DNA

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mfano wa mfumo wa DNA

DNA ni kifupi cha DeoxyriboNucleic Acid ambayo ni jina la molekuli kubwa ndani ya seli za viumbehai pamoja na wanyama, mimea, bakteria na virusi. Inabeba ndani yake habari zote za urithi wa kiumbehai yaani habari za tabia zote zinazopokelewa na wazazi. Kwenye DNA ziko geni zinazotunza habari maalumu juu ya urithi wa kiumbe.

Molekuli ya DNA ina umbo kama ngazi mbili za kupanda zilizounganishwa pamoja na kupindwa kama sukurubu. Kila ngazi ni nukleotidi ambayo ni muungo wa sukari fulani pamoja na moja kati ya besi ogania nne. Ufutano wa besi hizi unaamua namna gani kujenga protini wakati wa kujenga seli mpya.

DNA ina uwezo wa kujinakili. Wakati wa kuzaa inajipasua katikati ya pande mbili za "ngazi" yake. Hivyo nusu "ngazi" ya upande wa mzazi mmoja inaungana na nusu "ngazi" ya mzazi mwingine. Tabia kama ukubwa, rangi ya ngozi au nywele ziko kila moja mahali pake; zikiunganishwa kemia inaamua ni upande gani yenye athira zaidi.


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]