Nenda kwa yaliyomo

Besi (kemia)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa sauti ya chini tazama hapa: Besi

Besi ni dutu ya kikemia yenye uwezo wa kupokea ioni ya hidrojeni (H+) kutoka kwa dutu nyingine inayoitwa asidi. Tokeo la mmenyuko huo ni chumvi pamoja na maji.

Katika myeyusho wa maji besi hufanya ioni za hidroksidi (OH−) zinazoongeza thamani pH ya myeyusho. Ioni za hidroksidi ni kampaundi zinazotoa protoni kutoka asidi kwa kuunda molekuli ya maji. Kwa hiyo besi ni kinyume cha asidi na besi inaweza kubatilisha asidi - na pia kinyume.