Makka
Makka (rasmi: Makkah al-Mukarramah; Kar.: مكة المكرمة) ni mji wa Ufalme wa Uarabuni wa Saudia. Ina wakazi 1,294,167 (mwaka 2004). Mji uko kwenye bonde la Ibrahimu mnamo km 80 kutoka pwani la Bahari ya Shamu na bandari ya Jeddah. Mazingira ya mji ni jangwa mahali penyewe kuna visima vilivyowezesha kuwepo kwa mji tangu kale.
Makka kama mahali patakatifu wa Uislamu
[hariri | hariri chanzo]Makka ni mji mtakatifu wa Uislamu. Kila mwaka mamilioni wa Waislamu wanahiji kwenda Makka. Wakati huu wa hajj wanajaribu kufuata nyayo za mtume Muhammad. Makka ni mji uliofungwa kwa wasio Waislamu.
Kwa Waislamu Makka ni mji wa kuzaliwa kwake mtume Muhammad pia mahali alipokaa alipoanza kupokea aya za Kurani. Mjini kuna pia jengo la Kaaba linaloaminiwa ni msikiti iliyojengwa na Adamu na kutengenezwa upya na Ibrahimu (Abrahamu).
Hajj ya kwenda Makka ni moja kati ya nguzo tano za Uislamu.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Mahali pa Makka
-
Makka mwaka 1850
-
Kambi ya Wahiji
-
Ramani ya Kituruki ya Makka ya 1787
-
Msikiti Mkuu wa Makka pamoja na Kaaba baada ya swala ya Ijumaa
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Kibla ya Makka (kiing.) Ilihifadhiwa 25 Agosti 2006 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Makka kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |