Nenda kwa yaliyomo

Thamani pH

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mizani inayoonyeha Thamani pH

Thamani pH ni skeli inayoonyesha kiwango cha asidi katika dutu fulani. "pH" ni kifupi cha Kilatini "pondus Hydrogenii" (Kiingereza "potential of Hydrogen").

Skeli hii ina thamani kuanzia 0 hadi 14. Namba ndogo inaonyesha tabia ya kiasidi, namba kubwa tabia ya kibesi. Dutu isiyo na tabia ya besi wala asidi huwa na thamani pH ya 7. Asidi huwa na kiwango chini ya 7, besi njuu ya 7.


Mifano ya thamani pH

[hariri | hariri chanzo]
pH
Asidi ya betri1.0
Asidi ya tumboni2.0
Majimaji ya Limau2.4
Cola2.5
Siki2.9
Maji ya chungwa au tofaa3.5
Bia4.5
Kahawa5.0
Chai5.5
Mvua asidia< 5.6 (hadi 2.5)
Maziwa6.5
Maji tupu7.0
Damu7.34 - 7.45
Maji ya bahari8.0
Sabuni9.0 - 10.0