Zeruzeru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Albino American Alligator, Alligator mississippiensis katika California Academy of Sciences.
Baba na Mama wana jozi ya jeni ya kutawala melanini, 1 nzima na 1 bovu, kati ya watoto wanne uwezekano mkubwa ni *1 anazaliwa bila kuendeleza jeni bovu, *2 wakiendelea kubeba jeni bovu lakini hawaonekani, *1 akirithi jeni mbili bovu na kuonekana ni albino
Mwanamuziki Salif Keita kutoka nchini Mali
Pengwini Albino
Mvulana Mwafrika albino

Zeruzeru (kutoka Kizaramo / Kizigua "zeu" nyeupe[1]) au Albino (kutoka Kilatini "albus", yaani "mweupe") ni mtu anayekosa pigmenti ya melanini katika ngozi, nywele na macho au anayo kwa kiwango kidogo sana tu. Uzeruzeru au ualbino hutokea kwa watu na pia kwa wanyama.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Waathiriwa wenyewe nchini Tanzania waliamua wanapendelea kuitwa "watu wenye ualbino" kutokana na matumizi mabaya ya neno zeruzeru katika utamaduni wa Afrika ya Mashariki ambako watu mara nyingi waliona uhusiano kati ya waathiriwa na mapepo[2].

Asili[hariri | hariri chanzo]

Albino huzaliwa na hali ya kukosa uwezo wa kujenga pigmenti ya melanini ambayo ni muhimu kama kinga dhidi ya mnururisho wa jua. Watu wenye ualbino huwa na nywele nyeupe au njano, na ngozi nyeupenyeupe. Macho yao ni buluu au hata pinki.

Uwezo wa kujenga melanini mwilini hutawaliwa na jeni fulani. Kama jeni zote ianpatikana kwa jozi katika kromosomu za seli. Hali inatokea ya kwamba jeni moja katika jozi hii ni bovu. Tabia hii ni dhaifu, yaani jeni 1 nzima inatosha kuendelea na kutengeneza melanini. Lakini jeni zote mbili zinaingia katika urithi wa watoto wakati wa kuzaa. Mtu huzaliwa na ualbino, ni hali ya kurithiwa kama wazazi wote wawili wana jeni inayoruhusu ualbino. Hii inawezekana hata kama wazazi wote wawili hawaonyeshi dalili za ualbino wenyewe. Tabia hii inaendelea katika familia na inaweza kuonekana mara kwa mara au baada ya kizazi tu. Inategemea na kupatikana kwa jeni husika katika wazazi wote wawili.

Maana yake urithi wa ualbino unaweza kuendelea katika familia kwa vizazi kadhaa bila mtoto kutokea vile. Lakini pale ambako mume na mke wenye rangi ya kawaida walio na jeni hii wanazaa pamoja watoto wanaweza kutokea albino. Kijenitiki ualbino ni tabia dhaifu na kufuatana na sheria ya Gregor Mendel inatokea kwa wastani kwa mtoto mmoja kati ya watoto wanne.[3]

Athari[hariri | hariri chanzo]

Ualbino mara nyingi huitwa ugonjwa ingawa hii inategema jinsi ya kufafanua "ugonjwa".

Albino huzaliwa na hali ya pekee inayoweza kupunguza uwezo wake wa kuona vizuri lakini hii si lazima. Yuko hatarini ya kuchomwa kwenye ngozi na kupata magonjwa kutokana na athari ya nuru ya jua. Hali yake haiongezeki maishani mwake isipokuwa kama hali yake inasababisha uonjwa kutokea.

Ualbino huo unaweza kuathiri watu wa kila rangi lakini kwa sababu zisizoeleweka bado unapatikana Afrika Mashariki zaidi kuliko sehemu nyingine za dunia. Kwa mfano, nchini Tanzania kuna albino 1 kwa wakazi 1,400, kumbe wastani wa kimataifa ni 1 kwa 20,000.

Watu wanaoathiriwa sana na ualbino mara nyingi huwa na matatizo ya macho, pia wako katika hatari ya kubabuka kwa jua na kupata kansa ya ngozi.[4]

Tukiacha matatizo ya macho na hatari ya kansa ya ngozi, albino ni mtu wa kawaida hana afya mbaya lakini anapaswa kujihadhari asikae kwenye jua muda mrefu bila kinga.

Ushirikina[hariri | hariri chanzo]

Pengine katika jamii kuna watu wenye maono mabaya dhidi ya wazeruzeru. Kuna pia imani potovu, hasa katika sehemu za Afrika (ambako albino anaonekana sana kuliko sehemu nyingine za dunia ambako watu wengi huwa na ngozi nyeupe kiasi) ya kwamba miili ya albino huwa na nguvu ya uchawi. Imani hiyo ilisababisha mauaji ya maalbino kwa kusudi la kutumia sehemu za miili yao kwa uchawi. Nchini Tanzania katika miaka 2000-2015 walau watu 75 waliuawa hivyo.[5]

Watu mashuhuri walioathiriwa na ualbino[hariri | hariri chanzo]

msichana mwenye albinizim kutokaPapua Guinea mpya

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. linganisha kamusi ya Sacleux, "Zeu-zeu"
  2. Hapa jina sahihi la kuita wtu wenye albinism[dead link], tovuti ya mtembezi.com, toleo la 9 Juni 2016 (ilitazamiwa 15 Juni 2016)
  3. understanding genetics: Albinism can be hidden Archived 23 Juni 2016 at the Wayback Machine., ilitazamiwa Juni 2016
  4. http://www.albinism.org/publications/what_is_albinism.html Archived 14 Mei 2012 at the Wayback Machine. What is albinism?
  5. Tanzania police arrest 32 witch-doctors over ritual albino killings (Guardian-UK Friday 6 March 2015)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Wikimedia Commons ina media kuhusu: