Njia ya bomba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Njia za bomba zinazotoka kwenye bandari ya Gdansk na kusafirisha mafuta na gesi zinazofika kwa meli.

Njia ya bomba (kwa Kiingereza: pipeline) ni mfumo wa kusafirisha vimiminika kama mafuta ya petroli au gesi hadi umbali mkubwa kwa kutumia mabomba yaliyounganishwa. Kuna pia njia za bomba zinazosafirisha madini au makaa yaliyochanganywa na maji kwa kusudi hili. Matumizi mengine ni kwa ajili ya maji safi, maji taka, maziwa au bia.

Teknolojia[hariri | hariri chanzo]

Njia hizo hutumia mabomba ya metali au ya plastiki. Mabomba hayo mara nyingi huwekwa katika mifereji na kufunikwa udongo. Kama ardhi ni ngumu au laini mno mabomba huwekwa juu ya ardhi. Kuna pia njia za bomba baharini.

Vimiminika husafirishwa kwa kutumia pampu; njia ndefu huwa na vituo vya pampu kila baada ya kilomita 100 hivi; umbali hutegemea kama njia ya bomba inapanda milima, inashuka chini au kuendelea tambarare.

Gesi hazihitaji pampu bali husukumwa kwa shinikizo. Mabomba ni ya feleji yaliyotengenezwa kwa umakini mkubwa ili kuepukana kabia mapengo yoyote. Njia ya bomba kwa gesi asilia huhitaji vituo vya kurudisha shinikizo kwenye njia yake.

Njia ya bomba la mafuta iliyopangwa kutoka Uganda kwenda Tanga - Tanzania.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Njia za bomba ni ghali, hata hivyo ni nafuu kusafirisha mafuta au gesi kwa njia hiyo ikiliganishwa na usafiri kwa barabara au reli.

Huko Marekani ilikadiriwa mwaka 2014 kuwa kiasi sanifu cha mafuta ("barrel") kinagharamia dolar 5 kwa njia ya bomba lakini dolar 10-15 kwa njia ya reli.

Kuna njia za bomba zinazoendelea kwa kilomita elfu kadhaa, kwa mfano kutoka Siberia - Urusi hadi Ulaya ya Magharibi, au kutoka Alaska hadi Marekani Bara.

Njia hizo zina uwezo wa kusafirisha viwango vikubwa; mfano ni njia ya bomba la gesi la Omani lenye kipenyo cha sentimita 81 inayopeleka kila siku mita za ujazo milioni 22.8 kwa umbali wa kilomita 300. Njia ya bomba la mafuta lenye kipenyo cha sentimita 71 kutoka bandari ya Wilhelmshaven (Ujerumani) inasafirisha tani milioni 15.5 kwa mwaka.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons