Urujuani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rangi ya urujuani
Rangi ya zambarau kwa ulinganifu

Urujuani ni rangi kati ya buluu na nyekundu. Iko karibu na zambarau lakini inaelekea zaidi upande wa buluu.

Ni rangi ya saba ya upinde wa mvua. Kifizikia ni rangi ambayo mawimbi yake ni fupi zaidi kati ya rangi zinazoonekana kwa binadamu; kama ni fupi zaidi inaendelea kuwa urujuanimno ambayo haionekani kwa macho yetu.