Besi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kwa dutu la kikemia tazama hapa: Besi (kemia)

Upeo kwa besi kwa maandishi ya noti

Besi ni jina kwa sauti ya chini katika muziki. Kifizikia besi huelezwa kuwa sauti yenye marudio kati hertz 0 hadi 150.

Marudio ya chini hupokelewa na binadamu siyo kupitia masikio pekee bali kwa mwili wote. Kwa hiyo hata watu viziwi wanasikia sauti za besi wanaweza kucheza kwa muziki yenye besi.

Katika muziki kuna ala za pekee kwa ajili ya besi kama vile gitaa ya besi au ngoma kubwa. Ala kadhaa kama piano au kinanda huwa na sauti za juu hadi besi.