Mauaji ya maalbino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mauaji ya maalbino ni mauaji juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi maarufu kama maalbino au zeruzeru.

Mambo yanayofanywa juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi ni haya yafuatayo.

Imani za kishirikina ambazo husababisha watu wasio na hatia kuuliwa kwa lengo la kutaka kutajirika kupitia watu hawa.

Lingine ni uwepo wa elimu finyu juu yao kuhusu umuhimu wa binadamu kuishi na si kuuliwa kama kwamba si watu ambao waliumbwa na Mungu. Hivyo basi hali hii hupelekea watu wenye ulemavu kama huu kukosa haki zao za msingi kama vile ile ya kuishi.

Njia za kuzuia mauaji ya maalbino ni yafuatayo: uwepo wa elimu juu ya umuhimu wa maalbino na si kuuliwa. Hivyo jamii haina budi kuwapa wote elimu, waelimishwe pia kuweka sheria na adhabu kali dhidi ya watu wanaowaonea wenye ulemavu.