Nenda kwa yaliyomo

Upasuaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wapasuaji wakikarabati mguu wa mtu

Upasuaji (kutoka kitenzi "kupasua": pia Operesheni kutoka Kiingereza "operation") ni matibabu maalumu yanayohusu tendo la kutibu mwili kwa kukata, na kurekebisha sehemu yenye maradhi au tatizo lingine lolote.

Mgonjwa ambaye anapasuliwa anaweza kuwa mtu au mnyama. Mpasuaji ni mtu ambaye hufanya upasuaji na mpasuaji msaidizi ni mtu ambaye husaidia katika operesheni.

Timu ya upasuaji huwa na mpasuaji, mpasuaji msaidizi, anayetia ganzi, muuguzi na fundi wa upasuaji.

Upasuaji wa kawaida huchukua muda wa dakika hadi saa kadhaa. 

Ufafanuzi

[hariri | hariri chanzo]

Upasuaji ni teknolojia yenye kuingilia tishu za kimwili .

Kwa jumla, utaratibu huchukuliwa kuwa upasuaji wakati unahusisha kukata tishu ya mgonjwa au kufungwa kwa jeraha

Aina zote za upasuaji huchukuliwa kama taratibu vamizi. Zinazochukuliwa kuwa si vamizi, haziingii muundo unaokatwa ama zinatumia mionzi.

Aina za upasuaji

[hariri | hariri chanzo]

Upasuaji kwa kawaida hujumuishwa kwa uharaka, aina ya utaratibu, mfumo wa mwili unaohusika, kiwango cha uvamizi, na vifaa maalum.

  • Kulingana na muda: upasuaji wa kuchagua hufanyika kurekebisha hali isiyotishia uhai, na hufanyika wakati mgonjwa ataomba kupasuliwa, baada ya chumba cha upasuaji na mpasuaji kuwa huru. Upasuaji wa nusu kuchagua ni ule ambao lazima ufanyike ili kuepuka ulemavu wa kudumu au kifo, lakini inaweza kuahirishwa kwa muda mfupi. Upasuaji wa dharura ni upasuaji ambao lazima ufanyike haraka ili kuokoa uhai, mguu/mkono, au uwezo wa kimwili.
  • Kulingana na kusudi: upasuaji ili kuchunguza hufanywa kusaidia au kuthibitisha utambuzi. Upasuaji wa matibabu hufanywa kutibu baada ya utambuzi. Upasuaji wa upodozi hufanyika 'kuboresha' muonekano.
  • Na aina ya utaratibu: Kukatwa kunahusisha kukata sehemu ya mwili, kama vile mkono au mguu; kuhasiwa ni pia mfano. Resection ni kuondolewa kwa kiungo chote cha au sehemu yote ya mwili, au sehemu muhimu (ini, figo n.k.) ya kiungo au sehemu ya mwili ambayo ina jina lake maalum. Kupandika kunahusisha kupachika sehemu ya mwili iliyogawanyika. Upasuaji upyaji unahusisha 'kurudisha upya' sehemu ya mwili iliyokatwa, iliyoumizwa au iliyoharibiwa. Ukataji ni kukata au kuondolewa kwa sehemu ya kiungo, tishu, au sehemu nyingine ya mwili kutoka kwa mgonjwa. Upasuaji wa kupandikiza ni kubadilisha kiungo au sehemu ya mwili kwa kuiingiza nyingine kutoka binadamu (au mnyama) mwengine katika mwili mgonjwa. Kuondoa kiungo au sehemu ya mwili kutoka kwa binadamu au mnyama anayeishi kwa ajili ya matumizi katika kupandikiza pia ni aina ya upasuaji.
  • Na sehemu ya mwili: Wakati upasuaji unafanyiwa kiungo, mfumo au muundo mmoja, unaweza kujumuishwa kwa kiungo, mfumo wa kiungo au tishu zinazohusika. Mifano ni pamoja na upasuaji wa moyo (inafanyiwa moyo), upasuaji wa utumbo (hufanyiwa utumbo na viungo njiani yake), na upasuaji wa mifupa (hufanyiwa mifupa au misuli).
  • Na kiwango cha uvamizi wa upasuaji: Upasuaji vamizi kidogo unahusisha kutengeneza chale(s) ndogo nje ili kuingiza vyombo vidogo zaidi ndani ya muundo wa mwili. Kwa upande wake, upasuaji wazi unahitaji chale kubwa ya kupata eneo linalohitajika.
  • Na vifaa vya kutumika: Upasuaji wa Laser inahusisha matumizi ya laser kwa ajili ya kukata tishu badala ya wembe vyombo vya upasuaji. Microsurgery inahusisha matumizi ya uendeshaji hadubini mpasuaji aone miundo midogo. Upasuaji kwa roboti hufanya upasuaji kutumia roboti.

Maelezo ya utaratibu wa upasuaji

[hariri | hariri chanzo]

Katika hospitali ya kisasa ya upasuaji ni mara nyingi hufanywa ndani ya thieta ya upasuaji kwa kutumia vifaa vya upasuaji, meza ya upasuaji ya mgonjwa, na vifaa vingine. Vyombo vya upasuaji lazima visafishwe kabisa, na kifaa lazima kibadilishwe au kisafishwe tena kama kimepata uchafu (kwa mfano kwa kugusisha kifaa cha upasuaji kwenye uso wa mpasuaji au mahali ambapo hapajasafishwa kabisa, chombo kinachukuliwa kuwa chafu). Wafanyakazi walio ndani ya thieta lazima wavalie nguo zilizosafishwa kabisa (nguo za daktari, kofia/kitambaa, gauni ya daktari, glavu safi, na barakoa), na lazima wasugue mikono kwa kuipitisha kwenye kemikali ya kuua bakteria kabla ya utaratibu wowote.

Huduma kabla ya upasuaji

[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya upasuaji, mgonjwa anapewa anachunguzwa kimatibabu, anafanyiwa majaribio kabla ya upasuaji, na hali ya mwili kurekodiwa. Kama matokeo haya ni ya kuridhisha, mgonjwa hutia saini katika fomu ya ridhaa na kupewa kibali cha kupasuliwa. Kama utaratibu unatarajiwa kumfanya mpasuliwa kupoteza damu nyingi, ombi la mchango wa damu wiki kadhaa kabla ya upasuaji. Kama upasuaji unahusisha mfumo wa utumbo, mgonjwa anaweza kuelekezwa kutayarisha matumbo kwa kunywa polyethilini glycol usiku kabla ya operesheni. Wagonjwa pia wanafaa kujinyima chakula na vinywaji ili kupunguza hatari ya upumuo wakati wa operesheni.

Baadhi ya mifumo ya matibabu hufanya eksirei mara kwa mara kabla ya upasuaji. Sababu yake ni daktari huenda akagundua hali ya kimatibabu ambayo ingetatiza upasuaji. Akiwa na ujuzi huo, anaweza kubadilisha namna ya upasuaji ule umpendelee mgonjwa.[1] Hata hivyo, wataalamu wengine hawapendelei kufanywa kwa eksirei wakati huu.  Vile vile, majaribio ya damu na mkojo hayafai kufanywa wakati huu.[2]

Matayarisho kwa ajili ya upasuaji

[hariri | hariri chanzo]

Mgonjwa huvalia mavazi aliyopewa avalie wakati wa upasuaji. Ishara muhimu hurekodiwa na mgonjwa hupewa dawa za kabla ya upasuaji (viuavijasumu, dawa za kutuliza maumivu n.k.). Mgonjwa akiingia ndani ya chumba cha upasuaji, ngozi iliyo mahali patakapopasuliwa husafishwa kwa kutumia antiseptiki kupunguza uwezekano wa maambukizi. Kama pana nywele, nywele hunyolewa kabla ya kusafishwa. Mgonjwa husaidiwa na anayefanya anaesthesia kutengeneza nafasi ya kupasuliwa, halafu pazia safi hutumiwa kuziba nafasi ile. [3]

Ganzi au nusukaputi hutumika kuzuia maumivu kutoka kwenye chale au tishu kufanyiwa jambo. 

Upasuaji

[hariri | hariri chanzo]

Chale hufanywa ili kufikia palipo na shida. Mishipa ya damu inaweza kubanwa au kuchomelewa ili kuzuia kutokwa na damu, na retractors hutumika nje kuweka sehemu iliyopasuliwa wazi. Mbinu ya kufikia sehemu iliyo na shida inaweza kuhusisha kukata ndani sana. Nyakati nyingine, mfupa unaweza kukatwa ili kufika ndani ya mwili; kwa mfano, kukata fuvu kwa ili kuufikia ubongo

Kazi ya kusahihisha tatizo katika mwili huendelea. Kazi hii inaweza kuhusisha:

  • Kukata
  • Kuondolewa sehemu ya kiungo
  • Kuunganisha viungo, tishu, nk.
  • Kusahihisha - kama vile pua lililovunjika
  • Kufunga mishipa.
  • Kupandikiza
  • Kuingiza sehemu iliyosanidiwa.
  • Kutengeneza ufunguzi mwilini.
  • Kuunganisha mifupa
  • Kukarabatisha fistula
  • taratibu nyinginezo

Mgonjwa anaweza kuongezewa damu ili kulipiza aliyopotea. Baada ya upasuaji, palipokuwa pamekatwa hufungwa angalau kwa kushonwa. Baada ya chale kufungwa, gesi za anaesthesia hukatizwa.[4]

Huduma baada ya upasuaji

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kukamilika kwa upasuaji, mgonjwa huhamishwa kwenye kitengo kingine ili apate nafuu kutokana na anaesthesia aliyifanyiwa na kufuatiliwa kwa karibu. Wakati mgonjwa anadhaniwa kupata nafuu kutokana na anaesthesia, yeye huhamishiwa mahali pengine katika hospitali au kuruhusiwa kurudi nyumbani. [5] 

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Insha kuhusu upasuaji kutoka Misri

Misri Ya Kale

[hariri | hariri chanzo]

Matibabu ya upasuaji hurudi nyuma hadi zama za kabla ya historia tunayoijua. Operesheni kuu zaidi ambayo ina ushahidi ni trepanation,[6] ambapo shimo hutobolewa katika fuvu, ili kutibu matatizo ya afya yanayohusiana na shinikizo la damu kichwani na magonjwa mengine. Shughuli za upasuaji zilifanywa na makuhani, katika matibabu yaliyo karibu na ya kisasa.[7][8] Maambukizo yalitibiwa kwa asali.[9]

Upasuaji wa kisasa

[hariri | hariri chanzo]

Udhibiti wa maumivu kwa njia ya anesthesia uligunduliwa katikati mwa karne ya 19. Kabla ya ujio wa anesthesia, upasuaji ilikuwa utaratibu  wenye uchungu vibaya sana na wapasuaji walijaribu kufanya operesheni haraka iwezekanavyo ili kupunguza mateso kwa mgonjwa. 

Matumizi ya Eksirei kama sehemu muhimu ya zana ya uchunguzi wa kimatibabu ilianza na ugunduzi wa miale ya Eksirei katika 1895 na mwanafizikia Mjerumani  Wilhelm Röntgen. Yeye aliona kwamba miale hiyo inaweza kupenya ngozi na kuruhusu mfumo wa mifupa kuonekana.

  1. American College of Radiology. "Five Things Physicians and Patients Should Question". Choosing Wisely: an initiative of the ABIM Foundation. American College of Radiology. Iliwekwa mnamo Agosti 17, 2012Kigezo:Inconsistent citations{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: postscript (link), citing
  2. American Society for Clinical Pathology, "Five Things Physicians and Patients Should Question", Choosing Wisely: an initiative of the ABIM Foundation, American Society for Clinical Pathology, iliwekwa mnamo Agosti 1, 2013{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link), which cites
  3. Martin, Shirley (2007). Minor Surgical Procedures for Nurses and Allied Healthcare Professionals. England: John Wiley & Sons, Ltd. uk. 122. ISBN 978-0-470-01990-0.
  4. Askitopoulou, H., Konsolaki, E., Ramoutsaki, I., Anastassaki, E. Surgical cures by sleep induction as the Asclepieion of Epidaurus. The history of anesthesia: proceedings of the Fifth International Symposium, by José Carlos Diz, Avelino Franco, Douglas R. Bacon, J. Rupreht, Julián Alvarez. Elsevier Science B.V., International Congress Series 1242(2002), pp. 11–17. [1]
  5. Doyle S. L.; Lysaght J.; Reynolds J. V. (2010). "Obesity and post-operative complications in patients undergoing non-bariatric surgery". Obesity Reviews. 11 (12): 875–886. doi:10.1111/j.1467-789X.2009.00700.x.
  6. Capasso, Luigi (2002). Principi di storia della patologia umana: corso di storia della medicina per gli studenti della Facoltà di medicina e chirurgia e della Facoltà di scienze infermieristiche (kwa Italian). Rome: SEU. ISBN 88-87753-65-2. OCLC 50485765.{{cite book}}: CS1 maint: unrecognized language (link)
  7. Shiffman, Melvin. Cosmetic Surgery: Art and Techniques. Springer. uk. 20. ISBN 978-3-642-21837-8.
  8. Sullivan R (1996). "The Identity and Work of the Ancient Egyptian Surgeon". Journal of the Royal Society of Medicine. 89 (8): 469.
  9. James P. Allen, The Art of Medicine in Ancient Egypt. (New York: The Metropolitan Museum of Art, 2005) 72.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Upasuaji kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.