Albino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Pengwini Albino
Mwanamuziki Salif Keita kutoka nchini Mali
Mvulana Mwafrika albino

Albino (kutoka Kilatini "albus", yaani "mweupe", au Zeruzeru) ni mtu anayekosa rangi ya melanini katika ngozi, nywele na macho au anayo kwa kiwango kidogo sana tu. Ualbino hutokea kwa watu na pia kwa wanyama.

Asili[hariri | hariri chanzo]

Mtu huzaliwa na ualbino, ni hali ya kurithiwa kama wazazi wote wawili wana jeni inayoruhusu ualbino. Hii inawezekana hata kama wazazi wote wawili hawaonyeshi dalili za ualbino wenyewe. Tabia inaendelea katika familia na inaweza kuonekana mara kwa mara au baada ya kizazi tu. Inategemea na kupatikana kwa jeni husika katika wazazi wote wawili.

Ugonjwa huo unapatikana Afrika Mashariki kuliko sehemu nyingine za dunia. Kwa mfano, nchini Tanzania kuna albino 1 kwa wakazi 1,400, kumbe wastani wa kimataifa ni 1 kwa 20,000.

Albino huzaliwa na hali ya kukosa uwezo wa kujenga pigmenti hii ambayo ni muhimu kama kinga dhidi ya mnururisho wa jua. Watu wenye ualbino huwa na nywele nyeupe au njano, na ngozi nyeupenyeupe. Macho yao ni buluu au hata pinki.

Watu wanaoathiriwa sana na ualbino mara nyingi huwa na matatizo ya macho, pia wako katika hatari ya kubabuka kwa jua na kupata kansa ya ngozi.[1]

Tukiacha matatizo ya macho na hatari ya kansa ya ngozi, albino ni mtu wa kawaida hana afya mbaya lakini anapaswa kujihadhari asikae kwenye jua muda mrefu bila kinga.

Ushirikina[hariri | hariri chanzo]

Pengine katika jamii kuna watu wenye maono mabaya dhidi ya wazeruzeru. Kuna pia imani potovu, hasa katika sehemu za Afrika (ambako zeruzeru anaonekana sana kuliko sehemu nyingine za dunia ambako watu wengi huwa na ngozi nyeupe kiasi) ya kwamba miili ya albino huwa na nguvu ya uchawi. Imani hiyo ilisababisha mauaji ya maalbino kwa kusudi la kutumia sehemu za miili yao kwa uchawi. Nchini Tanzania katika miaka 2000-2015 walau watu 75 waliuawa hivyo.[2]

Watu mashuhuri walioathiriwa na ualbino[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.albinism.org/publications/what_is_albinism.html What is albinism?
  2. Tanzania police arrest 32 witch-doctors over ritual albino killings (Guardian-UK Friday 6 March 2015)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: