Urujuanimno

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Urujuanimno upande wa lukoka fupi zaidi ya spektra inayoonekana

Urujuanimno (ing. ultraviolet, kifupi UV) ni aina ya nuru isiyoonekana kwa binadamu lakini kwa wanyama mbalimbali. Kwa lugha nyingine na makini zaidi ni sehemu ya mnururisho wa sumakuumeme mwenye lukoka (wavelength) baina ya nanomita 400 nm hadi 10 nm, ambayo ni lukoka fupi kuliko urujuani inayoonekana lakini ndefu zaidi kuliko eksirei.

Wanyama wengi pamoja na wadudu kadhaa, mamba, ndege wengine wadogo wanaweza kutambua urujuanimno. Mnururisho wa urujuanimno unafika duniani kama sehemu ya nuru ya jua.

Mnururisho wa urujuanimno na afya ya watu[hariri | hariri chanzo]

Viwango vikubwa vya mnururisho wa urujuanimno vinaweza kusababisha uharibifu kwa seli za binadamu. Ngozi ya binadamu inajenga rangi ya melanini kama kinga dhidi yake. Tabaka ya ozoni katika angahewa ya Dunia inachuja sehemu ya mnururisho huu lakini kwenye maeneo ya ikweta kiwango kinachopita hadi uso wa dunia ni kubwa zaidi.

Hapo ni sababu ya kwamba watu katika maeneo karibu na ikweta wana rangi nyeusinyeusi zaidi. Watu wanaoishi mbali na ikweta hawahitaji kiwango hiki cha kinga dhidi ya mnururisho wa urujuanimno na kwa sababu hiyo watu wenye rangi nyeupe zaidi waliweza kuendelea huko kaskazini. Pale ambako watu kutoka sehemu za kaskazini walihamia katika maeneo ya ikweta wana hatari kubwa zaidi kupata kansa ya ngozi na hii inaonekana katika asilimia kubwa ya kansa hii kati ya wazungu wa Australia.

Asilimia kubwa ya kansa ya ngozi kati ya watu walioathiriwa na zeruzeru katika Afrika ina sababu hiyohiyo.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Kujisomea[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
     . PMID 15262692
      . http://archderm.jamanetwork.com/article.aspx?articleid=480678.
     . PMID 12511035
      . http://www.bioone.org/doi/abs/10.1562/0031-8655(2002)076%3C0561%3AAHOUPF%3E2.0.CO%3B2.