John Cabot
John Cabot (kwa Kiitalia: Giovanni Caboto, 1450 - 1499) alikuwa baharia na mpelelezi kutoka nchini Italia. [1]
Mnamo 1497, akisafiri kuelekea magharibi kutoka Uingereza katika meli yake Mathew, aliingia katika kile alichodhani ni Asia. Hali halisi alikuwa amefika Amerika Kaskazini, katika maeneo ambayo sasa ni mashariki mwa Kanada, aliyodai kwa ajili ya Mfalme Henry VII wa Uingereza. [2]. Cabot alifariki huko England mnamo 1499. [3]
Miaka ya kwanza
[hariri | hariri chanzo]Giovanni Caboto (jina lake la Kiitalia) labda alizaliwa huko Genova mnamo 1450. [4] Hakuna habari nyingi zilizoandikwa juu ya maisha yake ya mapema. Alipokuwa bado mchanga, familia yake ilihamia Venezia. Venezia wakati huo ilikuwa bandari muhimu zaidi katika Ulaya yote. Kwa kukua huko alijifunza mengi juu ya meli na bahari. Cabot alikua baharia bora. Baba yake alikuwa mfanyabiashara akamfundisha Giovanni (John) yote juu ya biashara ya viungo.
Mnamo 1482 Cabot alimwoa mke wake Mattea[4]. Walikuwa na wana watatu ambao wote walisafiri na baba yao alipoendelea kuwa mfanyabiashara na kusafiri mbali. [5]
Mnamo 1490 aliondoka Venezia akahamia Hispania. Huko alijaribu kupata kibali cha safari ya kufika China, akiamini kwamba Kolumbus - aliyerudi siku zile kutoka safari yake ya "Uhindini" (hali halisi visiwa vya Karibi vya Amerika ya Kati) - alikuwa hajafika Asia bado. Hatimaye Cabot alihamia Bristol, Uingereza, mnamo 1496 alipopeleka mipango yake mbele ya mfalme wa Uingereza.
Safari ya kwenda Amerika Kaskazini
[hariri | hariri chanzo]Mabaharia kutoka Bristol waliwahi kufanya safari ndefu katika Atlantiki kabla ya kufika kwa Cabot. Cabot aliamini kwamba njia kwenye Atlantiki ya Kaskazini hadi China ingekuwa fupi kuliko kule ambako Kolumbus aliwahi kusafiri. Baada ya kupata kibali cha mfalme, Cabot alisafiri hatimaye mwaka 1497 akitumia jahazi 1 na mabaharia 20 akavuka Bahari ya Atlantiki Kaskazini kwa muda wa wiki saba hadi kufikia kisiwa cha Newfoundland. [6] Wakati wa safari waliona idadi kubwa ya samaki wa Chewa. Wavuvi Waingereza walimfuata baadaye kuvuna samaki hao kwenye Grand Banks ya Newfoundland.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "John Cabot Biography Explorer (c. 1450–c. 1499)". Bio/A&E Television Networks, LLC. Iliwekwa mnamo 16 Desemba 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "John Cabot". History/A&E Television Networks, LLC. Iliwekwa mnamo 16 Desemba 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "John Cabot: Explorer". EnchantedLearning.com. Iliwekwa mnamo 16 Desemba 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 Robin S. Doak, Cabot: John Cabot and the Journey to North America (Minneapolis, MN: Compass Point Books, 2003), pp. 4–12
- ↑ "John Cabot - c.1450 - 1498". BBC. Iliwekwa mnamo 16 Desemba 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Doug Sylvester, World Explorers (San Diego: Classroom Complete Press Ltd, 1997), p. 36