Ozoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ozoni (kwa Kiingereza: ozone, pia trioxygen) ni molekuli yenye alama ya O3 inayofanywa na atomi tatu za oksijeni.

Tabia[hariri | hariri chanzo]

Inaonekana kama gesi ya buluu yenye harufu kali. Inatokea katika matabaka ya juu ya angahewa ambako mnururisho wa urujuanimno unapasua molekuli za O2.

Inatokea pia katika mazingira ya mashine kama ya fotokopi zinazotumia volteji ya juu.

Si molekuli thabiti, hivyo inasambaratika tena baada ya muda.

Tabaka la ozoni[hariri | hariri chanzo]

Ozoni hupatikana kwa viwango vidogo vya ppm 0.6 katika angahewa. Kiasi kikubwa kipo kwenye tabakastrato baina ya kilomita 10 hadi 50 juu ya uso wa ardhi. Tabaka hili lenye ozoni linafyonza asilimia kubwa ya mnururisho wa urujuanimno (93-99%) ulio hatari kwa viumbehai duniani.

Athari kwa viumbehai[hariri | hariri chanzo]

Katika matabaka ya chini ya angahewa ozoni ni sumu kwa viumbehai ikitokea kwa viwango juu ya ppm 0.1. Kwa binadamu inaweza kukera pua na koo pamoja na kuleta kichefuchefu. Kuathiriwa kwa muda mrefu kunaweza kuleta kufura kwa mapafu[1].

Ppm 0.100 ni kiwango cha juu kinachoruhusiwa ndani ya karakana, viwanda au ofisi katika nchi kama Uingereza, Japani, Ufaransa, Uholanzi na Ujerumani.

Matumizi[hariri | hariri chanzo]

Kutokana na nguvu yake ya kuoksidisha, ozoni hutumiwa kwa madhumuni mbalimbali:

  • kusafisha maji: ozoni inaua bakteria na algae hivyo hutumiwa katika mchakato wa kusafisha maji kwa matumizi ya viwandani na maji ya kunywa

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Ozone backround information, Effects on humans, tovuti ya National Center for Biotechnology Information, iliangaliwa Mchi 2019
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ozoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.