivyo hatua zote zakibinadamu zinaambulia patupu. Einstein alifalisi maoni haya kama ifuatavyo: "Mtu anaweza kufanya kile anachotaka, lakini hawezi wito kile anachotaka." Kwa maana hii, alizizingatia kanuni ya Fichte yaulimwengu akili-tegemezi: "Dunia ni kwa raia." Dhana hii umewasilishwa jinsi kwamba, hutumika moja kwa moja kwa kubuni mtazamo wa kimaadili, hii ni kinyume na Descartes na Berkeley waliozingatia masuala ya kiepistemologia pekee yake. Kwa mujibu wa Schopenhauer, wito ni nguvu kipofu ambayo inatawala,sit u matendo ya watu binasfi, ihali maumbile yote ulimwenguni – na ni uovu ambao unapasawa kumalizwa na majukumu ya wanadamu: utawa na usafi wa moyo [40]. Ametambuliwa na kati moja ya mistari ya ufunguzi maarufu zaidi katika falsafa: "Dunia ni uwakilishi wangu." Friedrich Nietzsche aliathiriwa sana na wazo hili la wito, ingawa hatimaye aliukataa.

Sanaa na esthete[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu: esthete ya Arthur Schopenhauer

Kwa mujibu wa Schopenhauer, tamaa ya binadamu, "wito", na uchu husababisha mateso au maumivu. Njia ya muda mfupi ya kuepuka maumivu haya ni wa utafakari wakiusthete (kwa njia inayofanana na "Usablimashaji" wa Zapffe). Utafakari huu wakiusthete unaruhusu mtu kuepuka maumivu-hata hivyo kwa muda mfupi-kwa sababu hukomboa mtu kutokana kuona dunia kama tu mawasilisho. Badala yake, mtu husita kuangalia dunia kama kitu cha maonyesho  (kama raia chini ya katiba ya Kanuni za Misingi Yakutosha, wakati, nafasi na usababishi) ambapo mtu hupata kutengwanishwa; bali mtu anapata kunganishwa na  anakua mmoja na maonyesho: "mtu hataweza tena kutenganisha mtazamaji kutoka kwa mtazamo" (Dunia kama wito, na Uwakilishi, sehemu ya 34). Kutokana na kuzamishwa huku, mtu haijioni tena kibinafsi kama anayekabiliwa na mateso duniani kwa sababu ya uchu wake badala yake, anakua “raia wa ujuzi”  kwa mtazamo ambao ni “safi, huru kutoka wito, na wakati”( kifungu cha 34) ambapo kiini, "mawazo", ya dunia huonyeshwa. Sanaa ni dhana-tumizi zinazofuta huu utafakari mfupi wakiusthete ambapo inajaribu kuonyesha mtu amezamishwa ndani ya malimwengu, na hivyo hujaribu kuonyesha kiini / mawazo safi ya ulimwengu. Muziki, kwa mujibu wa Schopenhauer, ulikuwa ni aina safi kabisa ya sanaa Kwa sababu ilikuwa inaonyesha taswira ya  wito wenyewe bila kuenekana kama raia chini ya Kanuni ya Misingi za Kutosha , hivyo kama kitu kimoja. Kulingana na Daniel Albright, "Schopenhauer alifikiri kwamba muziki ndiyo pekee ya sanaa ambayo haikunakili mawazo, badala yake ililchukua mfumo wa wito wenyewe."

Alizingatia muziki kama huru kutoka wakati, lugha yakiulimwengu inayojulikana kila mahali, ambayo inaweza kuchanjia mataifa yote na uchangamfu, ikiwa imechukua mafuatano ya sauti maarufu.

Maadili[hariri | hariri chanzo]

Nadharia ya maadili ya Schopenhauer ilipendekeza kwamba kuwa ni  huruma tu ambayo inaweza kuendesha vitendo vya maadili. Kwa mujibu wa Schopenhauer, huruma peke yake ndio zuri katika kitu cha matendo, yaani, hawawezi kuongozwa na tumaini la matumizi yakibinafsi au hisia ya wajibu. Wanadamu pia wanaweza kuongozwa na ubinafsi , ufisadi na chuki. Vitendo vya ubinafsi na ufisadi ni zile ambazo huongozwa na masilahi binafsi, tamaa ya taanasa au kujinufaisha. Schopenhauer aliamini mengi ya matendo yetu ni ya darasa hili. Matendo ya chuki ni tofauti na matendo ya kibinafsi. Kama ilivyo katika matendo ya huruma, haya haijalenga matumizi au manufaa ya mtu kibinafsi. Lengo la matendo haya ni kusababisha uharibifu kwa wengine, bila kujipatia faida binafsi. Aliamini, kama Swami Vivekananda katika umoja wa wote na nafsi na pia aliamini kwamba ubinafsi ndio asili ya maumivu na migogoro, kwamba kupunguza ubinafsi ndio inaunda mipaka ya kanuni za maadili.

Adhabu[hariri | hariri chanzo]

 Kwa mujibu wa Schopenhauer, Wakati sisi hufanya uamuzi, "Sisi hudhani kwamba kama ni sharti uamuzi huo ulitanguliwa na jambo fulani ambapo ulipata kuibuka kutoka, na ni ile tunaitaita ‘msingi’ au ‘sababu’, au kwa usahihi zaidi ‘nia’, ya hatua iliyotekelezwa.”  Uchaguzi haufanyiki kwa uhuru. Matendo yetu hayawezi banduka na yameshapangwa mapema kwani "kila binadamu, hata kila kilicho hai, baada ya nia imeonekana, lazima apate kufanya hatua ambayo ni ya kipekee kwa mujibu wa tabia yake aliyozaliwa nayo na taratibu zisizobadilika." Hatua ya fulani dhahiri lazima ipate kutokea wakati ambapo nia maalum inaathiri tabia ya mtu ambayo amepewa na haibadiliki. Serikali, Schopenhauer alidai, huadhibu wahalifu kuzuia uhalifu wa baadaye. Inafanya hivyo kwa Kuweka "kando na kila nia inaweyozekana ya kufanya uhalifu nia ya nguvu zaidi ya kutoifanya, katika adhabu isiyoepukika. Kwa hiyo, kanuni ya jinai ni kama rejista kamili iwezekanavyo ya nia-pinganifu ya vitendo vyote jinai zinazoweza fikirika..”

... sheria na utimilifu wake, yaani adhabu, huelekezwa kimsingi kwa siku zijazo, si kwa siku za nyuma. Hii inatofautiana adhabu kwa kulipiza kisasi, kwani kulipiza kisasi kunahamasishwa na kilichotokea, na hivyo kwa siku za nyuma kama vile. Marejeleo yote ya kujibu mashambulizi kwa kusababisha maumivu fulani kwa wengine bila kuzingatia kokote kwa siku za usoni ni kulipisha kisasi, na haiwezi kua na lengo zaidi bali ile faraja kwa yale maumivu mtu amevumilia kwa kuona mateso yeye amemsababishia mwenzake. Kitu kama hicho ni uovu na ukatili, na haiwezi kuhalalishwa kimaadili .....  Nia ya adhabu.. ni kuepusha kutoka kwa uhalifu… Nia na azimio ya siku za usoni ndio inatenganisha adhabu na kulipisha kisasi, na kuadhibu ikona hii maana wakati tu inaitwa ili kutimiza sheria fulani.  Ni kwa njia hii tu ndio itaweza kutumika kwa namna isoyoepukika au kukosoleka kwa kesi zote za usoni; na hivyo inapea sheria nguvu ya kukomesha..

Je! Adhabu ya kifo zapaswa kuhalalishwa? “Ili kulinda maisha ya raia,”Schopenhauer alijibu, “adhabu ya kifo lazima zihitajike”. “Muaji, ambaye amehukumiwa kifo kwa mujibu wa sheria lazima atumike kama chombo, na haki kabisa. Ilikuzingatia usalama wa umma, ambao ndio wajibu mkuu wa serikali, na umepata kutishiwa na mtu huyu; kwa kikweli umepuuliziwa kama hukumu haijatekelezwa. Muuaji, maisha yake, utu wake, lazima awe chombo cha kutekeleza sheria, na hivyo rejesha usalama wa umma.” Schopenhauer alikataana na wale waliotaka adhabu ya kifo itupiliwe mbali. “Wale ambao wanaopendekeza ikomeshwe wanapaswa kupewa jibu:’ Kwanza toa mauaji kwa dunia, na kisha adhabu ya kifo itafuata”

Watu, kulingana na Schopenhauer, hawawezi kuimarishwa. Wanaweza kushawawishika tu na nia zenye nguzu zinazoshinda nia za uhalifu. Schopenhauer analitangaza kwamba “ubadilishaji wa maadili kwa kikweli haiwezekani kabisa, ila tu zuia njia kwa tendo..”

Alisema kwamba mafunzo haya hayakuwa na asili nayeye. Hapo mbeleni ilionekana kwa maandishi ya Plato, Seneca, Hobbes, Pufendorf, na Anselm Feuerbach. Schopenhauer alitangaza ya kwamba maadishi haya yalichafuliwa na makosa yaliyofuata na kwa hivyo ilikua na haja ya ufafanuzi.

Dhana ya kisiasa na ya kijamii[hariri | hariri chanzo]

Siasa[hariri | hariri chanzo]

Siasa za Schopenhauer zilikuwa, kwa sehemu kubwa, marejeleo ya mfumo wake wa maadili (ya jamii ilipata sauti kwa Die beiden Grundprobleme der Ethik, inayopatikana kwa kiingereza kwa vitabu viwili, On the Basis of Morality na On the Freedom of the wito ). Maadili pia ilimiliki karibu robo ya kazi yake kuu, Dunia kama wito na Uwakilishi

Katika maoni ya mara kwa mara ya siasa katika kazi zake za Parerga and Paralipomena na Manuscript Remains, Schopenhauer anajieleza mwenyewe kama mpendekezi wa serikali finyu. Cha mno, alidhani, ni kuwa serikali inapaswa “kuwacha kila mtu huru ajitafutie wokovu wake mwenyewe”,  na ikiwa serikali itasita kudoea au kuingilia haya, yeye alipendekeza zaidi “afadhali kutawaliwa na simba kuliko panya wenzake”- hiyo nikumaanisha, na mfalme, kuliko kiongozi wa demokrasia. Schopenhauer aliunga mkono maoni ya Thomas Hobbes ya umuhimu wa serikali, na wa utendakazi wake, kuchunga mielekeo yetu ya uharibufu ambayo ni ya undani na imeambatana na asili ya aina yetu. Yeye bado alitetea tawi huru za utunga-sheria, mahakama, na utekelezaji za nguvu, na aliona mfalme kama kipengele huru ambacho kinaweza tekeleza haki (anamaanisha katika matumizi ya kila siku, sio kwa maana ya kikosmologia). Alitangaza ufalme kama “kile ambacho ni cha hali ya kawaida kwa binadamu” kwani “uerevu daima chini ya serikali ya ufalme umekua ukipata nafasi bora zaidi kupiku adui wake mkuu, ujinga” alihujumu ujamhuri kama “yasiyo asili kwani inasusia hatua za uerevu wajuu, sanaa na sayansi”

Utata wa nungunungu[hariri | hariri chanzo]

 Utata wa nungunungu, ni fumbo wa changamoto zinazoathiri umoja na urafiki wa watu. Huelezea hali ambayo jamii ya nungunungu hujaribu kusongeana karibu pamoja ili kugawana joto katika msimu wa baridi. Lakini hupata kwamba zinaumizana na mishale yao mikali, hivyo wanapaswa kubaki mbali. Ingawa zote zilikua na nia ya uhusiano wa karibu wakusaidiana, hii huenda isifanyike, kwa sababu zisizoepukika.

Arthur Schopenhauer alitumia fumbo hili kuelezea dhana yake kuhusu hali ya mtu binafsi katika uhusiano wa ujamii na wengine. Utata wa nungunungu huonyesha kwamba ingawa nia njema, umoja na urafiki wa kibinadamu hauwezi fanyika bila kiasi fulani cha kuumizana, na huongoza watu kwa  tabia za kujitahadhari na husiano hafifu. Utata wa nungunungu, unapendekeza kuwa mpole na kutumia wastani katika uhusiano na wengine ili kujichunga, na pia kama njia ya kuzingatia wengine. Utata wa nungunungu umetumiwa na mwanasiakologia Sigmund Freud kueleza upweke na dhana za kujitenga.

Fumbo hii ilitoka kwa Parerga und Paralipomena, Volume II, Sura ya XXXI, Sehemu ya 396

Nungunugu kadhaa walikaribiana pamoja kutafuta joto katika siku ya baridi; lakini, vile walianza kuchomana na mishale yao, walilazimika kutawanyika. Lakini baridi iliwafukuza na kuwaleta tena pamoja, ambapo jambo lile lile lilifanyika tena. Hatimaye, baada ya mizunguko mingi ya kusogeana na kutawanyika, waligundua ni heri kubakisha nafasi kiasi kati yao. Kwa njia sawa, mahitaji hufanya nungunungu za kibinadamu kuletwa pamoja kwa ujamii, lakini hujipata wakisukumana na kuchomana na pembe za sifa mingi tofauti zinazopingana ambazo ziko kwa asili yao. Umbali wa wastani ambao hatimaye wanagundua ndio hali wanayoezaishi nayo, ni kanuni za upole na tabia mzuri; na wale wanopita mpaka huu wanaambiwa –kwa kiingereza- “keep your distance”. Kwa mpango huu mahitaji ya joto inatoshelezwa wastani tu; lakini pia watu hawadungwi. Mtu ambaye akona joto ndani yake anapendelea kubaki inje, ambapo hatadunga mtu wala hata dungwa yeye mwenyewe.