Kamusi sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia
Mandhari
(Elekezwa kutoka Kamusi Sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia)
"Kamusi sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia" (kifupi: KSBFK) ni kamusi iliyoandaliwa na wataalamu wa TUKI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1990 chini ya uhariri mkuu wa David P.B. Massamba.
Kamusi hii inakusanya maneno ya kisayansi kwa utaratibu ufuatao:
- neno la Kiingereza
- maelezo yake kwa Kiswahili
Mwishowe kuna jedwali la elementi ya kikemia.
Kamusi hii ilichapishwa upya mwaka 2004 na mwaka 2012.
Si rahisi kuipata katika maduka ya vitabu lakini inapatikana katika duka la TATAKI jinsi TUKI inaitwa siku hizi. Mada inafanana kiasi na ile ya kamusi Awali wa Sayansi na Teknolojia (KAST) lakini wala istilahi wala tahajia hazilingani sawa.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Kamusi sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia (KSBFK). Taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili, Dar es Salaam, Tanzania. ISBN 9976 911 092