Henry Ford

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Henry Ford

Amekufa 7 Aprili 1947
Nchi Marekani
Kazi yake mfanyabiashara

Henry Martin Ford (30 Julai 1863 - 7 Aprili 1947) alikuwa mhandisi na mfanyabiashara nchini Marekani. Alianza kutengeneza magari mwaka 1896 akaunda kampuni ya Ford Motor Company mjini Detroit.

Alianzisha mbinu Ya kazi ya kiwandani ulioigwa baadaye kote duniani. Alipasua kila kazi katika ufuatano wa hatua ndogondogo. Kila hatu ilipewa kwa mfanyakazi mmoja. Kwa mfano mmoja alikuwa na kazi tu kuweka tairi kwa gari na mwingine alifunga skrubu za tairi hii. Kwa kupasua mchakato wa kazi aliona ya kwamba kila kila mfanyakazi aliweza kutekeleza shughuli yake haraka zaidi tena kwa makosa machache. Kwa njia hii alifaulu kutengeneza magari haraka zaidi tena kwa bei nafuu kuliko makampuni mengine.

Gari la kwanza lililotengenezwa kwa idadi kubwa ilikuwa modeli ya Ford T akajenga milioni 15 Ford T. Pamoja na kupasua kazi aliamua kuwapa wafanyakazi wake mishahara mikubwa kuliko kawaida kwa sababu aliwataka kama wateja kwa gari lake.