Tiba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Matibabu)
Jump to navigation Jump to search
Binadamu akipewa tiba na madaktari

Tiba (au: Uganga) ni elimu kuhusu magonjwa ya Binadamu mwilini na rohoni, jinsi ya kuzuia magonjwa na kuhusu njia ya kurudisha uzima. Elimu hii inafuata mbinu za kisayansi, tofauti na uganga wa kienyeji au wa kimila.

Watu wanaoshughulikia magonjwa ya watu huitwa matabibu au waganga. Mara nyingi watu huwaita "daktari", lakini neno hili lamaanisha zaidi cheo cha kufaulu chuo kikuu kwenye ngazi ya juu; mara nyingi waganga husoma hadi cheo cha daktari wa tiba.

Watu wanaofanya kazi pamoja na tabibu ni muuguzi (nesi) na wasaidizi wengine.

Tiba imeendelea kiasi cha kuwa na masomo yake madogo yanayoangalia hasa magonjwa ya sehemu fulani ya mwili tu. Kila somo dogo lina wataalamu wake. kwa mfano tiba ya moyo, ya ngozi, ya viungo vya ndani, ya upasuaji, ya magonjwa ya watoto na kadhalika.

Rod of Asclepius2.svg Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tiba kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.