Venezia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Venezia
Collage Venezia.jpg
Venezia is located in Italia
Venezia
Venezia
Mahali pa Venezia katika Italia
Viwianishi: 45°26′00″N 12°20′00″E / 45.433333°N 12.333333°E / 45.433333; 12.333333
Nchi Italia
Mkoa Veneto
Wilaya Venizia
Idadi ya wakazi
 - 270,660
Tovuti: http://www.comune.venezia.it/
Maboti ya gondola mjini Venezia
Kitovu cha Venezia kwa jicho la ndege
Mfereji mkuu wa "Canale Grande"
Mifereji ni kama barabara

Venezia (pia: Venisi, Venice) ni mji wa Italia na makao makuu ya mkoa wa Veneto kwenye kaskazini-mashariki ya nchi.

Venezia ni mji wa pwani uliojengwa kwenye visiwa vidogo 117 ndani wa wamba la Venezia. Visiwa hivi vinakaa karibu kiasi ya kwamba madaraja 400 yanaunganisha mifereji kati yao. Mifereji ndani ya mji ni kama barabara na sehemu kubwa ya usafiri ni kwa maboti madogo.

Mji umekua kupitia eneo la visiwa tu na mwaka 2006 wakazi 269,000 walihesabiwa; 92,000 waliishi visiwani na wengine barani.

Venezia ni mji wa kale mwenye umri wa karibu miaka 1,500. Ilikuwa jamhuri ya kujitawala kabisa kwa karne nyingi hadi 1797 ilipovamiwa na Napoleon na kuunganishwa kwanza na Italia na baadaye na Austria. Tangu 1866 imekuwa sehemu ya Italia. Jamhuri ya Venezia ilikuwa dola lenye nguvu katika Mediteranea kwa sababu ilikuwa na manowari nyingi na vituo vya kijeshi kwenye visiwa vingi vya Mediteranea. Msingi wa nguvu yake ilikuwa biashara ya baharini na utajiri wake. Venezia ilikuwa kiungo wa kibiashara kati ya Uaya ya kikristo na dunia ya Kiislamu.

Kutokana na historia hii ya utajiri mji umejaa majengo mazuri na kazi za sanaa zinazovuta watalii mamilioni kila mwaka kutoka kila upande wa dunia. Venezia iko katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Italy looking like the flag.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Venezia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: