Kabati
Mandhari
Kabati (kutoka Kiingereza "cup-board") ni samani ambayo watu huitumia kuhifadhia vitu, kwa mfano: vyombo, nguo, mabeseni na midoli.
Kwa kawaida kabati linawekwa ofisini, sebuleni, jikoni, bafuni n.k.
Kwa kawaida ina rafu moja au zaidi ya kuweka vitu, pia inaweza kuwa na mlango wa mbao, chuma au kioo.
Kabati inaweza kutumika pia kama kitu cha mapambo katika nyumba.
Faida
[hariri | hariri chanzo]- 1) Husaidia kuwekea na kutunza nguo
- 2) Husaidia kuwekea vyombo mbalimbali
- 3) Husaidia kuwekea televisheni au runinga
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kabati ilianza kutumika miaka ya 1600 huko Emilia-Romagna nchini Italia na mara nyingi ilitumika ukumbini.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kabati kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |