Nasuri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nasuri (kwa Kiingereza fistula) kwa maana ya matibabu ni njia ndani ya mwili (zenye umbo kama bomba au mpira mdogo) zisizopatikana kwa kawaida na kuwa njia kati ya sehemu za mwili zisizounganika kwa kawaida. Zinaweza kusababisha maumivu pamoja na kuvuja kwa damu, usaha, mkojo, kinyesi ama ndani ya mwili au kutoka nje.

Nasuri hupatikana

  • kama nasuri ya ndani kati ya sehemu za mwili ambazo kwa kawaida hazina njia kati yao, kwa mfano kati ya uke na rektamu au utumbo
  • kama nasuri ya nje kati ya jipe la usaha mwilini na ngozi ya nje.

Nasuri zinaweza kutokea kote mwilini lakini zaidi kwenye utumbo na kwenye rektamu.

Michonyoto unaweza kuleta jipe la usaha mwilini na nasuri ni njia ya kutoka kwa usaha.

Sababu za kutokea kwa nasuri[hariri | hariri chanzo]

Kuna sababu mbalimbali za kutokea kwa nasuri.

Kama msamba wa mama unakatika vibaya wakati wa kumzaa mtoto njia kati ya uke na rektamu au utumbo unafunikwa na nasuri ya kudumu inaweza kubaki. Kwa njia ya nasuri hii damu, mkojo au hata sehemu za kinyesi zinaweza kuingia kwenye uke.

Michonyoto -hasa michonyoto ya kudumu- kwenye utumbo inasababisha pia kutokea kwa nasuri kwa mfano kati ya utumbo na kibofu nyongo.

Sababu nyingine ni uvimbe wa kansa, au uharibifu unaotokea wakati wa upasuaji.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nasuri kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.