Nenda kwa yaliyomo

Hekalu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nakala ya Parthenon ya Athens iliyojengwa huko Nashville (Tennessee) nchini Marekani
Hekalu la Kibudha huko Angkor Wat nchiniCambodia

Hekalu ni jengo la dini mbalimbali, lakini si zote.

Nyingine zinaita maabadi yao kwa majina tofauti, kutokana na mtazamo wa msingi.

Kwa mfano katika Uislamu jengo la ibada linaitwa msikiti.

Hekalu katika Uyahudi

[hariri | hariri chanzo]
Mfano wa hekalu la pili la Yerusalemu.

Katika Biblia lina umuhimu wa pekee hekalu la Yerusalemu, lililojengwa kwanza na mfalme Sulemani, mwana wa Daudi likabomolewa na mfalme Nebukadreza II wa Babuloni mwaka 586 K.K..

Hekalu hilo likajengwa upya (536 K.K. - 515 K.K.) baada ya uhamisho wa Babeli, likatakaswa na kuwekwa wakfu upya na Yuda Mmakabayo (164 K.K.), likapanuliwa na kupambwa na mfalme Herode Mkuu na Wayahudi wote (19-64 BK) hadi miaka michache kabla halijabomolewa tena na Warumi mwaka 70.

Tangu hapo halijajengwa tena, hivi kwamba sadaka zinazodaiwa na Torati hadi sasa haziwezi kutolewa kwa muda wa miaka 2000 hivi.

Tangu wakati wa uhamisho hadi leo Wayahudi wanaendelea kukusanyika katika majengo yanayoitwa masinagogi (yaani "mkutano").

Hekalu katika Ukristo

[hariri | hariri chanzo]

Yesu Kristo alikuwa ametabiri maangamizi hayo miaka 40 hivi ya nyuma, akisema saa imefika ya kumtolea Mungu Baba ibada mpya katika Roho na ukweli.

Alipotakasa hekalu hilo, alitangaza kuwa mwili wake mfufuka utakuwa ndio hekalu la kweli ambamo watu wote wamuendee Mungu na kumtolea ibada hiyo.

Ndiyo sababu kwa kawaida maabadi ya Wakristo huitwa kanisa (yaani "mkusanyiko"), si hekalu.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.