Siberia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Eneo la Siberia: nyekundu yote; Jimbo la Siberia ndani ya shirikisho la Urusi: nyekundu nyeusi

Siberia (Kirusi: Сиби́рь, Sibir; Kitartari: Seber) ni eneo kubwa katika mashariki ya Urusi.

Maana ya Siberia[hariri | hariri chanzo]

Kuna namna mbalimbali ya kutaja mipaka ya "Siberia".

  • Kijiografia mara nyingi "Siberia" yamaanisha sehemu ya Kiasia ya Urusi. Kwa maana hii eneo lake ni kubwa sana ni linajumlisha Asia ya Kaskazini yote.
  • Kisiasa ni sehemu tu ya eneo hili (tazama ramani). Kwa maana hii Siberia ni jimbo la shirikisho la Urusi. Kisiasa Ural na Mashariki ya Mbali ni majimbo ya pekee.

Mipaka ya Siberia ya kijiografia ni safu ya milima ya Ural upande wa magharibi, bahari ya Aktika kwa kaskazini, Pasifiki katika Mashariki na nchi za Kazakhstan, Mongolia na Uchina upande wa kusini. Siberia ni zaidi ya nusu la eneo la Urusi wote. Eneo lote ni kilomita za mraba milioni 9.6 ambayo ni karibu sawa na Ulaya yote (milioni 10.6 km²).

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Idadi ya wakazi ni ndogo kuna milioni 23 pekee. Walio wengi ni Warusi (79%) wanaoishi mjini. Wakazi asilia (21%) ni vikundi vingi vidogo; walio wengi ni wasemaji wa lugha za Kituruki. Utamaduni wao ulikuwa uvindaji na ufugaji lakini ni wachache tu wanaoendelea hivyo.

Hali ya hewa[hariri | hariri chanzo]

Hali ya hewa ya Siberia ni kali sana. Kipindi cha joto pana joto kali hadi +40 °C lakini kipindi cha baridi halijoto hushuka chini hadi -67 °C. Kijiji cha Oymyakon (katika jamhuri ya Sakha) ni mahali baridi duniani; -71.2 °C zilipimwa hapa.

Kipindi cha baridi ni kirefu, kipindi cha joto ni kifupi. Sehemu kubwa ya Siberia inafunikwa na theluji kwa muda wa miezi tisa kila mwaka. Hivyo kilimo kinawezekana katika kanda nyembamba la kusini. Sehemu kubwa nchi imefunikwa na misitu. Lakini maeneo baridi sana ya kaskazini hapana miti tena ni manyasi na majani tu.


Mito na maziwa[hariri | hariri chanzo]

Siberia ina mito mingi mikubwa. Lakini huganda kabisa wakati wa baridi yaani kwa sehemu kubwa wa mwaka isipokuwa ile katika kusini.

Milima[hariri | hariri chanzo]

Flag-map of Russia.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Siberia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.