Tabakastrato

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Tabakastrato katika angahewa

Tabakastrato (pia angastrato, kwa Kiingereza: stratosphere) ni tabaka mojawapo la angahewa ya Dunia. Inaanza takriban kilomita 8 juu ya uso wa ardhi (nchani; kilomita 18 juu ya ikweta) hadi kilomita 50.

Katika tabakastrato halijoto inapanda juu pamoja na kimo. Hii inasababishwa na ozoni iliyoko. Ozoni hufyonza mnururisho wa urujuanimno kutoka nuru ya Jua na kuibadilisha kuwa joto.

Hii ni tofauti na tabakatropo iliyoko chini yake. Huko halijoto inapungua kadiri ya kupungua kwa kimo. Pia katika tabakameso iliyoko juu ya tabakastrato halijoto inapungua kadiri ya kufikia juu zaidi.

Hakuna upepo wala mawingu katika tabakastrato, hivyo eropleni kubwa husafiri huko kwa safari za mbali ambako vurugu kutokana na upepo wa tabakatropo zimeshapungua.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tabakastrato kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.