Nenda kwa yaliyomo

Kanada

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mkanada)
Canada
Bendera ya Canada Nembo ya Canada
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Kilatini: A Mari Usque Ad Mare
("Bahari hadi bahari")
Wimbo wa taifa: "O Canada"
Wimbo wa kifalme: "God Save the King"
Lokeshen ya Canada
Mji mkuu Ottawa
45°24′ N 75°40′ W
Mji mkubwa nchini Toronto
Lugha rasmi Kiingereza, Kifaransa
Serikali Ufalme wa kikatiba, shirikisho,
demokrasia
Charles III
Mary Simon
Justin Trudeau
Uhuru
Sheria ya 1867
Mkataba wa Westminster
Sheria kuhusu Kanada

1 Julai 1867
11 Desemba 1931
17 Aprili 1982
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
9,984,670 km² (ya 2)
11.76
Idadi ya watu
 - 2023 kadirio
 - 2021 sensa
 - Msongamano wa watu
 
39,858,480 (ya 37)
36,991,981
4.2/km² (ya 236)
Fedha Dollar ya Kanada ($) (
CAD
)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-3.5 to -8)
(UTC-2.5 to -7)
Intaneti TLD .ca
Kodi ya simu +1



Kanada ni nchi kubwa ya Amerika ya Kaskazini na ya pili duniani kwa eneo baada ya Urusi, lakini idadi ya wakazi ni 39,858,480 tu (2023).

Kwenye nchi kavu imepakana na Marekani bara na jimbo la Alaska. Mbele ya pwani zake kuna kisiwa kikubwa cha Greenland ambacho ni chini ya Denmark halafu visiwa vidogo vya St. Pierre na Miquelon (Ufaransa).

Mji mkuu ni Ottawa.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Kanada ni nchi kubwa ya pili duniani lakini maeneo mengi ni baridi mno, hawana watu.

Pwani ya Kanada ni ndefu kushinda nchi zote za dunia, ikipakana na Atlantiki, Pasifiki na Bahari ya Aktika.

Jumla ya wakazi milioni 40 huishi katika majimbo 10 na maeneo matatu ya kitaifa.

Katika eno la km² 9,984,670, km² 9,093,507 ni nchi kavu na km² 891,163 ni maji.

Umbali kutoka Rasi Columbia kwenye kisiwa cha Ellesmere katika kaskazini hadi kisiwa cha Middle Island katika ziwa la Erie jimboni Ontaria ni km 4,634.

Umbali kutoka Rasi Spear katika Newfoundland upande wa mashariki hadi mpaka na Alaska upande wa magharibi ni km 5,514.

Mto mkubwa kabisa nchini Kanada ni Mto Mackenzie upande wa magharibi wa nchi.

Baadhi ya milima mirefu zaidi ni:

Mingine chini ya m 3,000 ni:

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Maeneo ya Kanada yalianza kukaliwa walau 14,000 iliyopita na wahamiaji kutoka Asia ya Kaskazini.

Wazungu wa kwanza waliofika walikuwa Wanorwei kutoka Greenland mnamo mwaka 1000 BK. Lakini hawakukaa muda mrefu sana.

Katika karne zilizofuata kuna uwezekano wa kwamba wavuvi kutoka Ulaya ya Kaskazini walifika pwani za Kanada mara kwa mara na kujenga makazi ya muda wakikausha samaki kwa ajili ya safari za kurudi, lakini hakuna uhakika.

Tarehe 26 Aprili 1497 alifika Mwitalia Giovanni Caboto (kwa Kiingereza huitwa "John Cabot") kwenye visiwa vya Newfoundland akiwa katika utumishi wa malkia wa Uingereza akavitangaza kuwa eneo la Waingereza.

Mnamo 1534/1535 Wafaransa walifika katika eneo la Mto Saint Lawrence na kujenga makao yao.

Wapelelezi na walowezi kutoka Ulaya walileta pamoja nao magonjwa ambayo hayakujulikana kwa wenyeji asilia na yalisababisha vifo vingi kati yao. Kupunguzwa kwa wakazi asilia kulisaidia upanuzi wa walowezi Wazungu kota Amerika.

Makoloni ya Waingereza na Wafaransa yalikua polepole. Katika Vita ya Miaka Saba Ufaransa ulipotea maeneo yake yote yaliyotwaliwa na Uingereza. Visiwa vya St. Pierre na Miquelon pekee vilibaki upande wa Ufaransa. Uingereza uliamua kukubali utamaduni wa pekee wa wakazi Wafaransa katika jimbo la Quebec. Hadi leo wanaendelea kutumia Kifaransa na kufuata hasa Ukatoliki, tofauti na Wakanada wenye asili ya Kiingereza walio zaidi Waprotestanti.

Wakati wa vita ya kupigania uhuru wa Marekani, wakazi wa Kanada walibaki upande wa Uingereza. Hivyo Kanada iliendelea chini ya Uingereza ikaitwa "Amerika ya Kaskazini ya Kiingereza".

Mwaka 1841 sehemu mbalimbali ziliunganishwa kama koloni moja la Kanada.

Mwaka 1867 Bunge la Uingereza lilikubali sheria iliyounda Shirikisho la Kanada lenya majimbo manne ya Ontario, Quebec, Nova Scotia na New Brunswick. Sasa Kanada ilikuwa nchi ya kujitawala chini ya Mfalme wa Uingereza.

Kujengwa kwa reli kati ya Atlantiki na Pasiki na kufika kwa wahamiaji kutoka Ulaya kuliimarisha nchi mpya. Majimbo mapya yaliundwa hadi kufika majimbo 10 na maeneo matatu chini ya shirikisho jinsi ilivyo sasa.

Kanada ilishikamana na Uingereza katika vita kuu za dunia zote mbili. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia nchi ilionekana kama nchi ya pekee iliyotoa sahihi yake yenyewe pamoja na Uingereza chini ya mkataba wa Versailles.

Mwaka 1927 ilipeleka balozi wa kwanza huko Marekani.

Uhuru kamili ulipatikana mwaka 1982. Hadi leo malkia wa Uingereza ni mkuu wa dola akiwakilishwa na gavana mkuu.

Zaidi ya nusu ya wakazi huishi katika miji mikubwa zaidi. Mji mkubwa ni Toronto yenye wakazi milioni 5.6 ambayo ni bandari kwenye Ziwa Ontario na kitovu cha viwanda. Montreal ni mji wa biashara wenye milioni 3.27.

Miji mingine mikubwa ni (idadi ya wakazi katika mabano):

Ramani ya Kanada na majimbo yake
  1. Alberta - AB
  2. British Columbia - BC
  3. Manitoba - MB
  4. New Brunswick - (Kiingereza) NB (Kifaransa) NB
  5. Newfoundland and Labrador - NL
  6. Northwest Territories - NT
  7. Nova Scotia - NS
  8. Nunavut - NU
  9. Ontario - (Kiingereza) ON (Kifaransa) ON
  10. Prince Edward Island - PE
  11. Quebec - (Kifaransa) PQ
  12. Saskatchewan - SK
  13. Yukon - YU

Watu na lugha

[hariri | hariri chanzo]

Wakazi asilia wa Kanada ni Waindio na Waeskimo walioingia Amerika kutoka Siberia (Asia). Hakuna hakika walikuwa wangapi wakati wa kufika kwa Wazungu lakini idadi yao ilipungua haraka kwa sababu watu kutoka Ulaya walileta magonjwa ya kuambukizwa na wenyeji walikosa kingamwili dhidi yake. Leo hii idadi imeongezeka tena kiasi: kuna takriban milioni 1.4 au asilimia 4.9 za Wakanada wote.

Wahamiaji kutoka Ùfaransa walitangulia, wakifuatwa na Waingereza, Waskoti na Waeire. Wengine walifuata kutoka Ujerumani, Italia, Urusi, Ukraine, Poland na penginepo. Kwa jumla wenye asili ya Ulaya ni 69.8%.

Katika miaka ya nyuma wahamiaji wengi wamefika kutoka China na Asia. Wahindi wengi waliofukuzwa Uganda wamehamia Kanada pia. Kwa sasa wenye asili ya Asia ni 19.3%, wakati wenye asili ya Afrika ni 3.8%. Wakazi asili ni 6.1%

Lugha rasmi ni Kiingereza (lugha mama ya 54%) na Kifaransa (19%). Lakini zinatambulika pia lugha 9 za kijimbo.

Upande wa dini, kadiri ya sensa ya mwaka 2021, kati ya wakazi 53.3% ni Wakristo. Kati yao, madhehebu makubwa ni: Wakatoliki (29.9%), Kanisa la Muungano la Kanada (3.3%) na Anglikana (3.1%). Waislamu ni 4.9%, Wahindu 2.3%, Singasinga 2.1%, Wabuddha 1.0%, Wayahudi 0.9%. Kwa jumla dini zinarudi nyuma, hazithaminiwi, tena tayari 34.6% hawana dini yoyote.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Taarifa za jumla
Serikali
Utalii
Masomo
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.