Waeskimo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wanawake na mtoto wa Kieskimo katika mavazi ya kiutamaduni (1999).

Waeskimo (kwa lugha yao wanaitwa Inuit) ni watu wanaotokana moja kwa moja na waliokuwa wenyeji wa kaskazini mwa Amerika kabla ya bara hilo kufikiwa na Christopher Columbus kutoka Ulaya (1492).

Asili[hariri | hariri chanzo]

Ramani ya uenezi wa binadamu duniani[1]

Utafiti uliofanywa kwa muda mrefu na kwa njia mbalimbali umekadiria kwamba mababu wa wakazi asilia wa Amerika walioenea hadi Amerika Kusini wakitokea Asia kaskazini mashariki miaka 14500 KK.

Inadhaniwa kwamba hao mababu waliishi muda mrefu na kuzaliana bila mawasiliano na binadamu wengine, labda katika eneo ambalo leo limefunikwa na maji kwenye mlangobahari wa Bering. Inakadiriwa DNA yao ilitokana na ile ya Waasia mashariki (2/3) na Waeurasia (1/3).

Baada ya kuingia na kusambaa katika bara hilo, lugha na utamaduni vilizidi kutofautiana. Waeskimo walijitofautisha na Waaleuti miaka 4,000 iliyopita. Kutoka Alaska magharibi walienea mashariki kuanzia miaka 1,000 iliyopita.

Hali ya sasa[hariri | hariri chanzo]

Idadi yao inaweza kuwa 155,000 wengi wao wakiishi Kanada na Greenland, lakini pia Alaska na Denmark.

Lugha yao ni ya jamii ya lugha za Kieskimo-Kialeuti.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Göran Burenhult: Die ersten Menschen, Weltbild Verlag, 2000. ISBN 3-8289-0741-5

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waeskimo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.