Eksirei

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Eksirei
Eksirei

Eksirei ni aina ya mionzi ya umeme. Eksirei ni mawimbi ya mionzi ya X.

Eksirei ina urefu wa wimbi mfupi, na hivyo zina nishati kubwa zaidi kuliko mionzi urujuanimno. Hizo zina urefu wa wimbi mfupi sana kuliko mwanga unaoonekana (mwanga ambao tunaweza kuona). Mionzi yenye urefu wa wimbi mfupi (nishati zaidi) kuliko eksirei inaitwa mionzi ya Gamma. Hizi ni sehemu zote za wigo wa umeme.

Urefu wa wimbi wa eksirei hufunika mahali mbalimbali. Eksirei nyingi zina urefu wa wimbi katika kiwango cha 0.01 hadi 10 nanometa. Hii inafanana na mawimbi katika petahezi 30 hadi exahezi 30 (3 × 1016 Hz hadi 3 × 1019 Hz) na nguvu katika kiwango cha 100 eV hadi 100 keV.

Eksirei inaweza kupita kwenye vitu vingi yabisi. Kwa sababu hii, huchukua picha mfano za mifupa ndani ya mwili.