Sanduku

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfano wa sanduku dogo lilotengenezwa kwa chuma.

Sanduku ni aina ya chombo kilichoundwa kwa ajili ya matumizi ya kudumu ama ya muda kama hifadhi na mara nyingi hutumika kwa ajili ya kusafirisha vitu mbalimbali. Pia hujulikana kwa jina lingine kama kasha.

Sanduku huenda likafanywa na mbao au chuma, karatasi ngumu. Kwa ukubwa yanaweza kutofautiana kutoka dogo sana (kama kasha la kiberiti) hadi kubwa sana (kama masanduku yanayobebwa na meli). Masanduku yapo ya maumbo tofauti, kwa mfano yapo yenye umbo la pembe tatu, pembe nne, duara na maumbo mengine mengi.