Hija

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wayahudi wakisali kwenye Ukuta wa Maombolezo, Yerusalemu.
Mlango mkuu wa Kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu, Yerusalemu.
Hija ya Waislamu kwenye Masjid al-Haram, Maka, mwaka 2008.

Hija (kutoka Kiarabu حج, hajj, kitenzi kuhiji) ni ziara ya kidini yaani ni safari inayofanyika kwa sababu ya dini, ikilenga patakatifu fulani.

Kwa maana ya kiroho, maisha yote ni safari ya kumuelekea Mungu au uzima wa milele n.k.

Sababu ya kwenda mahali maalumu ni tumaini la kuwa karibu zaidi na imani mahali ambako mambo muhimu ya historia ya dini husika yalitokea; mara nyingi pia imani ya kwamba sala itakuwa na nguvu au mafanikio zaidi pale.

Desturi ya kuhiji iko katika dini mbalimbali.

Masharti ya Hijja katika Uislamu][hariri | hariri chanzo]

  • 1. Uislamu. Hijja haimlazimu kafiri, na akihiji haisihi hijja yake.
  • 2. Kuwa na akili. Hija haimlazimu mwendawazimu, kwa neno lake ﷺ: (Watu watatu hawaandikiwi dhambi: aliyelala mpaka azunduke, mtoto mapaka abaleghe na mwendawazimu mpaka apate akili) [Imepokewa na Abu Daud.].
  • 3. Kubaleghe. Hijja haimlazimu mtoto mdogo, na lau mtoto mdogo atahirimia hija basi hija yake itasihi. Lakini haimtoshelezi na Hijja ya Uislamu, na itahesabiwa ni Sunna. Hii ni kwa hadithi ya Ibnu ‹Abbas t kwamba mwanamke mmoja alimuinulia Mtume wa Mwenyezi Mungu mtoto, na akasema: «Je, huyu ana Hija? Mtume akasema: (Ndio, nawe una thawabu) [Imepokewa na Muslim]
  • 4. Uhuru. Hijja haimlazimu mtumwa, kwa kuwa Mtume amesema: (Mtumwa yoyote aliyehiji kisha akaachwa huru, basi itamlazimu Hija nyingine) [Imepokewa na Muslim.].
  • 5. Uwezo. Nao ni kuwa na matumizi [Zaad: Vitu anvyovihitajia kama chakula, kinywaji na mavazi.] na kipando [ Raahilah: Kipando anachokipanda kama gari au ndege au meli..], kwa neno lake Mwenyezi Mungu: {Ni haki ya Mwenyezi Mungu juu ya watu waikusudie Alkaba kwa ibada ya Hija kwa anayeweza kwenda huko} [3: 97]
  • 6. Kuweko na maharimu. [Mahram: ni yule ambaye ni haramu kwa mwanamke kuolewa naye kama baba, ndugu na mjomba.] ya Mwanamke. Kwa hadithi ya Ibnu ‹Abbas t kuwa alisema: Nilimsikia Mtume akisema: (Hasafiri mwanamke isipokuwa pamoja na mtu maharimu yake). Akainuka mtu mmoja akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mke wangu ametoka kwenda kuhiji, na mimi nimejisajili katika vita kadha na kadha. Akasema Mtume: (Toka uende kuhiji na mkeo) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.][1]

Jina[hariri | hariri chanzo]

Kiasili neno "hija" katika Kiswahili lilimaanisha tu safari ya Waislamu kwenda Makka kwa sababu katika utamaduni wa Waswahili hili lilikuwa safari ya kidini pekee yenye jina maalumu.

Lakini Wakristo wamepokea neno hili pia kwa safari zao za kiroho na siku hizi linatumiwa kwa kutaja safari za aina hii kwa jumla kati ya dini zote.

Wingi wa watu kwenye hija[hariri | hariri chanzo]

Hija mashuhuri dunani inawezekana ni hajj ya Kiislamu kwenda Makka.

Lakini hija mbalimbali za Uhindu zina namba kubwa zaidi ya mahudhurio. Kumbh Mela huko Allahabad kwenye mto Ganges ilikuwa na wahijji milioni 60 mwaka 2001.[2]

Pia ndani ya Uislamu kuna watu zaidi wanaohudhuria umra (ziara za Makka nje ya hajj) au ziara ya Karbala.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.al-feqh.com/sw/hukumu-za-hija-na-umra
  2. tazama kifungo "Notes on Kumbh Mela numbers". Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-02-05. Iliwekwa mnamo 2015-05-28.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.