Nenda kwa yaliyomo

Melanini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Viinitete (embryo) viwili vya samaki, juu chenye melanini, chini bila melanini

Melanini ni jina la pigmenti katika ngozi ya juu zinazofanya ngozi kuwa na rangi asilia fulani. Inapatikana pia katika nywele na sehemu za jicho.

Kazi ya melanini inaaminiwa kupunguza athira ya mnururisho wa urujuanimno (ing. ultraviolet) katika nuru ya jua. Watu wenye melanini nyingi yaani rangi nyeusi-nyeusi huathiriwa mara chache na kansa ya ngozi kuliko watu wenye rangi nyeupe-nyeupe. Hii ni sababu ya kwamba katika mazingira penye nuru kali zaidi (kama karibu na ikweta) mara nyingi watu huwa na melanini nyingi hivyo rangi nyeusi-nyesi kuliko watu katika mazingira penye nuru hafifu zaidi.

Ukosefu wa melanini husababisha mtu kuwa albino.


Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]