Kolombia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
República de Colombia
Jamhuri ya Kolombia
Bendera ya Kolombia Nembo ya Kolombia
Bendera Nembo
Wito la taifa: Kihispania: Libertad y Orden
"Uhuru na Utaratibu"
Wimbo wa taifa: Oh, Gloria Inmarcesible!
Ewe heshima isiyouzika
Lokeshen ya Kolombia
Mji mkuu Bogota
4°39′ N 74°3′ W
Mji mkubwa nchini Bogota
Lugha rasmi Kihispania
Serikali Jamhuri
Juan Manuel Santos Calderón
Uhuru
Ilitangazwa
Ilitambuliwa

20 Julai 1810
7 Agosti 1819
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
1,141,748 km² (ya 26)
8.8%
Idadi ya watu
 - Julai 2005 kadirio
 - 2005 sensa
 - Msongamano wa watu
 
45,600,000 (ya 28)
41,242,948
40/km² (161st)
Fedha Peso ya Kolombia (COP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-5)
(UTC)
Intaneti TLD .co
Kodi ya simu +57

-Ramani ya Kolombia

Kolombia (Kihisp.: República de Colombia) ni nchi kwenye pembe la kaskazini ya Amerika ya Kusini. Imepakana na Venezuela, Brazil, Ekuador, Peru na Panama. Ina pwani mbili za Pasifiki na Atlantiki.

Jina la nchi limeteuliwa kwa heshima ya Kristoforo Kolumbus (Kihisp.: Cristóbal Colón; Kiit.:Cristoforo Colombo) aliyegundua njia kati ya Hispania na Amerika mwaka 1492.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Upande wa magharibi wa nchi kuna milima ya Andes inayopatikana kwa safu tatu za milima zinazoitwa "Kordileri". Kati ya milima hii kuna chanzo cha mito miwili mikubwa ya nchi ndiyo Rio Cauca na Rio Magdalena inayoishia katika Bahari ya Karibi (Atlantiki). Mto mkubwa upande wa magharibi ni Atrato inayoishia Pasifiki.

Milima ya juu ni Pico Cristobal Colon na Pico Simon Bolivar yenye kimo cha 5,775 m kila moja.

Sehemu ya mashariki ya Kolombia ni tambarare yenye misitu minene. Mito yake kama vile Putumayo, Yapura, Meta na Guaviare inaishia ama katika mto Orinoko au kwenye Amazonas.

Visiwa[hariri | hariri chanzo]

Koloumbia ina visiwa katika bahari zote mbili. Upande wa Karibi / Atlantiki kuna funguvisiwa ya San Andres na Providencia iliyoko baharini 770 km kutoka bara. Karibu na pwani la Karibi ni kisiwa cha Fuerte na funguvisiwa za San Bernardo na del Rosario.

Visiwa vya Malpelo, Gorgona na Gorgonilla viko katika Pasifiki.

Miji[hariri | hariri chanzo]

Miji mikubwa ni mji mkuu Santa Fé de Bogotá, Medellín, Cali, Cartagena de Indias, Barranquilla, Ibagué, Manizales, Pasto, Cúcuta na Bucaramanga.

Picha:CASADENARIÑO.jpg
Ikulu ya Rais wa Kolombia

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Kuna wakazi milioni 41 wengi wako mjini hasa katika mabonde ya Rio Cauca na Rio Magdalena na kwenye mwambao wa bahari ya Karibi.

Asili ya wakazi ni ya mchanganyiko wa vikundi vitatu:

  • wenyeji asilia ("Wahindi wekundu" au Waindio)
  • Wazungu kutoka Hispania
  • watoto wa Waafrika waliofika kama watumwa

Sehemu kubwa ni chotara wa Waindio na Wazungu (takriban 60%), halafu Wazungu wenye asili ya Kihispania (20%), halafu chotara wa Waafrika na Wazungu (14%) na chotara wa Waindio na Waafrika (3%). Wakolombia wenye asili tupu ya Kiafrika ni %, enye asili tupu ya Waindio ni 1%.

Kuna uhamiaji mkubwa kutoka mashambani kuelekea mjini. Mwaka 1994 asilimia 74 za wakazi wote wa nchi walikaa mjini. Mikoa ya mashariki ina zaidi ya nusu ya eneo la taifa lakini asilimia 3 za wakazi pekee.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mataifa asilia ya Waindio walikuwa Wachibcha, Waarawak na Wakaribi.

Hasa Wachibcha waliokalia nyanda za juu walikuwa na utamaduni wa kimaandishi; walitumia kalenda, mahesabu na alfabeti yao. Lakini hawakujenga miji na madola yao yalikuwa madogo.

Wahispania walijenga miji ya kwanza Santa Marta (1527) na Cartagena de Indias (1533) kwenye pwani. Tangu 1537 waliingia katika nyanda za juu na kuvamia maeneo ya Wachibcha. Hapo walijenga miji ya Santa Fé de Bogotá na Tunja (zote mbili 1539).

Baadaye Kolombia ilikuwa kitovu cha ufalme mdogo Granada Mpya.

Tangu mwaka 1813 kiongozi Simon Bolivar alipigania uhuru wa koloni za Amerika ya Kusini. 1819 Jamhuri ya "Gran Colombia" (Kolombia kubwa) iliundwa iliyodumu hadi 1831. Baadaye iliachana kuwa nchi za pekee za Kolombia (pamoja na Panama), Venezuela na Ecuador.

Kolumbia iliona vita za wenyewe kwa wenyewe; wakati wa "vita ya siku 1000" Marekani ilitumia udhaifu wa nchi na kusaidia ghasia katika Panama iliyosababisha uasi wa Panama kuwa nchi ya pekee mwaka 1903.

Sehemu ya pili ya karne ya 20 iliona vita mpya ya wenyewe kwa wenyewe iliyoendela hadi mwaka 2006. Shemu za nchi ziko chini ya wanamigambo wanaodumisha utawala wao kwa biashara ya madawa ya kulevya hasa Kokain.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Nchi na maeneo ya Amerika Kusini

Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyana ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
South America.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kolombia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA