Nenda kwa yaliyomo

Metafizikia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Konfutsu.

Metafizikia ni tawi la falsafa linalochunguza asili msingi ya ulimwengu.

Kifupi, metafizika inajaribu kujibu hasa maswali mawili: 1. nini kipo? 2. kama kipo, kinakaaje?

Hivyo, mada za uchunguzi za wanametafizikia ni kama vile: kuwepo, violwa na sifa zao, nafasi na wakati, usababishi na uwezekano. Tawi kuu la metafizika ni ontologia, uchunguzi wa kundi za kuwepo na namna zinavyohusiana.

Kuna dhana mbili pana kuhusu ni “dunia” gani haswa inayochunguzwa na metafizika. Ile maarufu, maoni ya zama inayodhani kwamba violwa zinazotibwa na metafizika ziko kuwepo huru kutokana na mtazamaji yeyote. Yenyewe ina umaarufu kidogo, na dhana za majuzi inadhani kwamba violwa ambazo zinachunguzwa na metafizikia zina kuwepo kwa akili ya mtazamaji tu, hivyo raia anakua mfumo wa kujichunguza na uchambuaji wa dhana. Wanafalsafa kadhaa, haswa Emmanuel Kant na Arthur Schopenhauer, wanaongea kuhusu “dunia” zote mbili na jinsi zinavyotangamana.

Wanafalsafa kadhaa na wanasayansi, kama vile wanamantiki chaya, wametupilia mbali somo zima la metafizikia na kusema halina maana, lakini wengine wanakiri kuwa somo hili ni halali.

Etimologia

[hariri | hariri chanzo]

Neno “metafizikia” limetokana na maneno ya Kigiriki: μετα meta (“ng'ambo ya”, “juu ya” ama “baada ya”) na φυσίκή fysike (fizikia). Ilitumika mara za kwanza kama kichwa cha maandishi kadhaa ya Aristoteli kwa umbo la μετὰ τὰ φυσικά meta ta fysika baada ya fizikia.

Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Metafizikia kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.