Herode Mkuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Herode Mkuu.
Herode akiteka Yerusalemu.
Hekalu la Yerusalemu.
Mamajusi mbele ya Herode.
Mchoro wa Duccio di Buoninsegna kuhusu Mauaji ya watoto wachanga yaliyoagizwa na Herode.

Herode Mkuu (73 KK hivi - 4 KK) ni jina la heshima linalotumika kumtajia mtu maarufu zaidi wa ukoo wa kifalme wa Yudea katika karne ya 1 KK.

Akiwa kwa asili mtu wa kabila la Waedomu, alitawala Yudea yote chini ya himaya ya Dola la Roma.

Mkatili hasa, aliua hata mke wake mmojawapo na baadhi ya watoto.

Ingawa alifuata dini ya Uyahudi na kuanza kazi kubwa ya kupanua na kupamba hekalu la Yerusalemu, alizingatia zaidi ustaarabu wa Kigiriki na kuendeleza miji kipagani.

Ni maarufu zaidi kutokana na taarifa za Injili ya Mathayo kuhusu jinsi alivyopokea kutoka kwa Mamajusi habari ya kuzaliwa kwa Mfalme wa Wayahudi, Yesu. Kwa hofu yake aliposhindwa kumtambua mtoto huyo, aliagiza wauawe watoto wote wa kiume chini ya umri wa miaka 2.

Familia[hariri | hariri chanzo]

Familia ya Herode Mkuu
Mke Watoto
Doride
 • Antipatro, alifariki 4 KK
Mariamne I
 • Aleksanda, alifariki 7 KK
 • Aristobulo, alifariki 7 KK
 • Salampsio
 • Cypro
Mariamne II
 • Herode II, alifariki 6
 • Herode Filipo
Malthace
 • Arkelao, mfalme mdogo wa Yudea
 • Herode Antipa, mfalme mdogo wa Galilaya
 • Olimpia
Kleopatra wa Yerusalemu
 • Herode Filipo II, mfalme mdogo wa Perea
 • Herode
Pallade
 • Fasaele
Fedra
 • Rossane
Elpide
 • Salome