Nenda kwa yaliyomo

Pembenne

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Pembe nne)

Pembenne ni umbo bapa lenye pande nne. Kwa lugha nyingine ni pembenyingi yenye pembe nne.

Pembenne hutokea kama nukta nne kwenye ubapa zinaunganishwa kwa mistari inayofunga eneo ndani yake.

Maumbo ya pekee ya pembenne ni mstatili, mraba, trapeza na msambamba.

Kila pembenne huwa na ulalo mbili.

Jumla ya pembe zote ndani ya pembenne ni nyuzi 360°.

Maumbo mbalimbali za pembenne

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: