Praha
Praha (pia: Praga, Prague (tamka: Prag) -Kicheki: Praha) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Ucheki mwenye wakazi milioni 1.2. Kutokana na uzuri wa majengo yake za kihistoria imeitwa "mji wa dhahabu" au "mji wa minara 100".
Jiografia[hariri | hariri chanzo]
Mji uko kando la mto Vltava katika Ucheki ya magharibi. Kitovu cha mji kipo katika pindo la mto kati ya vilima viwili. Mji umeenea zaidi hadi nyanda za juu za jirani. Ndani ya eneo la mji kuna visiwa kadhaa mtoni. Milima ya juu karibi na mji inafikia kimo cha 381 na 385 m.
Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]
- Tovuti rasmi Archived 20 Machi 2004 at the Wayback Machine.
- Majengo ya Kihistoria Archived 15 Machi 2007 at the Wayback Machine.
- Hoteli za Praha Archived 16 Machi 2007 at the Wayback Machine.
Picha za Praha[hariri | hariri chanzo]
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Praha kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |