Sinagogi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ukumbi wa sinagogi kisiwani Rhodos
Sinagogi ya Kale mjini Praha

Sinagogi ni nyumba ya dini na ya jamii ya Wayahudi inayotumika hasa kusali.

Etimolojia[hariri | hariri chanzo]

Neno linatokana na Kigiriki συναγωγή sinagoge likimaanisha "mkutano"; ni tafsiri ya Kiebrania בית כנסת beit knesset yaani "nyumba ya mkutano".

Wayahudi hutumia pia neno la Kiyiddish "shul" (=shule) kutajia sinagogi.

Muundo[hariri | hariri chanzo]

Chumba kikuu ni ukumbi wa sala lakini mara nyingi kipo pamoja na vyumba vya pembeni kama vile madarasa, ofisi na vingine.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Katika Israeli ya Kale (kabla ya maangamizi ya Yerusalemu mwaka 587 KK) inaonekana hakukuwa na sinagogi: walau halitajwi kabisa katika Agano la Kale.

Hakuna uhakika kamili lakini inaonekana ya kwamba masinagogi yalianzishwa baada ya hekalu ya Yerusalemu kubomolewa pamoja na kuanza uhamisho wa Wayahudi kwenda nchi mbalimbali.

Tangu kuharibiwa kwa Hekalu la Pili mwaka 70 Wayahudi wana masinagogi tu kufanyia ibada.

Yaliyomo[hariri | hariri chanzo]

Ukumbi wa sala huwa na sehemu zifuatazo:

  • sanduku la Torati ni kabati au sanduku ambako hati za kuviringisha zenye mwandiko wa Biblia ya Kiebrania hutunzwa;
  • taa inayoendelea kuwaka muda wote;
  • meza ya msomaji ambako hati za torati hufunguliwa na kusomwa;
  • mimbari ya mafundisho;
  • kinara cha menorah chenye mishumaa 7 au 9.
Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sinagogi kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.